Kuhusu majoka makubwa yapandishwayo angani kutoka kwenye maji

Kuhusu majoka makubwa yapandishwayo angani kutoka kwenye maji

Kuna uzi humu una zaidi ya kurasa 27..Mod unganisheni hii tusiumizane vichwa.
 
Kwa hiyo uchawi wa wavuvi huzuia hili jambo la kijiografia??

If yes basi nguvu za giza ni kali na zina uwezo pia wa kufanya hicho mnachobishia hapa, kupandisha nyoka waliofungwa minyororo huko juu
Wewe bibi upo? Nmekumis[emoji8]
 
Kwa hiyo uchawi wa wavuvi huzuia hili jambo la kijiografia??

If yes basi nguvu za giza ni kali na zina uwezo pia wa kufanya hicho mnachobishia hapa, kupandisha nyoka waliofungwa minyororo huko juu
Mkuu sio nyoka NI aina flani hivi ya kimbunga kinaigwa MSOKE au kisulisuli

Na kuhusu wavuvi kuuzuia NI kweli na hufundishwa MVUVI yeyote kabla hajaanza kazi ya ziwani au baharini!

Na Kuna njia nyingi Sana za kuzuia hicho kimbunga ( joka )

Mfano kikianza Kama umekiona kwa mbali na kimeshaungana na kinaelekea kuja mliko njia mojawapo Kama Kuna mmja wenu hajatailiwa anatakiwa avue nguo na aonyeshe govi lake upepo unapotokea

Kimbunga hicho hukatika katikati yaani Cha juu kitaenda juu na Cha chini kitabaki chini!

Njia NYINGINE Kama kimetokea mko ziwani na wote hamna magovi unachukua maji kwenye sabuzo unainua juu kisha unayamwaga kabla hayajaisha unapitisha kisu katikati ya hayo maji mfano wa kuyakata na wenyewe utakatika hivyo hivyo

Na NYINGINE nyingi

Hata Kasia unaweza kutumia Kama kisu!
 
Majoka hayo hupandishwa kutoka kwenye maji iwe ya bahari, ziwa au mito na huonekana yamefungwa minyororo mikubwa sana inayopitiliza kwenye mawingu. Ni matukio nadra lakini huweza kushuhudiwa hasa na watu wa mahali fulani.

Vimbunga vya kwenye maji vinajulikana na wala mtu hawezi kuvichanganya na matukio ya nyoka kupandishwa angani. Matukio hayo yapo mengi na hutokea baharini, ziwani au kwenye mito. Sehemu hizi zote ni makazi ya ufalme wa shetani wa kwenye maji au marine spiritual world. Ufalme wa shetani una falme ndogo ndogo nyingi sana ila zipo kubwa 4: uflame wa anga, ufalme wa ardhi, ufalme wa moto na ufalme wa maji.

Ufalme wa maji ndio mkubwa zaidi ya falme zote za shetani, takribani 80% ya ufalme wa shetani ni marime kingdom. Na ufalme wa maji una mashetani yenye nguvu zaidi kuliko falme nyingine. Na watu wengi wanaopagawa na mapepo huwa mara nyingi yanatoka ufalme wa maji. Majini haya hujilikana kama water mermaids, mermaids, Africa sehemu nyingi hasa Nigeria huita water mammy au kwa wengine huita water sirens. Hapa Tanzania roho za ufalme huu huweza kujitokeza has baharini na hujulikama kama nguva.

Malkia wa ufalme wa maji hujulikana kwa kiingereza kama queen of the coast, yaani malkia wa mwambao. Zile roho zenye nguvu sana za ushawishi katika mambo yote na hasa mambo ya mapenzi au uongo wowote (seduction) huwa zinatoka katika ufalme wa maji, roho hizi huitwa seducing spirits ambazo zinaongozwa na mkuu wao aitwae Jezebel. Huyu ndio yule kahaba aketiye juu ya maji mengi na kuwapotosha mataifa. Maji mengi biblia inasema yanamaanisha watu, makundi, mataifa na makabila (Ufunuo 17:15).

Sasa kwa habari ya majoka nimefuatilia jambo hili na nimepata habari nyingi tu. Huwa majoka makubwa sana huonekana yakipandishwa kutoka kwenye maji huku yakiwa yamefungwa minyororo mikubwa sana kwani majoka hayo ni makubwa ajabu unene wake huwa kama mbuyu mkubwa. Likiwa linapandishwa angani utaona lipo juu hewani na mnyororo mkubwa umelifunga na mnyororo huo huishia mawinguni. Mingyororo hivyo hufanya sauti kubwa kamba ilivyo minyororo lakini utadhani ni kengele kubwa zinalia. Watu hujaribu kuona nani analipandisha joka hilo lakini macho yao huishia kuona hadi mawinguni tu na joka hilo hupandishwa hadi kutokomea mawinguni.

Tafsiri yake ni kwamba majoka hayo huwa wakuu wa mizimu au familiar spirits za ufalme wa maji. Mnajua kuwa mizimu ni mapepo au majini mahalia. Yaani mizimu huwa ni mapepo ya watu ama wa ukoo fulani, kabila au hata nchi flani na mizimu huwa ndio roho zinazojishughulisha na watu hao katika mambo yote ya ufalme wa shetani. Mizimu hujua mengi kuhusu kabila au familia na inakuwa na nguvu kubwa kwa watu wale kwani inaabudiwa kama mungu na pia imetolewa sadaka nyingi na kwa miaka mingi sana.

Kwa wakati fulani Mungu kwa uwezo wake na pia kutokana na mabadiliko ya mila na desturi za watu fulani au kutokana na sala za waana wa Mungu, mizimu hiyo hupoteza nguvu au huondolewa na kupelekwa mahali pa kusubiri hukumu ya mwisho. Mungu huweza kuacha baadhi ya mambo hayo kuonekana na wanadamu na mara nyingi huwa watu wa kabila ama familia husika waliokuwa wakitumikishwa na mzimu huo. Matukio hayo nimeyafuatilia Morogoro lakini yapo sehemu zote na yapo katika level ya familia, ukoo, kabila, nchi, bara au dunia nzima.
Ni kweli kabisa eneo flani mikoa ya kusini alioneksna joka mkubwa na wazee wakisimulia eneo moja akitokea pembezeoni mwa mji akielekea baharini uku akiwa amefungwa minyororo. ama hakika Mungu angetupa kuyaona hayo yote tungekufa kabla ya wakati.
 
Mkuu sio nyoka NI aina flani hivi ya kimbunga kinaigwa MSOKE au kisulisuli

Na kuhusu wavuvi kuuzuia NI kweli na hufundishwa MVUVI yeyote kabla hajaanza kazi ya ziwani au baharini!

Na Kuna njia nyingi Sana za kuzuia hicho kimbunga ( joka )

Mfano kikianza Kama umekiona kwa mbali na kimeshaungana na kinaelekea kuja mliko njia mojawapo Kama Kuna mmja wenu hajatailiwa anatakiwa avue nguo na aonyeshe govi lake upepo unapotokea

Kimbunga hicho hukatika katikati yaani Cha juu kitaenda juu na Cha chini kitabaki chini!

Njia NYINGINE Kama kimetokea mko ziwani na wote hamna magovi unachukua maji kwenye sabuzo unainua juu kisha unayamwaga kabla hayajaisha unapitisha kisu katikati ya hayo maji mfano wa kuyakata na wenyewe utakatika hivyo hivyo

Na NYINGINE nyingi

Hata Kasia unaweza kutumia Kama kisu!
Ngoja nicheke tu
 
moro sehemu gani mkuu,au kule korelo

Sent using Jamii Forums mobile app
Ulizia kule anapotoka chifu Kingalu, huyo mdudu akiwa anapandishwa juu huwa inapiga mvua ya kufa mtu milimani huko....vigoma na filimbi zinasikika na kama ni usiku miale ya moto inaonekana.
Wenyeji wana kwambia joka anapalizwa, huyo joka huleta mafuriko sana huko Morogoro.
Wenyeji wanajua sana sema wamepiga kimya.
 
Mkuu sio nyoka NI aina flani hivi ya kimbunga kinaigwa MSOKE au kisulisuli

Na kuhusu wavuvi kuuzuia NI kweli na hufundishwa MVUVI yeyote kabla hajaanza kazi ya ziwani au baharini!

Na Kuna njia nyingi Sana za kuzuia hicho kimbunga ( joka )

Mfano kikianza Kama umekiona kwa mbali na kimeshaungana na kinaelekea kuja mliko njia mojawapo Kama Kuna mmja wenu hajatailiwa anatakiwa avue nguo na aonyeshe govi lake upepo unapotokea

Kimbunga hicho hukatika katikati yaani Cha juu kitaenda juu na Cha chini kitabaki chini!

Njia NYINGINE Kama kimetokea mko ziwani na wote hamna magovi unachukua maji kwenye sabuzo unainua juu kisha unayamwaga kabla hayajaisha unapitisha kisu katikati ya hayo maji mfano wa kuyakata na wenyewe utakatika hivyo hivyo

Na NYINGINE nyingi

Hata Kasia unaweza kutumia Kama kisu!
Kumbe magovi nayo yanafaida huko majini[emoji1]
 
Sasa tuamini kipi wengine wanadai ni mambo ya kigeografia wengine wanadai ni mashetani[emoji849]
 
Back
Top Bottom