Kuhusu majoka makubwa yapandishwayo angani kutoka kwenye maji

Kuna uzi humu una zaidi ya kurasa 27..Mod unganisheni hii tusiumizane vichwa.
 
Kwa hiyo uchawi wa wavuvi huzuia hili jambo la kijiografia??

If yes basi nguvu za giza ni kali na zina uwezo pia wa kufanya hicho mnachobishia hapa, kupandisha nyoka waliofungwa minyororo huko juu
Wewe bibi upo? Nmekumis[emoji8]
 
Kwa hiyo uchawi wa wavuvi huzuia hili jambo la kijiografia??

If yes basi nguvu za giza ni kali na zina uwezo pia wa kufanya hicho mnachobishia hapa, kupandisha nyoka waliofungwa minyororo huko juu
Mkuu sio nyoka NI aina flani hivi ya kimbunga kinaigwa MSOKE au kisulisuli

Na kuhusu wavuvi kuuzuia NI kweli na hufundishwa MVUVI yeyote kabla hajaanza kazi ya ziwani au baharini!

Na Kuna njia nyingi Sana za kuzuia hicho kimbunga ( joka )

Mfano kikianza Kama umekiona kwa mbali na kimeshaungana na kinaelekea kuja mliko njia mojawapo Kama Kuna mmja wenu hajatailiwa anatakiwa avue nguo na aonyeshe govi lake upepo unapotokea

Kimbunga hicho hukatika katikati yaani Cha juu kitaenda juu na Cha chini kitabaki chini!

Njia NYINGINE Kama kimetokea mko ziwani na wote hamna magovi unachukua maji kwenye sabuzo unainua juu kisha unayamwaga kabla hayajaisha unapitisha kisu katikati ya hayo maji mfano wa kuyakata na wenyewe utakatika hivyo hivyo

Na NYINGINE nyingi

Hata Kasia unaweza kutumia Kama kisu!
 
Ni kweli kabisa eneo flani mikoa ya kusini alioneksna joka mkubwa na wazee wakisimulia eneo moja akitokea pembezeoni mwa mji akielekea baharini uku akiwa amefungwa minyororo. ama hakika Mungu angetupa kuyaona hayo yote tungekufa kabla ya wakati.
 
Ngoja nicheke tu
 
moro sehemu gani mkuu,au kule korelo

Sent using Jamii Forums mobile app
Ulizia kule anapotoka chifu Kingalu, huyo mdudu akiwa anapandishwa juu huwa inapiga mvua ya kufa mtu milimani huko....vigoma na filimbi zinasikika na kama ni usiku miale ya moto inaonekana.
Wenyeji wana kwambia joka anapalizwa, huyo joka huleta mafuriko sana huko Morogoro.
Wenyeji wanajua sana sema wamepiga kimya.
 
Kumbe magovi nayo yanafaida huko majini[emoji1]
 
Sasa tuamini kipi wengine wanadai ni mambo ya kigeografia wengine wanadai ni mashetani[emoji849]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…