Mlalamikaji daily
JF-Expert Member
- May 19, 2014
- 1,018
- 2,366
Hapo zamani za kale kwenye kijiji cha msituni kulikuwa na mzee mmoja aliyejulikana kama Mzee Filipo..
Alikuwa mrefu, mnene mweusi..
Alitisha sana!
Kutokana na mwonekano wake alitawala kijiji kizima na hata uchaguzi ulipokuwa ukifanyika ilikuwa kama danganya toto Tu! Kwani siku chache kabla ya uchaguzi mzee Filipo alihakikisha wagombea wenzake aidha wanajitoa au wanamuunga mkono yeye, na wale waliojifanya wagumu waliona cha mtema kuni na wengine iliwabidi kuhama nje ya kijiji!
Basi miaka ikapita na mzee Filipo pole pole akaanza kupoteza ushawishi kama waswahili wasemavyo hakuna marefu yasiyo na ncha!
Lakini kwakuwa mzee Filipo alishaamua kijiji ni chake hakutaka kusoma alama za nyakati basi akaendelea kununua wanakijiji na nyimbo za kumsifia na kumpongeza kila kona zikaanza kusikika...
" Mzee Filipo ni nomaa...Mzee Filipo atawale milele, Mzee Filipo apite bila kupingwa n.k"
Yaani mpaka chekechea wakaanza kuimba nyimbo za mzee Filipo..
Tena unaambiwa hata kipindi cha uchaguzi kilikua bado!
Lakini mzee Filipo alishinda tayari uchaguzi!
Basi ikatokea siku moja ikabidi kuwe na chakula cha kitaifa ambapo kila familia ilibidi ipike chakula chake na baadae chakula kile kitakachoonekana kuwa kitamu zaidi ndio kinatangazwa kuwa chakula cha kitaifa!
Na familia iliyotoa chakula kitamu zaidi inapewa kuongoza mashamba na mito yote pale kijijini!
Basi familia ya mzee Filipo kila mwaka yenyewe ilikuwa inashinda maana kuanzia wapishi na wale wanaoonja chakula kuingia kwenye mashindano hayo alikuwa anawateua yeye mwenyewe mzee Filipo!
Sasa kwa kupenda sifa, kwenye mashindano ya mwaka ule mzee Filipo akasema wote wanaotaka kushindana waende na kwamba safari hii majaji hawatakuwa wale wa miaka yote bali watachaguliwa kutoka familia zenyewe...
#inaendelea Part 2 kwenye komenti