KUHUSU MARIDHIANO PART 2
Basi kuna wanakijiji ambao walikuwa wamehama kumuogopa mzee Filipo wakaitwa warudi kijijini wajenge kijiji chao wengine wakarudi wengine wakakataa kurudi..
Basi michujo ikaanza na baadae akaonekana kuna mzee Paulo alikuwa na nguvu kubwa ya ushawishi na anaweza kujenga hoja..
Taarifa zikamfikia Mzee Filipo..
Mzee Paulo alisema kwamba yupo tayari yeye na familia yake kuingia kwenye mashindano lakini kamati ya mashindano ibadilike isiwe ile ambayo mzee Filipo atashinda hata kabla ya mashindano kuanza!
Taarifa zikamfikia Mzee Filipo..
Akawaita watu wake wakaja na fix..
Wakasema kwamba eti kwa kipindi kile majaji wanaoteua sio wale wa kipindi kile ...
Yaani ipo hivi mwanzo ni wazazi ndio waliokuwa wanateua washiriki na washindi...
Lakini wakadai kwamba kwa sasa wale wazazi hawachagui tena isipokuwa wanachagua watoto wao wakafanye iyo kazi kwa niaba yao..
Basi Mzee Paulo akasema huo ni ujinga na huo ni uongo hakuna mashindano hapo.. akajitoa!
Huku mzee Filipo akatengeneza familia kibao na mashindano yakaendelea na familia zote zilizoshiriki pamoja na mzee Filipo kazi yao ikawa kumpiga vijembe mzee Paulo..
Mara ametia mpira kwapani, mara ameogopa amejua atashindwa n.k.
Mpaka siku chache kabla ya mashindano akasema Mzee Paulo anataka kukwamisha mashindano na akamtia ndani!
Na familia nyingine zikaendelea na mchakato..
Basi watoto wa mzee Paulo wakasema sio busara watu kuingia kwenye mashindano ya chakula na mzee wao akiwa ndani..
Wakae kwanza watengeneze sheria na ikibidi safari hii majaji wa kamati watoke kijiji jirani!!
Weee
Mzee Filipo akasema NEVER!!
Mashindano yanafanyika!!
Baadhi ya wanakijiji sasa wakaanza kuhoji mbona mashindano ya mwaka huu yamekuwa hivi?
Kwanini mzee Filipo asikubali tu kukaa na wenzake wakatengeneza sheria si atashinda tu kama miaka yote?
Basi pole pole kila aliyeanza kuhoji kuhusu uhalali wa mashindano akaanza kupotea mmoja baada ya mwingine...
Na hatimaye mashindano yakafanyika familia ya mzee Filipo ikashinda kwa 98%!!
Basi baada ya USHINDI
sasa mzee Filipo akasema
Haya sasa NJOONI TUKAE MEZANI tujadiliane kuhusu mashindano yajayo!!