Kuhusu Matibabu kutoka kwa Mwajiri

Kuhusu Matibabu kutoka kwa Mwajiri

mischa

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
368
Reaction score
177
Nimeajiriwa kwenye shirika la kigeni au binafsi(sio serikalini),

Mkataba nnao wa mwaka renewable kila mwaka,lakini kwenye matibabu mwajiri hunitibu kupitia hospitali moja tu,

Yaani shirika limeteua hospitali mmoja ambayo wafanyakazi hutibiwa pale tu tena OPD ukilazwa garama ni zako(hawalipi IN-Patient),

Na matibabu ni mm tu hawaangalii familia yangu,maana nikiugua mkoani nitumie garama yangu.

Je,Sheria ya kazi inasemaje kuhusu hili??

Ni wapi serikalini twaweza shitaki hili suala??
 
sijajua hasa mkataba wako wa kazi unasemaje kuhusu matibabu. Je kampuni linawalipia bima ya afya? kwa ulivyoeleza naona mwajiri wako anajitolea tu kama msaada (kuwatibia) hata hivyo kama unaona unaonewa una haki ya kumshtaki mwajiri wako, unatakiwa kuanzia baraza la usuluhishi (CMA)
 
Mkataba wa kazi kipengele cha matibabu yeye mwajiri kainisha tu kwamba Ofisi itakugharamikia matibabu hospital X na matibabu hayo ni OPD tu sio In patient wala sio familia ni ww tu.
Naona si haki maana shirika kubwa tu kwann wasitupatie bima ya afya?
Maanake nikiendaa mkoani nisiumwe?ama nikiumwa najigharamia..
 
Kama ameainisha (amewka wazi) na wew uliusoma na kuukubali sidhani kama unachance ya kumuhukumu vnginevyo hata hyo kaz utaikosa.
 
Naona kuna mischief sehemu! Mwajiri wako hachangii kwenye mfuko wa bima ya afya (NHIF)?
 
Naona kuna mischief sehemu! Mwajiri wako hachangii kwenye mfuko wa bima ya afya (NHIF)?

Hapana hachangii kwenye mfuko wa bima,shirika ni secta binafsi yeye anasema hawana fungu la ku cover bima kwa wafanyakazi wote.
 
Kama ameainisha (amewka wazi) na wew uliusoma na kuukubali sidhani kama unachance ya kumuhukumu vnginevyo hata hyo kaz utaikosa.

Sawa,lakini swali langu linakuja Je sheria ya nchi inasemaje kuhusu bima ya afya kwa wafanyakazi?kuna kifungu chochote kitakachombana huyu mwajiri wangu?
 
Bima ya afya ni lazima kama ilivyo kwa mifuko mingine ya hifadhi ya jamii (bila shaka tayari umeunganishwa na mfuko mmoja wapo). Kumbuka NHIF haichangiwi na Mwajiri bali Mwajiriwa, otherwise kama tayari Mwajiri wenu aliwaunganisha katika bima nyingine yenye sera mbovu kiasi hicho
 
Tumeunganishwa kwenye mfuko wa hifadhi wa ppf,ila hatuna kabisa mfuko wa bima.
 
Sawa,lakini swali langu linakuja Je sheria ya nchi inasemaje kuhusu bima ya afya kwa wafanyakazi?kuna kifungu chochote kitakachombana huyu mwajiri wangu?

Bima ya afya kwa tanzania sio sheria kwamba mwajiri anabanwa na sheria kumpatia mwajiriwa...kama ilivyo GPA na worksman compesation au bima ya gari...

So mwajiri binafsi(private sector)akikupa bima ya afya ni favor yake tuu
 
Ni kwl, mimi nipo acacia northmara gold mine ,mwajr wetu hutupatia hutuma ya matibabu lakn hmu ndam kuna kampuni za kizawa hazitoi favor ya matibabu.
 
Ivi sheria inazungumziaje kuhusu ongezeko la mshahara kwa mwaka haswa sekta binafsi? Nasema hvyo kwa 7bu mpka sasa kuna mgogoro wa chnchn kat ya (NUMET) chama cha wafanyaz na mgodi! Naombwa kufahamishwa
 
Sawa,lakini swali langu linakuja Je sheria ya nchi inasemaje kuhusu bima ya afya kwa wafanyakazi?kuna kifungu chochote kitakachombana huyu mwajiri wangu?

Kuna baadhi ya waajiri wanawaunganisha watumishi wao katika mifumo fulani ya kimatibabu kama medex na mengine, lakin hakuna sheria inayo mlazimisha kabisa mwajiri akutibu isipokua ile ya kusema mwajiri atatengeneza mazingira ya mwajiriwa wake kupata matibabu hapo ndio utaona watumishi hasa wa gvt wanaingizwa ktk NHIF moja kwa moja kwa gharama zao.
 
Back
Top Bottom