Kuhusu NMB wakala

Nyamboboy

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2017
Posts
362
Reaction score
454
Habari za wakati huu.
Nianze kwa kukiri kuwa mimi ni wakala wa NMB,Nataka kutoa malalamiko yangu kwa Bank hii kuhusu kamisheni tunazopewa kwa kazi ya uwakala ukilinganisha na hela wanayokatwa wateja wetu.Nashindwa kuelewa kwa nini bank hii inawakata wateja hela kutwa wakiwa wanatoa pesa ila sisi mawakala tunaambulia fedha ndogo sana.Imefikia mda bank hii haioni kazi kubwa tunayoifanya sisi mawakala.Tunanunua machine za POSS milioni moja laki moja na elfu sitini(Tsh1160000) tunaweka mitaji yetu mikubwa hii yote kwa ajili ya kuifaidisha Bank alafu sisi tunabaki bila chochote.NMB na bank nyingine liangalieni hili tofauti na hapo mawakala wataachana na kazi hii.Asante
 
Kuna agent wao mmoja ananishauri nichukue mashine , embu nipe uhalisia kiongozi.
 
Mnabaki bila chochote vipi Mkuu!?? Kwani commission yako ni asilimia ngapi ya mauzo/miamala !?? Je wanakulipa nje ya makubaliano ya Mkataba!??
 
Eleza vizuri mnabakije bila chochote zile asilimia za commission hauzipati kama inavyotakiwa au?
 
Kakimbia Uzi wake!!




KAZI ni kipimo cha UTU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…