Kuhusu sakata la mkataba wa bandari, safari hii lazima kelele za chura zimzuie mtu kuteka maji

Kuhusu sakata la mkataba wa bandari, safari hii lazima kelele za chura zimzuie mtu kuteka maji

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
13,897
Reaction score
18,477
Natoa woto kwa watanzania wote kwa ujumla, safari hii watanzania tushikamane kupiga makelele kila kona hadi yafanyike mageuzi makubwa kuhusu mtazamo na mawazo ya viongozi wetu kuhusiana na mkataba mbovu sana wa bandari za Tanzania!

Kwa ujumla wetu safari hii "kelele za chura lazima zimzuie mtu kuchota maji”

Kuna msemo pendwa huko kwenye chama cha kijani kuwa "makelele ya chura hayawezi kumzuia mtu kuchota maji". Msemo huu hutumika kwenye muktadha wa watawala kuziba masikio yao kuhusu malalamiko ya wanachi kuhusu mambo mbali mbali yasiyokuwa na maslahi kwa Taifa.

Naomba huu uzi ukimbie kwa kasi ya mwanga na ujae kelele hadi wahusika wasiweze kula wala kulala na tuwasemee kwa Mungu pia!!

Viongozi wetu tunawapenda na tunawaheshimu lakini katika hili tunasema HAPANA!!
 
Kuna kitu hakipo sawa kuhusu uwekezaji huu. Kwanini wanaulazimisha ilihali wenye kutafutiwa fedha kwa ajili ya maendeleo yao wamezikataa?
Ni busara kutumia hekima kidogo tu hao wanaosukumwa na mwekezaji watambue kuwa wananchi hawawahitaji hao wawekezaji wao hiyo waachane nae na bandari iendeshwe na kusimamiwa na serikali kwa kuwekeza mtaji, vifaa na teknolojia. Ni simple tu hawahitaji kutumia maguvu kumkinga na kumtetea mwekezaji anayepingwa Kila alikowekeza!
 
Ngoja tuone hadi mwisho wa hii issue, yaani bunge lipitishe halafu raia wakatae, je wadau mpo tayari kuandamana? Maana kupopoma humu haisaidii
 
Siyo kumzuia tu kuteka maji, bali pia kumkwangua kabisa.
 
Ngoja tuone hadi mwisho wa hii issue, yaani bunge lipitishe halafu raia wakatae, je wadau mpo tayari kuandamana? Maana kupopoma humu haisaidii
Hatua kwa hatua. Kuna muda wa kupiga dhidi ya mkataba wa kishenzi wa DP.

Wakishupaza shingo, utakuja muda wa kuandamana kuukataa mkataba kwa nguvu.

Wakishupaza shingo, utakuja wakati wa kumwondoa Rais na serikali yake isiyoheshimu matakwa ya umma.
 
Back
Top Bottom