Kuhusu suala la Mwigulu Nchemba; Elimu ya msingi kuwa miaka kumi

Mwamba 777

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2020
Posts
2,780
Reaction score
4,504
Kwa kawaida mtoto mpaka afike chuo kikuu na kuhitimu tyari anakuwa na umri wa miaka 25 na zaidi.

SWALA hili la elimu ya msingi miaka kumi ni kuzeesha WATANZANIA madarasani na kupotezeana muda

Imajeni mpaka mtoto amalize shule ya msingi miaka kumi ajiunge sekondari o'leval atoke hapo aende a'level mpaka chuo, amalize chuo akae mtaani miaka 3 au 4 na zaidi ndo aje apate ajira. Je hapo hajazeekea darasani??

Pia Kuna ajira wanaweka limitations za umri mwisho miaka 20 hadi 28, je hapo hawa vijana watapata fursa hiyo au Bado watakuwa wapo chuoni?

Soma Pia: Mwigulu: Elimu ya msingi ya lazima kuwa miaka 10

Hili SWALA serikali iliangalie Kwa umakini na undani zaidi, kama wakitekeleza mpango huo waziondoe limitations za umri KATIKA ajira.

Ajira zote za serikali na KATIKA taasisi zote za serikali na binafsi umri wa mwisho kuingia kazini uwe ni miaka 45 na waongeze muda wa kustaafu wafanye miaka 65 au 70.
 
Chama cha majambazi
1776207325756.jpg
 
Kwa kawaida mtoto mpaka afike chuo kikuu na kuhitimu tyari anakuwa na umri wa miaka 25 na zaidi.

SWALA hili la elimu ya msingi miaka kumi ni kuzeesha WATANZANIA madarasani na kupotezeana muda

Imajeni mpaka mtoto amalize shule ya msingi miaka kumi ajiunge sekondari o'leval atoke hapo aende a'level mpaka chuo, amalize chuo akae mtaani miaka 3 au 4 na zaidi ndo aje apate ajira. Je hapo hajazeekea darasani??

Pia Kuna ajira wanaweka limitations za umri mwisho miaka 20 hadi 28, je hapo hawa vijana watapata fursa hiyo au Bado watakuwa wapo chuoni?

Hili SWALA serikali iliangalie Kwa umakini na undani zaidi, kama wakitekeleza mpango huo waziondoe limitations za umri KATIKA ajira.

Ajira zote za serikali na KATIKA taasisi zote za serikali na binafsi umri wa mwisho kuingia kazini uwe ni miaka 45 na waongeze muda wa kustaafu wafanye miaka 65 au 70.
MZEE UMESHINDWA KUMUELEWA. AMESEMA HIVYO BAADA YA SERIKALI KUAMUA KUWA ELIMU YA MSINGI NI KUANZIA DARASA LA KWANZA MPAKA KIDATO CHA NNE. HIVYO KWA SASA KIDATO CHA NNE NI ELIMU YA MSINGI
 
Elimu inayozungumziwa ni elimu ya msingi madarasa 6,sekondari madarasa manne,kwa pamoja ni madarasa kumi ambayo ni ya lazima
 
amini usiamini kuna kitu kimejificha na kina uhusiano na islamization of tanzagiza, mtakuja kuona baada ya kila kitu kuwa wazi, kuna mambo yatakuwa yamewekwa ya dini islam, waziri wa elimu mzanzibari hajawekwa bila ya sababu ...
 
Elewa hivi miaka 6msingi miaka 4 hio sekondary itakuwa 10 ,advance 2
Mtoto ataanza la kwanza akiwa na umri wa miaka 6 plus 10 atakuwa 16 umri advance 2 itafika 18
Ushaelewa wala hakuna cha kuzeeka hapo mkuu
 
Upo mbali na taarifa mleta mada.
Badala ya lawama anza na kuuliza kwanza.

Elimu ya msingi ni kutoka darasa la kwanza hadi kidato cha nne, hapo kumbuka pia darasa la sita ni la mwisho kisha kwenda sekondari kwa miaka minne, hapo inakamilisha mwaka wa kumi tokea aanze darasa la kwanza.
 
amini usiamini kuna kitu kimejificha na kina uhusiano na islamization of tanzagiza, mtakuja kuona baada ya kila kitu kuwa wazi, kuna mambo yatakuwa yamewekwa ya dini islam, waziri wa elimu mzanzibari hajawekwa bila ya sababu ...

Hawataweza mkuu.
 
Hiyo miaka 3 ya ziada ni ya kuwafundisha nini kipya ambacho hakiwezi kufundishwa ndani ya miaka 6?

Tuna viongozi wa ajabu sana.
 
Back
Top Bottom