Na buku 5000 ya udoso usiisahau
Vipi kuhusu college of informatic naombeni ada yao na jinsi kujua hapo kwa informatic ni vipi
Pia mambo ya afya kama ana bima
Bima imejumuishwa kwenye direct cost soma vzur huko juu kuna maelezo zaid
Utaratibu uliopo ukiwa na bima kama ya NHIF hutohitajika kulipia tena cost ya matibabu ndivyo ilivyo sehemu zote
Katika suala la malipo hasa ya michango ( direct cost) mwanachuo anahitajika kulipa michango yote ambayo ni sh.282,500.
Ili kueusha usumbufu usiokuwa Wa lazima ni vyema mwanachuo akalipia michango yote kwani ukifika tu kitu cha kwanza watakuhitaji upande kwenye sehemu husika ya usajili ukiwa umelipa kiwango tajwa.
Kuhusiana na malipo ya ada (tuition fee) utalipa kulingana na kiwango cha mkopo ulichopata...nikiwa na maana kwamba umepata asilimia ngapi..kama haujafaham jinsi ya kukokotoa mkopo wako mchanganuo hutolewa pindi mnapofika pale chuoni.
Kwa ujumla mazingira ni ya kawaida na yanakuruhusu kusoma (kwa wale Wa education) changamoto ni chache tu hasa upatikanaji Wa maji ambao ni kwa asilimia 80 kama alivyochangia mdau hapo juu..
Kuhusu suala la kulipa nusu bado haijulikan kama wataukubali huo mfumo japo walisema unaweza kutumika ila kwa mwanachuo ambae atachelewa kulipia michango yake matokeo yake huendelea kushikiliwa mpaka pale atakapokamilisha michango yote..!!
Hongereni na karibun UDOM..!!
Mkuu kuna mdogo Wangu amepata college of health direct cost ni 303,500 lakin kwa sababu anabima hajalipia ile laki ya medical, je itaathir au watamzengua registration? I mean kalipa 203,500 badala ya 303,500 cuz ana bima ya afya