Kuhusu utafiti wa tatizo la ajira, Dkt. Mpango usihadae Watanzania

Kuhusu utafiti wa tatizo la ajira, Dkt. Mpango usihadae Watanzania

Rigidity

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2024
Posts
391
Reaction score
482
Habari za asubuhi wanajukwaa.

Nikisikiliza habari za magazetini leo nimesikia eti makamu wa Rais Dk. Mpango amewataka wanaofanya utafiti watafiti tatizo la ajira kwa vijana limeanzia wapi.

Kama mpaka leo kama kiongozi hujajua kama tatizo kubwa ni nani bora kunyamaza kuliko kuongea kauli kama hizo kama kiongozi mwandamizi nchini.

Pia eti anashangaa vijana kuchukua mashangazi. Mzee Mpango hotuba uliandaliwa au ulitoa kichwani?

Kwaufupi namshauri mzee asizungumzie suala la ukosefu wa ajira. Labda zaidi aishauri serikali isizalishe baadhi ya wataalam maana wamejaa kibao mtaani na ajira hamtoi.
 
Hahahaha, yaleyale. Kwanini Tanzania masikini - "hata mimi sijui"

Tumeachia kila kitu kiende kienyejienyeji matokeo kila mahala pako hovyo.

Tukiwa kwenye majukwaa tunapotafuta kura, huwa tunawatumia machawa wetu, wadangaji mjini na bodaboda kuonyesha hakuna tatizo la ajira Bali wanaolalamiki aka wasomi ndio tatizo na kuruhusu hata majukwaa kutumika kutukana wasomi.

Failure to plan is plan to failure.
 
Unafuta FAO la kujitoa ambalo vijana wengi walikuwa wanapatia mitaji unatarajia Nini? Mtu anamiaka 24 unamwambia asubiri milioni mbili akifikisha umri wa miaka 55
 
Habari za asubuhi wanajukwaa.

Nikisikiliza habari za magazetini leo nimesikia eti makamu wa Rais Dk. Mpango amewataka wanaofanya utafiti watafiti tatizo la ajira kwa vijana limeanzia wapi.

Kama mpaka leo kama kiongozi hujajua kama tatizo kubwa ni nani bora kunyamaza kuliko kuongea kauli kama hizo kama kiongozi mwandamizi nchini.

Pia eti anashangaa vijana kuchukua mashangazi. Mzee Mpango hotuba uliandaliwa au ulitoa kichwani?

Kwaufupi namshauri mzee asizungumzie suala la ukosefu wa ajira. Labda zaidi aishauri serikali isizalishe baadhi ya wataalam maana wamejaa kibao mtaani na ajira hamtoi.
Nmecheka sana jana.
 
Mfano wewe ume plan kutoa ajira kiasi gani kwa ndugu zako au umetoa ngapi? Ajira ziko aina mbili private na public

Wewe kama private umetoa ngapi?

Duh aisee.

Leo hii unauliza raia wametoa ajira ngapi?
Kazi ya Serikali ni nini sasa?
Binafsi nina mashamba nimeajili watu wengi huko na kwenye mzunguko wangu nimebeba watu wa kutosha.

Serikali ndio muajiri mkuu na mtunga sera mkuu zinazotoa mustakabali wa taifa, Sera nzuri zitaleta ajira zakutosha na sera mbovu matokeo yake ndio haya.
 
Kisababishi kimojawapo cha tatizo la ajira ni watoto wa wafanyabiashara wa kiswahili kuomba kazi serikalini badala ya kuwa kwenye biashara za wazazi wao kama ilivyo kwa wahindi na waarabu

Siô Kîla Mtoto wa mfanyabiashara anataka kuwa mfanyabiashara. Wengine wanapenda shughuli zingine za uzalishaji

Kama ilivyo siô kîla Mtoto wa Mwalimu anataka kuwa Mwalimu.
Au sio Kîla Mtoto wa Daktari anataka kuwa Daktari.

Kabla hujatoa maonî yako ni vizuri kuyapima Kwanza
 
Back
Top Bottom