Dalton elijah
JF-Expert Member
- Jul 19, 2022
- 373
- 829
- KWA miaka ya hivi karibuni kuna kukithiri kwa wizi wa mashada ya maua makaburini, na ung'oaji wa misalaba unaofanywa na baadhi ya wananchi kwa Malengo tofauti tofauti.
- Katika baadhi ya makaburi ambayo hayalindwi, kumekuwa na aina hiyo ya wizi hasa katika miji mikubwa kama Dar es Salaam, Arusha, lakini kwa sasa hali imeendelea kuwa mbaya, safari hii jiji la Mwanza limekumbwa na kadhia hiyo.
- kutokana na hali hiyo, hivi sasa baadhi ya ndugu wanalazimika kuweka alama za mawe kwenye makaburi ya wapendwa wao waliofariki, au misalaba ya mbao ambayo wanadai imekuwa ikiliwa na mchwa na kukosa uimara
- Inatusikitisha sana kutokana na vitendo hivyo ambavyo ni sawa na udhalilishaji wa ndugu waliokufa kwa kuibiwa alama zao, ambazo ni muhimu kwa kumbukumbu kujua walikozikwa.
- Hali imekuwa ikusishwa na Biashara ya chuma chakavu ambayo kwa kiasi kikubwa ndiyo imesababisha kukithiri kwa biashara hii, ambapo mbali na kung'oa misalaba. wamekuwa wakijihusisha katika biashara ambazo sio rasmi