Kuiba Misalaba, Mashada ya Maua Makaburini ni Laana

Kuiba Misalaba, Mashada ya Maua Makaburini ni Laana

Ukinunua tiles zilizovunjika vunjika sio kuwa zimevunjika safarini au dukani, hapana zingine zimeng'olewa makaburini
Nilishangaa nilipoenda makaburini kuona ya jirani tiles zimebebwa tena makaburi mengi tu

Hivi si laana hizi
 
Ukiona hata wafu wanaibiwa vyao ujue tumefika pabaya kama jamii. Sungu sungu irudishwe mitaani kuleta amani.
Sungusungu ilete amani?
Labda hauwajui Sungusungu vizuri
 
Kuiba msalaba uliopo kaburini na kuiba fedha zilizotolewa na wafadhili kununua dawa, na watu wakafariki kwa kukosa dawa zilizopaswa kununuliwa, ni kipi chenye laana zaidi?

Wote ngoma droo ikizingatiwa walisema wenyewe: "kifo ni kifo tu."
 
Zamani makaburi yaliogopwa sana, hata mchana tu ilikuwa ni ngumu kupita maeneo hayo yalitisha. Siku hizi kuna vinjia vingi vinakatisha makaburini, kuna watu wanazurura makaburini na mifuko ya salfeti wakitafuta vyuma chakavu na takataka zingine kama chupa za plastiki.
Hii ni dalili ya wajinga kuwa wengi hii nchi mtu anaiba msalaba ili akauze kilo 300
 
Back
Top Bottom