Zamani makaburi yaliogopwa sana, hata mchana tu ilikuwa ni ngumu kupita maeneo hayo yalitisha. Siku hizi kuna vinjia vingi vinakatisha makaburini, kuna watu wanazurura makaburini na mifuko ya salfeti wakitafuta vyuma chakavu na takataka zingine kama chupa za plastiki.