Kuibiwa kusikie tu

Kuibiwa kusikie tu

Mkuu siku ukikuta mwizi anashughulikiwa, utasema watu wanajichukulia sheria mkononi? Mimi wezi hukumu yao ni kuwapeleka kwa baba mbinguni,akawasamehe huko.
 
Sasa hata akichangiwa,si anaweza kurudia tena kosa lile lile? Ataenda tena kuzitoa hela zote kisha apande Daladala ziibiwe tena,

Lazima tu solve tatizo kwanza.
Mkuu ataweka pesa kwenye Busta kwahiyo vibaka hawata weza kumuibia tena, Mimi mfumo wangu wa kuweka pesa natumia aina Mbili moja napenda Busta yenye mifuko ndiyo naitumia kuweka pesa nyingi labda milioni hii ni nzur kama naenda umbali mrefu na natumia daladala za kugombania, Mbinu ya pili natumia begi la mgongoni kuweka pesa ila mabegi yangu yote yana sehemu nyingi ndani zilizo jificha yani nikituma kanichukulie pesa utatafuta utasema hakuna,au nafunga begi na vikufuli vidogo.
Kwenye daladala vibaka ni wengi mida za Asubuhi na jioni tena njia za Tandale uzur, Makumbusho hizi sehemu lazima utunze pesa ndani ya Busta, ni vizur vijana tuache kununua bossa tununua Busta zenye mifuko na zipo Busta nyingine zina mfuko wa nyuma zina kifungo una vaa Busta yako ndani nje uvaa surali imeisha hiyo.
 
Next time ukiwa na hela nyingingingi kidogo sio vibaya ukasacrifice kiasi kidogo upande usafiri wenye usalama mkuu.

Kuna viumbe wananusa hela.
 
Siku nyingine ukiwa na hela nyingi usipande daladala na usitembee umbali mrefu kwa miguu, ni mwendo wa boda au uber au bolt. Pia ukiwa na hela na usalama mdogo weka hela kwenye tigo pesq au mpesa, bora upate hasara ya buku 5 kutoa hio laki 3 kuliko kuipoteza yote
 
Siku ya jana niliibiwa pesa ndani ya daladala kiasi cha 350000 yani usiku mzima nimekosa usingizi. Hapa nilipo kichwa kinauma hatari 😭😭
Kosa ulilofanya baada ya kugundua umepigwa ni ile kuanza kulia kwa sauti kubwa, kugalagala chini na kuanza kuhadithia kila mtu kwamba umeibiwa. Ungekausha tu mkuu wala hakukua na haja ya kwenda polisi.
 
Back
Top Bottom