Kuibiwa kusikie tu

Kuibiwa kusikie tu

Mkuu, kila mtu ana kiwango chake cha hela anachoona ni kikubwa.

Kwako inaweza kuwa hela ya matumizi ya siku 1 ila kwa mwingine ni matumizi ya mwezi na zaidi.

Hiyo ndio hali ilivyo miongoni mwa jamii yetu
Unajua kuna watu humu wanadharau sana mkuu na wao kisa wamejipata na wanazani life ni kwa kila mtu
 
Next time tumia hii formula. Zamani na mm nlikuwa mbahili, yaani nikitaka kufanya malipo kama hela iko Bank, badala ya kuwa assign bank wanisaidie kulipa huo muamala tena kwa gharama ya Tshs elfu10 tu, najikuta naenda ku withdraw hata 10m kisha nabeba naenda kulipa Cash. Sasa basi, huko njiani kulivyo na risk mtu akikuona tu umetoka Bank na Kibegi... anajua huyu atakuwa na rundo la hela. Lakini kibishi bishi nikawa nafanikiwa. Ila nilikuwa nafanya patapotea bila kujua Hadi siku nlipokuja gundua kuwa elfu 10 sio kitu kwa gharama ya usalama wa Tsh 10m. Pia unaweza poteza maisha hata kwa tshs elfu 50,10, 5. watu wasivyo na utu pale wanapoona kitu Hela.

Hivyo basi, kwa sasa na tokea nilivyojitambua, nikiwa nataka kufanya muamala kuanzia 1m na zaidi, naenda zangu Bank nafanya Bank transfer. Hiyo inakuwa salaama zaidi.

Sasa basi, mjomba hapa, alitakiwa, akodi Bolt/Uber kwa bei ya tshs 5,000 ili kuilinda 350,000/= yake, matokeo yake amejiaminisha na kwenda kujichanganya kwenye mbanano wa Public Transport, yakamkuta yaliyomfika.

Kuna siku enzi hizo natoka kibaruani Mwenge Dsm nakuja zangu Ilala, nikawa nimeweka elfu 20 kwenye Pochi mfuko wa Nyuma. Tukapanda DCM za mbagala wakati huo miaka ya 2002 usafiri ni mgumu kichizi babake. Hata ukipata la kusimama unashukuru, Japo nashukia Ilala Boma.

Sasa basi, kumbe bwana sio wote wanakuwaga , ni abiria, wengine ni vibaka wanajitafutia Riziki kwenye mifuko ya Watu, wengine unakuta Mtu kavaaa vizuri kweli kweli na huwezi kumshtukia.

Jamaa mmoja, akawa anapenyeza mikono mifukoni mwa watu, ghafla nikasikia Mkono ukawa unafungua kifungo cha Mfuko wangu wa nyuma, nami nikatulia, kwa vile wallet ilikuwa imebana, nikasema akishaanza kuivuta ni mtaiti Mkono. Na kweli, nilifanikiwa, ile nageuka, ananikonyeza, Nyamaza huku akinionyesha bisi bisi, akasema sina cha kupoteza Mwanangu kama utalisanua.

Basi movie likaishia hapo hapo, nikamsitiri.
Hadi hapo hakukuibia ila alikukanya usiseme kuwa kuna kibaka mule ndani?

Nawaza kama ungewasanua watu au konda pindi ulipokuwa unashuka ili ashughulikiwe, wakati huo wewe ushaondoka.
 
Mwendokasi wamejaa sana nishawaumbua kama watatu, ila mwezi uliopita nilipigwa mimi laki 3 alafu nilimshtukia sema mbanano ule nilisogea ndani naona ananiangalia kwa kuibiwa mara yeye ndo ananipanga eti sogea utaibiwa niliposogea wakapeana ishara wakashuka nami kushuka kituo cha mwisho ndiyo nagundua hapa kausha damu wananihusu, wezi walaaniwe hasawa mwendokasi
 
Mkuu, kila mtu ana kiwango chake cha hela anachoona ni kikubwa.

Kwako inaweza kuwa hela ya matumizi ya siku 1 ila kwa mwingine ni matumizi ya mwezi na zaidi.

Hiyo ndio hali ilivyo miongoni mwa jamii yetu
Mimi nachojua jf hakuna masikini. wote wanagari kali wanabiashara zamaana, wanamajumba makubwa, kazi nzuri, wanapisi kali kama ni wanawake wanawaume matajiri bila kusahau wanadrive magari makali mfano bmw na sio passo
 
Mwendokasi wamejaa sana nishawaumbua kama watatu, ila mwezi uliopita nilipigwa mimi laki 3 alafu nilimshtukia sema mbanano ule nilisogea ndani naona ananiangalia kwa kuibiwa mara yeye ndo ananipanga eti sogea utaibiwa niliposogea wakapeana ishara wakashuka nami kushuka kituo cha mwisho ndiyo nagundua hapa kausha damu wananihusu, wezi walaaniwe hasawa mwendokasi
Ulikuwa umeziweka mfuko upi hizo hela
 
Mimi nachojua jf hakuna masikini. wote wanagari kali wanabiashara zamaana, wanamajumba makubwa, kazi nzuri, wanapisi kali kama ni wanawake wanawaume matajiri bila kusahau wanadrive magari makali mfano bmw na sio passo
Tuliopo humu ndio tuliopo mtaani.

Mtaani kwako, wote mna hizi sifa ylizotaja hapa?
 
Ulikuwa unatembea nazo ili iweje??tembea na pesa mwisho 50 tu zingine ziwe benki au kwa simu basi
 
Back
Top Bottom