Kuibuka kwa wimbi la Ujambazi hasa DSM ni kukomoana ndani ya Jeshi la Polisi?

Kuibuka kwa wimbi la Ujambazi hasa DSM ni kukomoana ndani ya Jeshi la Polisi?

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
16,419
Reaction score
26,594
Vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalama vijiulize hili swali kwa makini.

Hii hali si ya kawaida na sisi wananchi tunaiona kwa macho yetu.

Hili wibi la ujambazi lililoibuka hasa baada ya Mama Samia kuingia madarakani na kutaka mabadiliko, hasa Dar es Salaam, kuna nini nyuma yake?

Tunajua kuwa majambazi kuna mtandao wao, na tunajua kuwa Polisi nao wana ingalau fununu juu ya mitandao hiyo na mara nyingi inachukua hatua kuivunja.

Wezi wa magari na vipuri wana mitandao yao.
Majambazi wa kuvunja nyumba na kuiba wana mitandao yao.
Waporaji na vibaka wanajulikana hasa maskani zao.
Wezi wa kalamu na kughushi nao wana mitandao yao.

Sasa ni kama wameamua saa ya kuonyesha uwezao wao na kufanya wnachotaka umewadia.
Hili ndio swali langu. Why now?

Je, wamepata "green light" ya kuendelea na vitu vyo toka sehemu fulani ndani ya jeshi la polisi?
Je, hii ni komoana komoana ndani ya jeshi la polisi?
Je, ni kwamaba bila mimi hapo DSM mambo hayataenda?

Nimejiuliza haya maswali sipati jibu.

Lakini waswahili walisema, Kikulacho ki nguoni mwako.
 
Hili suala la ujambazi naona linakuzwa kupita kiasi, haiwezekani na haitakuja kutokea nchi hii kusiwe na ujambazi.

Matukio ya sasa ni ya kawaida sana, jiji lenye watu karibu milioni 6 matukio haya ya sasa ni madogo sana.

Ujambazi ulikuwa enzi zile za kuteka vituo vya Polisi, kuvamia mabenki nk.
 
Ww ujambazi ambao uliwai kutokea ni kama wa epa , meremeta, escrow nk hao ndo waliiba hela nyingi sana sema wapo tu mtaani wanadunda.
 
Mwananchi wa Kawaida kwake hili ni Tishio kubwa kuliko hata Escrow. Maana shida inampata moja kwa moja.
 
Hapana, kwasasa yamezidi hata mama yenu alikiri hivyo hata wasiompenda hayati wanaona na kukiri hali sio nzuri
Mbn kipindi Cha magu machalii wawili wa mtaani walisumbua sana kuiba kwenye matigo pesa Ila wakauliwa na wazee na walifanya matukio Sana walisumbua 2019 baada ya kuuliwa vijana wa maskani yake walifanya fujo Sana na wengi wakakamatwa ,mchizi mwingine wa tatu wa kitaaani nae mtu hatari kapotea haonekani Ike tetesi zinasema kafuchwa sentro.

Ujambazi ulikuwepo.
 
Ushauri muhimu kuhusu jiji la Dsm:-

1. Fungeni CCTV camera maeneo muhimu na barabara zote za Dsm kama tulivyofanya Nairobi Kenya. Hakuna ujambazi tena.
2. Masuala ya kanda maalumu yamepitwa na wakati. Wekeni RPC mmoja tu wa Dsm.
3. Mikoa ya kipolisi iliyoweka Dsm ilikuwa ni lengo la ulaji na kuuziana deal ili kwingine kuharibike ili ukipambana unahamishiwa mkoa kamili kama arusha .mikoa ya kipolisi iondolewe.
4. Suala la polisi jamii ni muhimu kutumika Dsm. Mkuu wa kitengo cha polisi jamii tanzania hajui kaxi yake afukuzwe.
5. Kamati za ulinzi na usalama temeke , kinondoni na ilala hazijui wajibu wao, wakuu wa wilaya hizo mara watakapoteuliwa wilaya zifuatazo ( ilala,temeke, kinondoni, Rorya,na tarime) maDC wake WATEULIWE kutoka JWTZ au Jeshi la polisi.
 
Ushauri muhimu kuhusu jiji la Dsm:-
1. Fungeni CCTV camera maeneo muhimu na barabara zote za Dsm kama tulivyanya Nairobi Kenya. Hakuna ujambazi tena.
2. Masuala ya kanda maalumu yamepitwa na wakati. Wekeni RPC mmoja tu wa Dsm .
3. Mikoa ya kipolisi iliyoweka Dsm ilikuwa ni lengo la ulaji na kuuziana deal ili kwingine kuharibike ilu ukimbambana unahamishiwa mkoa kamili kama arusha .mikoa ya kipolisi iondolewe.
4. Suala la polisi jamii ni muhimu kutumika Dsm. Mkuu wa kitengo cha polisi jamii tanzania hajui kaxi yake afukuzwe.
5. Kamati za ulinzi na usalama temeke , kinondoni na ilala hazijui wajibu wao, wakuu wa wilaya hizo mara watakapoteuliwa wilaya zifuatazo ( ilala,temeke, kinondoni, Rorya,na tarime) maDC wake WATEULIWE kutoka JWTZ au kesho la polisi.
Mkuu nakubaliana na maoni yako ingawaje si yote.
Lakini tukumbuke kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya majambazi na maafisa wa polisi, hasa wale waliopitia upelelezi.
 
Back
Top Bottom