Kuifanya League ya Tanzania a Better Product

Kuifanya League ya Tanzania a Better Product

Kuongeza Wadhamini
TFF na wadau watafute wadhamini zaidi, hata kuuza TV rights za kila game ili ionyeshwe na kuwashauri wadau wenye makampuni kufadhili league

Wadhamini nao ni wafanya biashara ati. Wako tayari kui-invest tuu pale ambapo watapata faida. Hakuna mdhamini wa maana atakuja kudhamini ligi ambayo haoinyeshi projections yoyote ya kuimarika. Kwa maana nyingine inabidi kwanza ligi iimarishwe. Kama ligi ikiimarishwa wadhamini watajitokeza wenyewe bila hata TFF kuwatafuta.

Kuonyesha kila Game kwenye TV
Kuuza rights za kuonyesha Mpira / Mechi zote kwa Pesa nyingi itakayosaidia kuwekwa kwenye Fungu la Kuzigawia Timu entrance Fee ya Washibi watakaoingia kwenye mpira ni Pesa ndogo kuzitegemea, na hazitatosha.

Huwezi kuuza rights za kuonyesha ligi kwa pesa nyingi wakati ligi yenyewe ipo katika hali ya chini. Hakuna TV ya maana ambayo itakuwa tayari kununua hizo rights kwa pesa nyingi. Hivyo bado ligi inabidi iimarishwe kwanza, na ikiwa imara lazima TV zitaweka bids za juu kununua hizo rights. TVs want to show the best, simply because viewers want to pay those TVs to view the best players in the game. Cheki mfano, BT Sport walivyomwaga pesa kuonyesha Champions League na kuipiga bao Sky Sports waliokuwa wanatoa pesa ya kawaida tuu.

Kuongeza / Kubadilisha Aina ya Fungu la Kugawia Timu
Badala ya Fungu la kiingilio kugawiwa timu zinazoshinda kwa percent nusu kwa nusu (baada ya makato ya TFF, Uwanja n.k.) Nashauri fedha igawiwe kwa Mafungu ya Percent Kubwa Zaidi kwa Timu itakayoshinda Mchezo husika na Ndogo kwa timu itakayofungwa (endapo Timu zitadraw) basi wote wapewe fungu dogo na zinazobaki ziwekwe kwenye Kapu na kuja kupewa Timu mwisho wa League itakayochukua Kombe.., kwa kufanya hivi nadhani kutapunguza Timu masikini kuuza Mechi; pia kila game itakuwa na maana sababu kushinda game kutakuwa na faida kubwa, kuliko kufungwa

Hapo unaweza kudhani unatatua tatizo la timu masikini kuuza mechi kumbe unaleta tatizo la timu kubwa kununua mechi na pengine kuwahonga hata marefa. Kwa wenzetu timu inayocheza nyumbani inachukua mapato yote. Tatizo kwetu timu hazimiliki viwanja. Tatizo la timu kuuza mechi ni pana zaidi na linahusisha suala zima la kuzoeleka kwa rushwa katika katika jamii yetu. Maana hata jana Liverpool si wangewahonga Crystal Palace na kubeba points zote?

Kuhakikisha / Kusaidia Mashabiki kuwa RegionalKwa sasa tumeona kwamba zaidi ya Simba na Yanga timu nyingine za mikoani hazina kabisa mashabiki.., kwahio ili kuwe na uzalendo na watu kupenda Timu inasaidia kama Timu itakuwa ina uhusiano mkubwa na mkoa inakotoka.., Kwa mfano kama kila Mkoa ikiwa na Timu yake Mfano Mwanza Heroes; au Igembensabo, au Simiyu Stars.., kwa kuanzia wakazi wa mji husika watakuwa na uhusiano na upendo zaidi na Timu zao na wafadhili local watapatikana zaidi, ingawa hizi Timu zitaruhiwa kusajili kutoka popote na kila mkoa utaruhusiwa kwa na Timu hata zaidi ya moja kwa kuanzia ila mwisho wa ligi zikishuka hata kama mkoa fulani utakuwa hauna timu itaendelea hivyo hivyo. Na kwa kuanzia Timu ambazo zipo tayari kwenye League kina Simba na Yanga n.k. zitaendelea hivyo hivyo ila kila mkoa kwa kuanzia huimizwe kuwa na Timu ya mkoa ambayo ipo kwenye league (na hii itasaidia kupata vipaji kutoka mikoani)

Huwezi kulazimisha watu kuwa wafuasi wa timu fulani ili kuimarisha regionalism in sports, but I can see where you are coming from. Miaka hiyo zilikuwepo timu kubwa na kali tuu karibia kila mkoa. Mikoa mingine kama Tanga na Mbeya ilikuwa na timu zaidi ya moja kwenye ligi kuu lakini siku hizi siyo hivyo tena.

I would say the best approach ni kuimarisha soka at the local level bila kujali regionalism. Wengine wanaita "grassroot football". Hii kitu iliwepo zamani mpaka kwenye shule za msingi. Nakumbuka wakati huo nikiwa primary tulikuwa tunashindana kikata, kitarafa, kiwilaya mpaka kimkoa. Pia kila jioni tukitoka shule tulikuwa tunaenda kucheza mpira na kujiandaa kurudi home kula kichapo.

Siku hizi hakuna hata viwanja kitaani kuchezea mpira. Zile sehemu ambazo zilikuwa wazi kumefunguliwa mashina ya vyama vya siasa, zimekuwa sehemu za kupaki magari usiku, sehemu nyingine kuna pubs/grocery na maeneo mengine ya wazi yamevamiwa na watu binafisi. Siku hizi mtoko wa vijana jioni kwenda kwenye mikutano ya siasa ambayo mingi yao inafanyika jioni kwenye viwanja hivyo hivyo ambayo vijana walitakiwa wasakate kabumbu mida hiyo. Serikali za mitaa na vyama vya soka at lower level havifanyi ya kutosha kutoa facilities na gharama nyingine za ku-support michezo at local level. Najua huko chini hawapati support ya kutosha kutoka juu na hilo ni tatizo lingine.

Juzi juzi hapa nimemsoma Wambura akiwataka waandishi wa habari za michezo wajikite zaidi kwenye habari za kunzisha, kuendeleza na kuimarisha academies za soka. Akalalamika kuwa waandishi wa habari huwa wanafocus zaidi kwenye timu za Simba na Yanga badala ya watoto. Nikajiuliza kwani jukumu la waandishi wa habari ni kuanzisha, kuendeleza na kuimarisha football academies? Kwani ziko academies ngapi so far? Pia wasomaji wa hao waandishi huwa wanapenda kusoma nini? Maana mara nyingi waandishi wa habari wanaandika kile ambacho kinapendwa kusomwa zaidi na wasomaji wao. Waandishi wa habari ni wafanyabiasha pia. They are not volunteers. Na wengine hawaandiki habari kama hawajapewa bahasha ya kaki.

It was interesting kusoma kiongozi wa chama cha soka akilaumu waandishi wa habari badala ya kuanza na chama chake kwanza. Hapo alikuwa anacheza mchezo wa kutupiana mipira kwa sababu siyo kazi ya waandishi wa habari ku-supervise football academies kama Wambura alivyodai. Siyo kazi ya waandishi wa habari kuhakikisha kuwa mchezaji anaimarika kwa kwa kuwa na the Five S alizozitaja Wambura. Wambura anajawataja akina Messi na Nymeir jinsi walivyogunduliwa lakini sidhani kama waligunduliwa na waandishi wa habari. Hata hizo nchi alizozitaja kama Brazil, Ujerumani, Uingereza, n.k wachezaji hawagunduliwi na waandishi wa habari. Kazi yao ni kuripoti na labda ku-analyse wachezaji ambao tayari wameshaguduliwa.

HITIMISHO. Nadhani kwa kufanya hayo italeta uzalendo zaidi na kila game sababu itakuwa na faida kubwa kila mshindi wa game atapata pesa na mwisho wa siku atakayeshinda League mwisho wa mwaka na yeye apate dau la pesa nyingi kulingana na Nafasi atakayomaliza nayo.Kwa kuwa kila game itakuwa na Price Tag/Kifuta Jasho kikubwa nina uhakika kutakuwa na Ushindani Mkubwa

Nadhani the best approach ni kuangalia kwanza the underlying causes ya kuwa na kiwango cha chini cha soka. Kwanza tusisahau kuwa Tanzania ilikuwa koloni la Waingereza. Tofauti na Wafaransa, Waingereza hawakuendeleza kabisa soka kwenye makoloni yao baada ya kupata uhuru. Kwa Wafaransa baada ya makoloni yake kupata uhuru, walikuwa wana-scout wachezaji kutoka kwenye hizo nchi na kupelekwa kucheza kwenye klabu za Ufaransa. This has motivated kids to want to perform at the same level as their peers.

Kuna matatizo mengine makubwa kama ukosefu wa grassroot football and kutokuwepo kwa uwekezaji kwenye soka. Pia Tanzania hakuna scouting kabisa. Simply hakuna kitu kama hicho. Sidhani hata kama kuna mtu ambaye ameajiriwa specifically kwa kazi ya scouting in Tanzania. In fact hakuna hata academy system ya kuwezesha mtu kufanya hiyo scouting. Leo kweli Arsenal au Man Utd wanaweza kumlipa mtu kuja kufanya scouting Tanzania?

Pia sababu kubwa sana ya kuwa na kiwango cha chini cha soka ni ukosefu wa political will. Kuna watu wanadhani mafanikio kwenye sekta ya michezo yanakuja hivi hivi tuu. There must be a political will. Kwa mfano, Cameroon, katika miaka ya 1980s, serikali yao ilikuja na programu (siyo mpango kama tulivyozea hapa Bongo) ya kuendeleza soka. Serikali ilihusisha sekta binafsi kujenga shule za soka. Hii ilisaidia kukuza wachezaji wazuri ambao waligunduliwa mapema sana na kuendelezwa mpaka kucheza kimataifa, ikiwemo timu ya taifa lao.

Pia Ivory Coast, serikali yao ilikuja na program kuwa nchi yao lazima icheze fainali za Kombe la dunia baada miaka nadhani 20 au 25. Wakaaza kutengeneza mazingira. Na kweli baada ya muda huo wakafanikiwa kuchezea hizo fainali. It was a strong political will followed by investment ya ukweli into the academy system ambayo ilikuja kusaidiwa na akina Jean Marc Guilou katika miaka ya 1990s. Hawa akina Droba na Yahaya Toure, na wengine hawakuanza hivi hivi tuu. Lakini hapa kwetu unasikia watu wakisema kuwa lazima tucheze fainali za zijazo za kombe la dunia. Tunapenda shortcuts wakati hazipo kwenye soka. Mcheza soka siyo kama mwanamuziki wa Bongo Fleva.

Kwa upande wa Afrika, wachezaji wenye umri kati ya miaka 6-13 wanakuwa kwenye level moja in terms of their ability on the pitch. Physically wanakuwa kwenye level moja. Pia technically na jinsi wanavyo-pass mpira vyote vinakuwa kwenye level moja. Tofauti inaanza kujitokeza kuanzia umri wa miaka 13 kwenda mbele.

Sasa tofauti iliyopo kati ya Cameroon/Ivory Coast na Tanzania ni kile kinachotokea baada ya mchezaji kufikisha umri wa miaka 13. Cameroon na Ivory Coast tayari wana miundo na michakato inayosaidia kuwaendeleza wachezaji wenye umri huo na kuwa-promote kufanikiwa kimataifa kwenye ngazi mbalimbali za timu zao za taifa na kwa nchi nzima kwa ujumla. Tanzania hatuna miundo na michakato kama hiyo na kama ipo basi hakuna emphasis ya kutosha kwenye hizo structures and processes.

Kwa hiyo ili ligi ya Tanzania iwe a better product inabidi tufikirie kwa mapana zaidi. We have to go back to the root causes ya kuwa na kiwango cha chini cha soka kwa sababu hizi sababu ndizo hizo hizo zinazofanya ligi iwe mbovu. Kwa maneno mengine solutions zako zinafaa zaidi kwa ligi ambayo tayari ni productive au projections zinaonyesha kuwa it will be productive miaka 10 au 15 ijayo.
 
EMT nimekupata unachoongelea.., na kukuza viwango vya wachezaji academies n.k. vitasaidia zaidi Timu yetu ya Taifa na wachezaji wetu kucheza nje ya nchi.. ila nina swali moja.., ili League iwe na ushindani, Je ni lazima viwango vya wachezaji viwe juu ? Point yangu hapa ni kwamba hata kama Messi na Ronaldo wangekuwa watanzania sidhani kama wangecheza Simba au Yanga bali wangeenda ulaya kwenye exposure na pesa nyingi..

Maana yangu hapa ni kwamba Je ni kweli kiwango cha Soka kimeshuka sana toka enzi za kina MajiMaji, Sigara, Pamba na Coastal Union ? au watu kipindi kile walikuwa wanaangalia kwa kukosa alternatives za starehe na pia ushindani ulikuwepo kidogo.. ? Maana yangu ni kwamba hata tufanye nini kwa mazingira yetu ni vigumu League ya Bongo kushindana na the likes of La Liga na EPL ila kuna uwezekano wa kufanya hii league kuwa na attachment na wakazi wa sehemu husika kuona kwamba hiki ni changu au hiki ni cha nyumbani hata kama ni kibaya ila sababu mimi ni mkazi wa Mbeya siku Timu yangu ya Mbeya City ikicheza na Mwanza au Lindi lazima nikawashabikie na hata kama sisi ni wachovu ile kuna ule upenzi ambao ni zaidi ya washabiki... Ninakubaliana na wewe kwa kufanya Timu ya Taifa iwe bora lazima academies na kukuza vipaji kuwepo..., ila kwa kurudisha uzalendo wa watu kuangalia mpira wa nyumbani lazima ushindani uwepo na watu kupenda na kusupport timu zao regionally na sio kila mtu kuwa mshabiki wa Simba au Yanga hizo nyingine ni 2nd Choice...

Mimi nakumbuka kulikuwa hakuna raha kama kuangalia mashindano ya mpira baina ya shule yetu na shule pinzani yaani ule ushabiki na upenzi unakufanya uangalie tu na siku ukifungwa unaona kweli ni aibu na nadhani hii ilisabishwa na ushindani na sio kiwango cha soka
 
Last edited by a moderator:
Binafsi nadhani Azam haitaweza kuwa kama Simba na Yanga na sababu kubwa ni ile association na watu.., yaani Mashabiki wengi hawatakuwa na ile mentality kwamba hii timu ni ya kwetu, bali ni Timu ya Azam; issue kama hii tena imeipata hata Toto ya Mwanza wakazi wengi hawaipendi sababu inaonekana ni Timu ya viongozi wachache..

Ndio maana nikasema kama shinikizo na motisha ikitolewa kwamba kila mkoa waanzishe Timu ya Mkoa ambayo watu wengi watakuwa na mahusiano na Timu husika kwamba ni Timu yao, hii itapelekea watu kuwa wapenzi badala ya kushabikia peke yake.., yaani hata timu ikifanya vibaya. Nadhani bahati hii wanayo England Utamaduni wao ni watu kushabikia Timu zinazotoka sehemu yao
Mentor njoo mpe uliyokutana nayo kwenye daladala. Mpaka udini umeingia kwenye hizi timu mbili.
 
Last edited by a moderator:
.. ila nina swali moja.., ili League iwe na ushindani, Je, ni lazima viwango vya wachezaji viwe juu?

Kwenye heading ya uzi wako ni ulitumia neno "better" tofauti na neno "ushindani" ulilotumia baadae. Kuwa "competitive" does no necessarily mean that you are the "best". Mtu anaweza kusema kuwa ili ligi iwe na ushindani siyo lazima iwe na wachezaji wanaocheza kwa kiwango cha juu sana.

Kwa mfano, inadaiwa kuwa Ligi za Russia na Brazil ndizo zenye ushindani mkubwa kupita zote duniani. Hata hivyo, Ligi ya Russia haina wachezaji ambao viwango vyao ni vya juu sana kulinganisha na ligi nyingine. Ile ya Brazil, most of their best players play abroad. Ligi ya Uingereza inaweza isiwe competitive kama inavyodaiwa, ila wao ni wajanja kwenye kui-market and kui-promote.

Maana yangu hapa ni kwamba Je ni kweli kiwango cha Soka kimeshuka sana toka enzi za kina MajiMaji, Sigara, Pamba na Coastal Union? au watu kipindi kile walikuwa wanaangalia kwa kukosa alternatives za starehe na pia ushindani ulikuwepo kidogo.. ? Maana yangu ni kwamba hata tufanye nini kwa mazingira yetu ni vigumu League ya Bongo kushindana na the likes of La Liga na EPL ila kuna uwezekano wa kufanya hii league kuwa na attachment na wakazi wa sehemu husika kuona kwamba hiki ni changu au hiki ni cha nyumbani hata kama ni kibaya ila sababu mimi ni mkazi wa Mbeya siku Timu yangu ya Mbeya City ikicheza na Mwanza au Lindi lazima nikawashabikie na hata kama sisi ni wachovu ile kuna ule upenzi ambao ni zaidi ya washabiki... Ninakubaliana na wewe kwa kufanya Timu ya Taifa iwe bora lazima academies na kukuza vipaji kuwepo..., ila kwa kurudisha uzalendo wa watu kuangalia mpira wa nyumbani lazima ushindani uwepo na watu kupenda na kusupport timu zao regionally na sio kila mtu kuwa mshabiki wa Simba au Yanga hizo nyingine ni 2nd Choice... Mimi nakumbuka kulikuwa hakuna raha kama kuangalia mashindano ya mpira baina ya shule yetu na shule pinzani yaani ule ushabiki na upenzi unakufanya uangalie tu na siku ukifungwa unaona kweli ni aibu na nadhani hii ilisabishwa na ushindani na sio kiwango cha soka

Nilishawahi kuhoji hili before kwenye uzi wangu mmoja.

_65551370_159980404.jpg


Mimi ni mshabiki wa Manchester United. Nimekuwa mshabiki wa Manchester United kwa muda wa miaka 15 sasa. Napenda jinsi wanavyocheza. Napenda staili wanayocheza. Napenda jinsi walivyo na ujasiri wa kupambana mpaka dakika ya mwisho.

Kwa kawaida huwa napenda kuangalia mechi za Manchester United na marafiki zangu kupitia vibanda maarufu vinavyoonyesha mechi hizo, almaarufu kwa jina la "vibandaumiza".

Siyo kwamba sina satellite nyumbani bali sipendi upweke. Sipendi kuangalia soka nyumbani nikiwa peke yangu. Nikiwa kwenye vibandaumiza nikiangalia soka na marafiki zangu na mashabiki wengine wa timu za Arsenal and Chelsea inanipa furaha tele kutokana na kubishana, kuzomeana, kuchekana, kupakiana mitusi na kushangilia ushindi kwa kelele.

Kwa kweli sina muda wa kuangalia mechi za timu za nyumbani. Nilikuwa naangalia miaka ya 1990 wakati timu yangu ilipokuwa ikicheza lakini siku hizi haichezi tena. Haipo tena kwenye ligi kuu. Ndiyo maana siangalii tena soka la nyumbani. Siku hizi naangalia tuu ligi za nje.

Sifurahii kabisa aina ya soka inayochezwa na timu zetu za nyumbani. Huu ni ukweli. Soka la timu za nyumbani haliburudishi kabisa. Labda ndiyo maana watu hawaangalii tena mara kwa mara. Tunapenda zaidi kuangalia mechi za nje na wewe unajua wazi kwamba huu ni ukweli mtupu.

Hayo yalikuwa maneno ya Kabir Ahmed, Kaduna kutoka Nigeria alipokuwa akihojiwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) kama sehemu ya makala inayoenda kwa kichwa cha habari “Is Satellite TV Killing African Football?” (Satellite TV inaua soka la Afrika?).

Kwa mujibu wa makala hiyo, tokea satellite TVs zilipoanza kuonyesha ligi kuu za Ulaya katikati ya miaka ya 1990, wapenzi wa soka Afrika wamekuwa hawana uhakika kama wafurahie au wahuzunike. Kwa upande mmoja, wengi wamejikuta wanapata fursa ya kuangalia klabu bora za soka duniani kupitia luninga. Kwa upande mwingine, wengi pia wamekuta kuwa ligi za nyumbani walizokuwa wanaangalia hazikuwa za kiwango cha juu kama zile za Uingereza, Uhispania na Italia.

Ni kitu gani hasa kinaua soka la Tanzania? Ni Satellite TV? Kama ni Satellite TV mbona Supersport imekuwa ikimiliki haki za kuonyesha ligi kuu za Kenya, Zambia, Uganda, Ghana, Angola na Tanzania kwa kasibu miaka saba sasa?

Ni nini hasa kinaua soka la Tanzania? Wachezaji bora wa Afrika kukimbilia Ulaya na kuacha ligi za nyumbani bila wachezaji wazuri. Hii sababu ina-apply Tanzania? Ni kwa sababu ya ligi za nyumbani kuwa na maandalizi mabovu, na kutawaliwa na rushwa, miundombinu mibovu?

Pia wachambuzi wa soka wanadai kuwa kiwango cha soka kilichoonyeshwa kwenye fainali za Kombe la Afrika siku chaache zilizopita kilikuwa cha chini sana. Kwa nini?

Soma michango ya wadau hapa walieleza mengi sana: https://www.jamiiforums.com/sports/403020-kwa-nini-mimi-ni-mshabiki-wa-manchester-united.html


 
Mentor njoo mpe uliyokutana nayo kwenye daladala. Mpaka udini umeingia kwenye hizi timu mbili.

Ni kweli kaka EMT soka la Tanzania liaathiriwa na 'udini na usiasa' jambo ambalo naona ndilo linaloangamiza taifa katika kila sekta.

Huwa napata shida kuwaza solution ya tatizo hili, si kwa soka tu...
 
Last edited by a moderator:
Ni kweli kabisa na hapa nakubaliana na wewe kwa asilimia 100. Kwanza ukiangalia tu mpira wenyewe wa Simba na yanga yaani hauna hata mvuto na ndiyo maana hata makocha wa nje wakija na kuziona hizi timu wanazikandia kwa mpira walionao. Kingine nilicho gundua ni kwamba watanzania wengi huwa hawajuwi mpira kihivyo, utakuta mtu anashabikia eti Mrisho Ngassa kukimbia uwanjani bila mpira, yaani mtu/Ngassa kakosa wazo/mbinu za kumtoka beki watu wanashangalia na utawasikia dah Ngassa bwana ana mikiki uwanjani? Kocha akiona ubovu wake na kumtoa mashabaiki wanaandamana, for what jiulize. Hizi timu bwana ni za kijinga na zinatawaliwa kwa mfumo wa kijinga. Wewe jiulize, wale wazee sijuwi kina Akilimali na kunuka mdomo kote kule anaisaidia nini Yanga? Na bado yupo tu kupiga kelele wakati hana mchango wowote klabuni zaidi ya kuleta migogoro. Kampuni ya bia ikitoa misaada yote inakwenda Simba na Yanga....kama kweli wanataka kuendeleza mpira wa Tanzania kwanini wasigawe hayo mabasi kwa timu zote za Premier League? Toa mgao sawa uone kama Simba na Yanga watashinda ubingwa bara. Tanzania vipaji vipo vingi tu huko mikoani ila mfumo wetu wa kis.enge pamoja na kukosa viongozi makini wa kuendeleza soka letu ndiyo unaoua mpira wa kibongo na kufanya ukose msisimko.

Uwepo wa mzee Akilimali na team yake inasadifu jinsi gani Mashabiki na wapenzi wa YAnga walivyo maandazi, yan wazee kama wale wazuie maendeleo badal ya kuwatimua na kuwatafuta profesional people kuendesha team.

Team ina miaka 75 ila haina hata uwanja wa mazoezi?
 
Mkuu EMT

Nadhani kujua ni wapi tunataka tufike ni vema tukajua ni wapi tulipo sasa... Maana yangu ni kwamba je tunataka kipi katika soka letu:-

Je tunataka Timu ya taifa bora ? jibu kama ni ndiyo basi hapa hakuna jinsi zaidi ya kuboresha grass root football na academies na kupata vipaji vizuri zaidi na hapa hata kama league yetu isipokuwa na ushindani sana kama talent zetu zinaweza kucheza nje basi Timu ya Taifa inaweza ikawa bora regardless ya uzuri/ubaya wa ligi yetu.

Ila mimi hapa point niliyoiongelea hata kama ligi ikiwa na vipaji na wajuzi wa soka kama hakuna ushindani basi sidhani kama watu watapenda kuiangalia.., ndio maana baada ya Bayern Kuchukua Kombe kabla ya mechi kadhaa games zilizobaki ni kama kumalizia ratiba tu, sababu there is nothing to play for. Vilevile lazima tufanye SWOT analysis ya kujua weakness na strengths na opportunities zilizopo kwenye ligi yetu, sidhani kama hata tufanye nini ligi yetu inaweza ikawa nzuri hadi mataifa ya nje yapende kuiangalia.., lakini sababu ya attachment ya watu kwamba hii ni Timu ya nyumbani ukiweka ingridient moja tu ya ushindani...,nadhani unaweza ukawabadilisha watu mtaani badala ya kuwataja Messi, Ronaldo na Wayne Rooney.., basi wawataje Messi, Ronaldo na Ngassa.., As well as kuangalia league za nje (ambazo kuna superior qualities) watu wataangalia hata ligi ya nyumbani (sababu kuna ushindani na bragging rights) so long as kuna ushindani na sio mtu kuweza kupanga ni nani watachukua kombe na nani watashuka daraja hata kabla ligi haijaanza

Mfano mzuri ni jinsi Mbeya City ilivyowaunganisha na kuwavutia wakazi wa Mbeya na kuwafanya wawe proud; sasa unadhani same thing ikitokea Simiyu na Shinyanga na Katavi ... hapo kweli hatutapata a better product ambayo hata sponsors wataona value kumwaga mapesa ?
 
Last edited by a moderator:
Azam wanapotea kivipi Kibanga?

Kwa Tabia yao ya Kuanza kugombania wachezaji wakibongo tena hawa wazeee lazima wapotee, kwani nilitegemea waige mfano wa Enyimba, TP Mazembe sasa amabo walikuwa wanasajili Vijana Africa nzima na kuwafua kisha kuwauza nje.

wao wanenda kugomba wachezaji wneye Umri wa miaka 25+(na ya kibongo maana hiyo kwa vyovyote ongeza mitano ndio utapata halisi.)


Kwa wachezaji wa Aina hii sahahu mafani kio kwenye makombe ya kimataifa, na ukiyataka lazima upate wachzaji kutoka huko kwenye nchi zenye mafanikio kama urabubi na Africa magharibi maana wanajua tayari jinsi ya kucheza humo, na sio hawa wetu wao cheza ligi ya Miezi 3 imeisha.
 
Mfano mzuri ni jinsi Mbeya City ilivyowaunganisha na kuwavutia wakazi wa Mbeya na kuwafanya wawe proud; sasa unadhani same thing ikitokea Simiyu na Shinyanga na Katavi ... hapo kweli hatutapata a better product ambayo hata sponsors wataona value kumwaga mapesa ?

Watu wa marketing wanaweza kukuambia kuwa competitive does not necessarily mean that you will sell your product more than your competitors.

Kwa maana nyingine quality ina-play part pia. Wapo watu ambao wako tayari kulipa zaidi to get/see the best. Unaweza kuanzisha mashindano ya golf pale Gymkama ukayafanya yakawa very competitive lakini kama the best of the best hawatashiriki then sana sana utapata average sponsors.

Kwenye mashindano ya riadha, Usain Bolt has dominated the 100m kwa muda, which one could argue that hii imepunguza competition maana hata kabla hawajaanza kukimbia unajua lazima atashinda tuu. Lakini kushinda kwake kila mara kumepunguza au kumeinua riadha hasa za mita 100 kwa wanaume?

Kuna ligi ambazo ni very competitive in the world lakini hazisikiki. Unafikiri ni kwa nini sponsors na TVs zinamwaga mahela ili kusponsor/kuonyesha Champions League kuliko ilivyo kwa Europa League? What are they looking for in the Champions League ambacho hakipatikani kwenye Europa League?

Pia tusisahau kuwa competition does not only mean ku-compete dhidi ya wengine. You can also compete against yourself to get the best out of yourself.
 
Siasa katika soka letu ndo inafanya ligi kudorora kidogo ujio wa mbeya city umeleta ushindan na amsha amsha kwa mashabiki maana kila wakisika mbeya city wanacheza mashabiki wengi walikuwa wanafuatilia kwa ukaribu iwe kwa mema au mabaya na hiyo ndo inayotakiwa timu zote zikiwa hivyo hata hao wadhamini mnaosema wa kurusha matangazo hayo watakuwa na moyo wa kurusha kila mechi maana watakuwa na uhakika wa kufuatiliwa na watu wengi kulingana na ushindani wa timu husika,tatizo usimba na uyanga umeteka na watu wamechoka kuona kila siku simba au yanga wanachukua kombe hata kama viwango vyao si vya kuridhisha
 
Watu wa marketing wanaweza kukuambia kuwa competitive does not necessarily mean that you will sell your product more than your competitors.

Well in football competitive does not mean necessarily utauza better ila lack of competitiveness will definetely ensure that no one will subscribe to it na mashindano hayo yatakufa kifo cha kawaida.., sababu kumbuka haya ni mashindano hivyo lazima kuwe na ushindani

Kwa maana nyingine quality ina-play part pia. Wapo watu ambao wako tayari kulipa zaidi to get/see the best. Unaweza kuanzisha mashindano ya golf pale Gymkama ukayafanya yakawa very competitive lakini kama the best of the best hawatashiriki then sana sana utapata average sponsors.
Ndio maana nikasema it depends na mchezo Golf mtu sio necessarily anashindana na wenzake vile vile anashindana ili kupata points kubwa, yaani its a skills game, golf unaweza hata kucheza peke yako just trying to beat your previous points.

Kwenye mashindano ya riadha, Usain Bolt has dominated the 100m kwa muda, which one could argue that hii imepunguza competition maana hata kabla hawajaanza kukimbia unajua lazima atashinda tuu. Lakini kushinda kwake kila mara kumepunguza au kumeinua riadha hasa za mita 100 kwa wanaume?
Again Bolt hashindani ili awashinde wale watu alionao bali anashindana kuvunja na record ya dunia, hata angekimbia peke yake watu wangeangalia sababu he is running againts time tofauti na mpira wa miguu

Kuna ligi ambazo ni very competitive in the world lakini hazisikiki. Unafikiri ni kwa nini sponsors na TVs zinamwaga mahela ili kusponsor/kuonyesha Champions League kuliko ilivyo kwa Europa League? What are they ooking for in the Champions League ambacho hakipatikani kwenye Europa League?
Sijaelewa kwenye comparison ya champions league na Europa League sababu Champions league inaishinda Europa kwa kila kitu, image yake ni kwamba its a loosers competition..

Ila kote huko nadhani tutakuwa tumetoka kwenye issue ya maana.., nadhani tukisema tufanye league yetu iweze compete the likes of leagues kwenye mataifa mengine its fighting a loosing battle hapa mimi point yangu ni kuifanya league yetu ipendwe na wazawa, wananchi na mashabiki wa nyumbani na hapo nikasema ingredient ni moja tu itakayosababisha hiki.., regionalization (yaani kufanya timu iwe ni mali au wananchi wafeel like kwamba hio ni mali yao) yaani kama watu wa mwanza wawe na association au feelings za kwamba hii timu ya Mwanza ni ya sisi wanamwanza.., hivyo hata kama Timu ya Mwanza ikicheza ugoro hawa watu wataendelea kuishabikia.., sababu hawa watu watakuwa ni wapenzi na sio washabiki peke yake.., vilevile mashirika na wafanyabiashara na wananchi wote husika wa sehemu husika watakuwa tayari ku-sponsor hizo timu zao. Na kwa kuwa na huu ushindani defenetely league itakuwa competitive na sioni kwanini itakosa internal sponsors..

Pia tusisahau kuwa competition does not only mean ku-compete dhidi ya wengine. You can also compete against yourself to get the best out of yourself.
Yes in other sports this works perfectly ila kwenye Soka kama timu moja itakuwa bora sana kuliko nyingine hii italeta monotonous na ingawa itakuwa furaha kwa wenye timu ila kwa mtu baki sidhani kama itasaidia.., Sidhani kama Bayern kuwaburuza wengine au Porto ilivyokuwa inawaburuza watu kule Portugal ilikuwa na faida sana na ndio maana watu wanasema kwa La Liga mwaka huu imevutia zaidi kwa sababu ya Atletico kuingia in the Mix... (its all about competitiveness)
 
Well in football competitive does not mean necessarily utauza better ila lack of competitiveness will definetely ensure that no one will subscribe to it na mashindano hayo yatakufa kifo cha kawaida.., sababu kumbuka haya ni mashindano hivyo lazima kuwe na ushindani

Hata biashara ni ushindani unless uwe una-monopolize the market. Pia ligi kama za Rusia na Brazil ni very competitive lakini ligi ya Uingereza is the most watched league in the world.


Ndio maana nikasema it depends na mchezo Golf mtu sio necessarily anashindana na wenzake vile vile anashindana ili kupata points kubwa, yaani its a skills game, golf unaweza hata kucheza peke yako just trying to beat your previous points.

Kwa hiyo football is not a skill game?


Again Bolt hashindani ili awashinde wale watu alionao bali anashindana kuvunja na record ya dunia, hata angekimbia peke yake watu wangeangalia sababu he is running againts time tofauti na mpira wa miguu

Ndiyo maana nikasema kuwa unaweza ku-compete against yourself.


Sijaelewa kwenye comparison ya champions league na Europa League sababu Champions league inaishinda Europa kwa kila kitu, image yake ni kwamba its a loosers competition..

Kwa hiyo Champions league ni more competitive than the Europa League. If so ni gani vinaifanya iwe juu zaidi ya Europa League. The fact kuwa Europa League league is a loosers competition does this make it less competitive?

Ila kote huko nadhani tutakuwa tumetoka kwenye issue ya maana.., nadhani tukisema tufanye league yetu iweze compete the likes of leagues kwenye mataifa mengine its fighting a loosing battle hapa mimi point yangu ni kuifanya league yetu ipendwe na wazawa, wananchi na mashabiki wa nyumbani na hapo nikasema ingredient ni moja tu itakayosababisha hiki.., regionalization (yaani kufanya timu iwe ni mali au wananchi wafeel like kwamba hio ni mali yao) yaani kama watu wa mwanza wawe na association au feelings za kwamba hii timu ya Mwanza ni ya sisi wanamwanza.., hivyo hata kama Timu ya Mwanza ikicheza ugoro hawa watu wataendelea kuishabikia.., sababu hawa watu watakuwa ni wapenzi na sio washabiki peke yake.., vilevile mashirika na wafanyabiashara na wananchi wote husika wa sehemu husika watakuwa tayari ku-sponsor hizo timu zao. Na kwa kuwa na huu ushindani defenetely league itakuwa competitive na sioni kwanini itakosa internal sponsors..

Sijui kama umefikiria kwa kina long term implications za regionalisation. Unaweza kuja kuishia kuwa na timu ya Wahaya, Wachaga, Wanyakyusa, nk. And possibly hutaweza kuichezea Haya FC kama wewe ni Manyakyusa. I would prefer a league where there is diversity. Watu wawe free ku-support timu wanayoipenda regardless ya location zao.

I would probably agree ku-regionalise ligi za madaraja ya chini, but there should be diversity in the top flights. Hata kwenye baadhi ya nchi nyingine wanapendekeza regionalisation in the lower leagues not in the top flights. Cheki kwa mfano: Would the regionalisation of football benefit the lower divisions?

Yes in other sports this works perfectly ila kwenye Soka kama timu moja itakuwa bora sana kuliko nyingine hii italeta monotonous na ingawa itakuwa furaha kwa wenye timu ila kwa mtu baki sidhani kama itasaidia.., Sidhani kama Bayern kuwaburuza wengine au Porto ilivyokuwa inawaburuza watu kule Portugal ilikuwa na faida sana na ndio maana watu wanasema kwa La Liga mwaka huu imevutia zaidi kwa sababu ya Atletico kuingia in the Mix... (its all about competitiveness)

Nafikiri ina-apply kwenye soka pia. Hata kama timu ipo better kiasi gani there are still some areas it may improve. Timu inaweza isifaidiike sana na self-competition, but this could benefits its fans and perhaps the neutrals. Self-competition might motivate you more than competing with others.
 
Hata biashara ni ushindani unless uwe una-monopolize the market. Pia ligi kama za Rusia na Brazil ni very competitive lakini ligi ya Uingereza is the most watched league in the world.
Unasema kana kwamba EPL sio competitive.., jambo la maana la kukumbuka competitiveness sio ingredient pekee bali ni ingredient muhimu EPL as well as being marketed na kuonyeshwa na TV nyingi duniani pia ni competitive na kuna talent ya one of the best players in the world, pia kumbuka sababu mimi na wewe hatuangalii Russian au Brazilian League sio kwamba wazawa wa huko hawaziangalii..., alafu kumbuka hata mahudhurio ya watu uwanjani yanachangiwa pia na kipato cha watu husika na security ya watu uwanjani, jambo ambalo English League wameliweza sana na kuweza kufanya uangaliaji wa mpira kuwa secure na family gathering ya watu kuweza kwenda kuangalia. Mfano mwingine wa league ambayo ni competitive ni Championship ya England (ligi ya chini ya EPL) ingawa talent sio kama EPL na sio watu wengi wanaoangalia kama EPL lakini bado kuna mashabiki tele wanaangalia (why..?) Moja sababu ya tabia ya watu kuangalia timu ya kwao na pili sababu ya competitiveness kila mtu anaweza kumfunga mwenzake on any given day..., kama one of those ingredients ingekuwa haipo ninakuhakikishia viwanja vingekuwa havijai


Kwa hiyo football is not a skill game?

Ofcource football is a skill game na kuna watu wanaangalia Brazil, Barcelona au Arsenal sababu ya talent/skills. Ila tofauti na comparison yako ya Golf na Mbio Fupi.., unaweza kumuangalia Tiger woods hata akicheza golf peke yake au Bolt akikimbia peke yake sababu mwisho wa siku sio ni wangapi kawashinda bali ni muda gani ametumia au point ngapi amatumia tofauti na mpira au masumbwi mshindani na yeye inabidi awe na umahili ili mchezo uvutie..




Kwa hiyo Champions league ni more competitive than the Europa League. If so ni gani vinaifanya iwe juu zaidi ya Europa League. The fact kuwa Europa League league is a loosers competition does this make it less competitive?
Ofcourse champions league ni more competitive sababu timu nyingi kutokana na kutoipa uzito (hususan timu kubwa kama zikiwa knocked out of Champions league) huwa zinaweka a second string squad and they dont care as much.. Ila hapa ni besides the point ingawa kwa neutrals wengi hawaangalii hii competition kama CL (sababu ni second string) lakini wale wenye timu zao bado wanaangalia...., hapo ndio point yangu inakuja sijasema tufanye Ligi ya Tanzania iwe bora hadi wakenya wapende kuangalia bali iwe bora hata wakazi / watanzania wapende kuangalia



Sijui kama umefikiria kwa kina long term implications za regionalisation. Unaweza kuja kuishia kuwa na timu ya Wahaya, Wachaga, Wanyakyusa, nk. And possibly hutaweza kuichezea Haya FC kama wewe ni Manyakyusa. I would prefer a league where there is diversity. Watu wawe free ku-support timu wanayoipenda regardless ya location zao.
Sidhani kama kutakuwa na ligi ya wachagga au wahaya peke yao sababu hakuna sehemu (region) ambayo wanaishi kabila moja peke yao.., nchi hii imetapakaa watu wa kila kabila, sidhani kama Mwanza kuna wasukuma peke yake au Dar kuna kabila moja kuliko mengine.., ila ikitokea timu moja ikawa na kabila moja kubwa sidhani kama ni tatizo so long as mtu wa kabila jingine hakatazwi kujiunga..., Jambo moja kubwa ambalo lifanya watu wengi wajae viwanjani katika EPL ni kwamba watu wengi wa UK kila mtu anasupport timu ya kwao (sehemu anapotoka/anapokaa) ingawa kuna timu chache kama ya Glory Hunters.. (Man United) ambayo ina washabiki wengi nje ya Manchaster na Wachache Manchester (Man City is the Most supported team in Manchester), kwahio sioni tatizo lolote la regionalization kwenye ligi yetu, pia sikusema ilazimishwe bali nimesema iwe supported / encouraged


Nafikiri ina-apply kwenye soka pia. Hata kama timu ipo better kiasi gani there are still some areas it may improve. Timu inaweza isifaidiike sana na self-competition, but this could benefits its fans and perhaps the neutrals. Self-competition might motivate you more than competing with others.
Its human nature ukiwa bora sana kuliko wenzako unabweteka, mfano mzuri utaona Timu yoyote ikichukua kombe mapema kabla ya mechi kuisha mara nyingi baada ya hapo inaanza kuchemsha na kupoteza mechi.. refer Bayern Munich this season
 
Kuonyesha kila Game kwenye TV
Kuuza rights za kuonyesha Mpira / Mechi zote kwa Pesa nyingi itakayosaidia kuwekwa kwenye Fungu la Kuzigawia Timu entrance Fee ya Washibi watakaoingia kwenye mpira ni Pesa ndogo kuzitegemea, na hazitatosha.
Kazi nzuri sana ya AZAM sasa hivi hii product nchini inapendwa kuliko product ya ligi yoyote ile duniani
 
Nili tegemea Azam wangekuwa Mfano wa kuiga lakini nimeona na wao wanapotea na soon Tutawasahau kwenye Soka.
Azam Timu au Azam Mdhamini ?

Azam Mdhamini apewe Kudos za hali ya Juu hii Product imekuwa kwenye midomo ya watu sababu ya kazi yake nzuri
 
Naweza kusema kuonyesha kila game kwenye TV limefanikiwa na AZAM apewe sifa zake maradufu..., sasa tukitaka tuendelee zaidi ni kuhakikisha mashabiki wanakuwa regional na hapo ni kwa kuwekeza kwenye Timu za mikoani na watu kuwa na utamaduni wa kushabikia timu zao za mitaani / mikoani
 
Sema ukweli, kwa 'uswahili' uliopo katika soka la Tanzania, ni kitambo sana nimeacha kuwa mfuatiliaji wa nini kinaendelea katika soka la bongo.
Nadhani baada ya coverage kuwepo kwenye TV kila game kuonyeshwa wadau nchini wanaangalia game za ndani sambamba na za nje...; kwahio kwenye hili hatua zimepigwa nadhani bado tuhakikishe Timu za mikoani zinakuwa na nguvu na nguvu hizo zitapatikana kwa Timu hizo kupata nguvu ya pesa
 
Nadhani baada ya coverage kuwepo kwenye TV kila game kuonyeshwa wadau nchini wanaangalia game za ndani sambamba na za nje...; kwahio kwenye hili hatua zimepigwa nadhani bado tuhakikishe Timu za mikoani zinakuwa na nguvu na nguvu hizo zitapatikana kwa Timu hizo kupata nguvu ya pesa
Miaka 10 imepita aisee na leo umeukumbuka uzi wako 👏👏👏👏
 
Miaka 10 imepita aisee na leo umeukumbuka uzi wako 👏👏👏👏
Na kwa kukua kwa amsha amsha ashukuriwe sana Azam kwa kuonyesha mpira / coverage kila game hii imeongeza watazamaji na watu kuzungumzia game..., ila bado kuna u-Simba na u-Yanga ikiwezekana Timu ndogo zikapataza following kutoka huko makwao huenda Soka ikawa among top Industries Tanzania
 
Naweza kusema kuonyesha kila game kwenye TV limefanikiwa na AZAM apewe sifa zake maradufu..., sasa tukitaka tuendelee zaidi ni kuhakikisha mashabiki wanakuwa regional na hapo ni kwa kuwekeza kwenye Timu za mikoani na watu kuwa na utamaduni wa kushabikia timu zao za mitaani / mikoani
Na suala la udhamini pia timu zetu zimefanikiwa sana, siku hizi hakuna timu ya ligi kuu ambayo utakuta kifuani kwenyw jezi zao kupo plain hakuna mdhamini..

Kuna baadhi ya club ndogo tu kama Namungo, Geita Gold, Singida big stars na nyinginezo utakuta zina wadhamini zaidi ya watano na kuendelea
 
Back
Top Bottom