EMT
Platinum Member
- Jan 13, 2010
- 14,477
- 15,325
Kuongeza Wadhamini
TFF na wadau watafute wadhamini zaidi, hata kuuza TV rights za kila game ili ionyeshwe na kuwashauri wadau wenye makampuni kufadhili league
Wadhamini nao ni wafanya biashara ati. Wako tayari kui-invest tuu pale ambapo watapata faida. Hakuna mdhamini wa maana atakuja kudhamini ligi ambayo haoinyeshi projections yoyote ya kuimarika. Kwa maana nyingine inabidi kwanza ligi iimarishwe. Kama ligi ikiimarishwa wadhamini watajitokeza wenyewe bila hata TFF kuwatafuta.
Kuonyesha kila Game kwenye TV
Kuuza rights za kuonyesha Mpira / Mechi zote kwa Pesa nyingi itakayosaidia kuwekwa kwenye Fungu la Kuzigawia Timu entrance Fee ya Washibi watakaoingia kwenye mpira ni Pesa ndogo kuzitegemea, na hazitatosha.
Huwezi kuuza rights za kuonyesha ligi kwa pesa nyingi wakati ligi yenyewe ipo katika hali ya chini. Hakuna TV ya maana ambayo itakuwa tayari kununua hizo rights kwa pesa nyingi. Hivyo bado ligi inabidi iimarishwe kwanza, na ikiwa imara lazima TV zitaweka bids za juu kununua hizo rights. TVs want to show the best, simply because viewers want to pay those TVs to view the best players in the game. Cheki mfano, BT Sport walivyomwaga pesa kuonyesha Champions League na kuipiga bao Sky Sports waliokuwa wanatoa pesa ya kawaida tuu.
Kuongeza / Kubadilisha Aina ya Fungu la Kugawia Timu
Badala ya Fungu la kiingilio kugawiwa timu zinazoshinda kwa percent nusu kwa nusu (baada ya makato ya TFF, Uwanja n.k.) Nashauri fedha igawiwe kwa Mafungu ya Percent Kubwa Zaidi kwa Timu itakayoshinda Mchezo husika na Ndogo kwa timu itakayofungwa (endapo Timu zitadraw) basi wote wapewe fungu dogo na zinazobaki ziwekwe kwenye Kapu na kuja kupewa Timu mwisho wa League itakayochukua Kombe.., kwa kufanya hivi nadhani kutapunguza Timu masikini kuuza Mechi; pia kila game itakuwa na maana sababu kushinda game kutakuwa na faida kubwa, kuliko kufungwa
Hapo unaweza kudhani unatatua tatizo la timu masikini kuuza mechi kumbe unaleta tatizo la timu kubwa kununua mechi na pengine kuwahonga hata marefa. Kwa wenzetu timu inayocheza nyumbani inachukua mapato yote. Tatizo kwetu timu hazimiliki viwanja. Tatizo la timu kuuza mechi ni pana zaidi na linahusisha suala zima la kuzoeleka kwa rushwa katika katika jamii yetu. Maana hata jana Liverpool si wangewahonga Crystal Palace na kubeba points zote?
Kuhakikisha / Kusaidia Mashabiki kuwa RegionalKwa sasa tumeona kwamba zaidi ya Simba na Yanga timu nyingine za mikoani hazina kabisa mashabiki.., kwahio ili kuwe na uzalendo na watu kupenda Timu inasaidia kama Timu itakuwa ina uhusiano mkubwa na mkoa inakotoka.., Kwa mfano kama kila Mkoa ikiwa na Timu yake Mfano Mwanza Heroes; au Igembensabo, au Simiyu Stars.., kwa kuanzia wakazi wa mji husika watakuwa na uhusiano na upendo zaidi na Timu zao na wafadhili local watapatikana zaidi, ingawa hizi Timu zitaruhiwa kusajili kutoka popote na kila mkoa utaruhusiwa kwa na Timu hata zaidi ya moja kwa kuanzia ila mwisho wa ligi zikishuka hata kama mkoa fulani utakuwa hauna timu itaendelea hivyo hivyo. Na kwa kuanzia Timu ambazo zipo tayari kwenye League kina Simba na Yanga n.k. zitaendelea hivyo hivyo ila kila mkoa kwa kuanzia huimizwe kuwa na Timu ya mkoa ambayo ipo kwenye league (na hii itasaidia kupata vipaji kutoka mikoani)
Huwezi kulazimisha watu kuwa wafuasi wa timu fulani ili kuimarisha regionalism in sports, but I can see where you are coming from. Miaka hiyo zilikuwepo timu kubwa na kali tuu karibia kila mkoa. Mikoa mingine kama Tanga na Mbeya ilikuwa na timu zaidi ya moja kwenye ligi kuu lakini siku hizi siyo hivyo tena.
I would say the best approach ni kuimarisha soka at the local level bila kujali regionalism. Wengine wanaita "grassroot football". Hii kitu iliwepo zamani mpaka kwenye shule za msingi. Nakumbuka wakati huo nikiwa primary tulikuwa tunashindana kikata, kitarafa, kiwilaya mpaka kimkoa. Pia kila jioni tukitoka shule tulikuwa tunaenda kucheza mpira na kujiandaa kurudi home kula kichapo.
Siku hizi hakuna hata viwanja kitaani kuchezea mpira. Zile sehemu ambazo zilikuwa wazi kumefunguliwa mashina ya vyama vya siasa, zimekuwa sehemu za kupaki magari usiku, sehemu nyingine kuna pubs/grocery na maeneo mengine ya wazi yamevamiwa na watu binafisi. Siku hizi mtoko wa vijana jioni kwenda kwenye mikutano ya siasa ambayo mingi yao inafanyika jioni kwenye viwanja hivyo hivyo ambayo vijana walitakiwa wasakate kabumbu mida hiyo. Serikali za mitaa na vyama vya soka at lower level havifanyi ya kutosha kutoa facilities na gharama nyingine za ku-support michezo at local level. Najua huko chini hawapati support ya kutosha kutoka juu na hilo ni tatizo lingine.
Juzi juzi hapa nimemsoma Wambura akiwataka waandishi wa habari za michezo wajikite zaidi kwenye habari za kunzisha, kuendeleza na kuimarisha academies za soka. Akalalamika kuwa waandishi wa habari huwa wanafocus zaidi kwenye timu za Simba na Yanga badala ya watoto. Nikajiuliza kwani jukumu la waandishi wa habari ni kuanzisha, kuendeleza na kuimarisha football academies? Kwani ziko academies ngapi so far? Pia wasomaji wa hao waandishi huwa wanapenda kusoma nini? Maana mara nyingi waandishi wa habari wanaandika kile ambacho kinapendwa kusomwa zaidi na wasomaji wao. Waandishi wa habari ni wafanyabiasha pia. They are not volunteers. Na wengine hawaandiki habari kama hawajapewa bahasha ya kaki.
It was interesting kusoma kiongozi wa chama cha soka akilaumu waandishi wa habari badala ya kuanza na chama chake kwanza. Hapo alikuwa anacheza mchezo wa kutupiana mipira kwa sababu siyo kazi ya waandishi wa habari ku-supervise football academies kama Wambura alivyodai. Siyo kazi ya waandishi wa habari kuhakikisha kuwa mchezaji anaimarika kwa kwa kuwa na the Five S alizozitaja Wambura. Wambura anajawataja akina Messi na Nymeir jinsi walivyogunduliwa lakini sidhani kama waligunduliwa na waandishi wa habari. Hata hizo nchi alizozitaja kama Brazil, Ujerumani, Uingereza, n.k wachezaji hawagunduliwi na waandishi wa habari. Kazi yao ni kuripoti na labda ku-analyse wachezaji ambao tayari wameshaguduliwa.
HITIMISHO. Nadhani kwa kufanya hayo italeta uzalendo zaidi na kila game sababu itakuwa na faida kubwa kila mshindi wa game atapata pesa na mwisho wa siku atakayeshinda League mwisho wa mwaka na yeye apate dau la pesa nyingi kulingana na Nafasi atakayomaliza nayo.Kwa kuwa kila game itakuwa na Price Tag/Kifuta Jasho kikubwa nina uhakika kutakuwa na Ushindani Mkubwa
Nadhani the best approach ni kuangalia kwanza the underlying causes ya kuwa na kiwango cha chini cha soka. Kwanza tusisahau kuwa Tanzania ilikuwa koloni la Waingereza. Tofauti na Wafaransa, Waingereza hawakuendeleza kabisa soka kwenye makoloni yao baada ya kupata uhuru. Kwa Wafaransa baada ya makoloni yake kupata uhuru, walikuwa wana-scout wachezaji kutoka kwenye hizo nchi na kupelekwa kucheza kwenye klabu za Ufaransa. This has motivated kids to want to perform at the same level as their peers.
Kuna matatizo mengine makubwa kama ukosefu wa grassroot football and kutokuwepo kwa uwekezaji kwenye soka. Pia Tanzania hakuna scouting kabisa. Simply hakuna kitu kama hicho. Sidhani hata kama kuna mtu ambaye ameajiriwa specifically kwa kazi ya scouting in Tanzania. In fact hakuna hata academy system ya kuwezesha mtu kufanya hiyo scouting. Leo kweli Arsenal au Man Utd wanaweza kumlipa mtu kuja kufanya scouting Tanzania?
Pia sababu kubwa sana ya kuwa na kiwango cha chini cha soka ni ukosefu wa political will. Kuna watu wanadhani mafanikio kwenye sekta ya michezo yanakuja hivi hivi tuu. There must be a political will. Kwa mfano, Cameroon, katika miaka ya 1980s, serikali yao ilikuja na programu (siyo mpango kama tulivyozea hapa Bongo) ya kuendeleza soka. Serikali ilihusisha sekta binafsi kujenga shule za soka. Hii ilisaidia kukuza wachezaji wazuri ambao waligunduliwa mapema sana na kuendelezwa mpaka kucheza kimataifa, ikiwemo timu ya taifa lao.
Pia Ivory Coast, serikali yao ilikuja na program kuwa nchi yao lazima icheze fainali za Kombe la dunia baada miaka nadhani 20 au 25. Wakaaza kutengeneza mazingira. Na kweli baada ya muda huo wakafanikiwa kuchezea hizo fainali. It was a strong political will followed by investment ya ukweli into the academy system ambayo ilikuja kusaidiwa na akina Jean Marc Guilou katika miaka ya 1990s. Hawa akina Droba na Yahaya Toure, na wengine hawakuanza hivi hivi tuu. Lakini hapa kwetu unasikia watu wakisema kuwa lazima tucheze fainali za zijazo za kombe la dunia. Tunapenda shortcuts wakati hazipo kwenye soka. Mcheza soka siyo kama mwanamuziki wa Bongo Fleva.
Kwa upande wa Afrika, wachezaji wenye umri kati ya miaka 6-13 wanakuwa kwenye level moja in terms of their ability on the pitch. Physically wanakuwa kwenye level moja. Pia technically na jinsi wanavyo-pass mpira vyote vinakuwa kwenye level moja. Tofauti inaanza kujitokeza kuanzia umri wa miaka 13 kwenda mbele.
Sasa tofauti iliyopo kati ya Cameroon/Ivory Coast na Tanzania ni kile kinachotokea baada ya mchezaji kufikisha umri wa miaka 13. Cameroon na Ivory Coast tayari wana miundo na michakato inayosaidia kuwaendeleza wachezaji wenye umri huo na kuwa-promote kufanikiwa kimataifa kwenye ngazi mbalimbali za timu zao za taifa na kwa nchi nzima kwa ujumla. Tanzania hatuna miundo na michakato kama hiyo na kama ipo basi hakuna emphasis ya kutosha kwenye hizo structures and processes.
Kwa hiyo ili ligi ya Tanzania iwe a better product inabidi tufikirie kwa mapana zaidi. We have to go back to the root causes ya kuwa na kiwango cha chini cha soka kwa sababu hizi sababu ndizo hizo hizo zinazofanya ligi iwe mbovu. Kwa maneno mengine solutions zako zinafaa zaidi kwa ligi ambayo tayari ni productive au projections zinaonyesha kuwa it will be productive miaka 10 au 15 ijayo.