Kuikataa Starlink Waziri na Serikali kwa ujumla iliona mbali

PerKnot

Member
Joined
Jan 15, 2018
Posts
69
Reaction score
87
Kiukweli nianze kwa kusema atukuzwe Mungu wa Mbinguni kwa kutupa neema ya siku ya leo. Moja kwa moja nikienda kwenye hoja napenda kuweka hoja mezani kama kichwa cha habari kinavyosema.

Kwa elimu yangu najua sasa tupo katika uchumi huru, unaotoa nafasi ya ushindani kati ya makapuni. Asilimia 99% ya kampuni ya simu na internet zinamilikiwa na wawekezaji toka nje, ili hali kwa Tanzania nadhani ni kampuni moja tuu ambayo ni TTCL. Hivyo kusema hilo, ni vyema serikali ingeiruhusu kampuni ya STARLINK nchini kwani pia ni uwekezaji toka nje.

Kwa kuikataa starlink naona, athari zaidi kuliko faida;

1. Bado soko la internet litahodhiwa na kampuni zile zile,
2. Huduma finyu zilizo na bei juu
3. Ukosefu wa ushindani wa ugunduzi na utafiti.
4. Tunakosa Ujuzi na uzoefu.
5. Tunakuja kuwa soko la Kenya (starlink Kenya), upuuuzi huu

Nashindwa kuendelea kuandika maana nikiliangalia hili swala na akili ya walioikataa naona kabisa, walikataa kwa maslahi yao binafsi na si kwaajili ya Watanzania.

Pia soma: Vita ya Starlink na Safaricom ni somo kwa kampuni za mawasiliano Tanzania
 
Heading na habari yako vinapingana vyenyewe.
 
Angeandika ulivyowaza wewe usingefungua Uzi na kuusoma hiyo inaitwa psychology.
 
Hueleweki
 
Upuuzi wa Nnape, hiyo ndiyo rushwa kubwa.
 
nape hatakiwi kupewa nafasi tena serikalini. abaki tu na tumbo lake lile (kidding).
 
Kwa
KWA KUONGEZEA .
Juzi nilingia mtandaoni ,kupata huduma za starlink ,nilichoshuhudia ni kuwa kuna kampuni toka Kenya inatangaza kigunga vile vidish kenya na Tanzania.


Nachojiuliza siku tukija kujua kuwa tumechelewa watakao kiwa wanakuja kufunga si watakauwa wakenya ?


Nadhani serikali ilikubali hili deal liwe chini ya kampuni tanzu yaaani starlink Tanzania ikimilikiwa 60% na starlink 30% na Ttcl 10% ziwekwe Dse.

Serikali tafadhalinii
 
Nape aliupiga mwingi, hao starlink tukiwaambia wabloku mtandao mchafu kama twita watakubali ? 🐼
 
Kila jambo Tanzania huwa lina taswira yake gizani, na huko gizani ndio waliko wenye nchi.
 
Nape aliupiga mwingi, hao starlink tukiwaambia wabloku mtandao mchafu kama twita watakubali ? 🐼
Wewe una faidika nini Starlink kunyimwa kuingia?

Unaendelea kulipa internet ya Voda gharama ni 10X ya Starlink na ya hovyo

Upo hapa unatetea makampuni ya simu nchini?Kwa lipi hasa walishakufanyia?

Au upo hapa kutetea serikali na wanasiasa wake wasiokua na AKILI yeyote?Nape ana akili?Katolea wapi?

Wewe ni consumer,na competition ikija ni better kwa consumer,high quality cheaper price

Kama unayapenda makampuni ya simu nchini yanakut0mba kila siku endelea

Plus Starlink ni LAZIMA aingie,anatoka superpower country sio some Kizimkazi village nation huko..ni simu moja ya Trump tu then everybody will stay in line
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…