Nilishakua kwenye hari unayoisema, nipo Dodoma naenda Singida, Dereva Mwanamke, anaendesha IT akiitoa Bandalini Dar anaipeleka Rwanda, Akanibeba pale njia Panda, hajalala vya kutosha toka atoke Dar jana yake, saa 8 mchana anaanza kusinzia Barabarani njia nzima anatembea yeye, mara ya kwanza nikamshtua, coz tulikua tunatembea njia isiyo yetu, mara pili akalala tena, nikamwambia mimi nimefanya kazi za Night shift, najua Uchovu ulivyo, nikamwambia paki pembeni ulale hata Dakika 15 tu ukiamka, usingizi utakata.
Akanisikiliza akapaki pembeni akalala kidogo, alivyoamka kawa mpya tukaendelea na safari, akinishukuru!
So ukiwa upo ndani ya Serikali badala ya kuikosoa kuna njia ya kuishauri kupitia Vikao, na isiposikia Ushauri, njia bora ni kujiuzuru.