Chanzo amezinguana na Mwl kwenye Assignment.
Walipewa individual Assignment, yeye akafanya baada ya kumaliza akamuomba mwanafunzi mwenzake akamfanyie typing kwa kutumia PC yake, maana yeye hana.
Wakati huo ilikuwa ni jioni mida ya saa moja na stationery walikuwa washafunga maana angeipeleka huko akafanyiwe typing.
Alisaidiwa kufanyiwa typing halafu kesho yake akaletewa akaenda kuiprint na kusubmit.
Baada ya Mwl kupitia kazi zao, wanafunzi kadhaa ikiwemo yeye ikabainika kazi zao zinafanana ndio wakaja kuulizwa kwa nini zimefana, akajieleza jinsi alivyoifanya kazi yake na akamuuliza mwenzake aliyempa amsaidie kutype kama aliigawa kazi yake kwa mtu akopi, akakataa kukiri kufanya hivyo.
Sasa Mwl akawaambia waandike Barua kujieleza kuhusu hilo sakata na sasa washaandika tayari na wamezisubmit. Hofu yake anafikiria hilo jambo ilihali yeye hajafanya kosa la kukopi ila mwingine ndio kakopi kazi yake jambo ambalo linampa stress sana.
Hajui maamuzi ya Mwl yatakuwaje.