KENZY
JF-Expert Member
- Dec 27, 2015
- 36,625
- 89,385
Hii mada ni pana sana maana inagusa maisha yetu ya kila siku ambayo yanavitu vingi sana ndani yake!.. tunaishi maisha katika dhana ya uchumi, mapenzi, Dini, siasa/uongozi, jamii n.k
Shida ipo hapa "unaishi huku unajifunza na wakati unajifunza vitu vinatokea dhahiri wala sio maigizo!"
Kama hukupata nafasi nzuri yakujifunza kuhusu maswala ya uchumi basi jua utapambanao tu!, katika namna moja ama nyengine!.
Hili swala linawatafuna wengi wao aidha hukufunzwa, hukufikiria kesho yako ama ni hali tu!, mfano mtu anaweza akaona kuanzisha familia ndio mafanikio lakini akasahau familia inagharama zake pia!, hivyo mtu anajikuta kuna mambo hajayatimiza kwasababu kinachoingia kuna mahali kinaenda!..
Hapo haujamaliza bado kuna swala la muda!, muda haujawahi kusimama. Haujawahi kukuambia "ngoja nikushike mkono twende sote!".
Wakati unahangaikia ndoto zako zitimie ndio wakati muda umekutupa mkono halafu uchumi nao unakuchumu!..😅
Hiyo ndio inaitwa kuishi huku unajifunza angali upo kwenye maisha yenyewe!.
Dunia ina elimu nyingi sana lakini inahitaji maarifa kwenye kujua ni elimu ipi uendenayo ili ikusaidie hapo ulipo, baadae na hata kizazi chako kama utabahatika kupata watoto.
Hapo kwenye elimu inahitaji uwe na ubongo mzuri katika kufikiri, kuchuja mambo n.k
Maisha yanakupa muda mchache mno wakujifunza ila unakupa muda mwingi wakuyaishi maisha!.
Lakini kumbuka ukitumia huohuo muda mchache unaweza kupata solution ya maisha yako leo, kesho na hata kwa wajukuu zako.
Niwatakie siku njema zenye afya ya akili na mwili.