Latent chaos
JF-Expert Member
- Jul 15, 2024
- 1,515
- 3,141
Jumapili njema waungwana, Natumaini kila mmoja wetu yupo salama, wengine mpo viwanja, wengine mnapambana na usingizi wa mchana nk.
Sasa ndugu zangu leo nimekaa nikakumbuka experience fulani niliyowahi kupitia field wakati naanza kazi miaka zaidi ya kumi ilopita , na kadri nilivyofikiria nikagundua kuna kitu kinachojirudia mara kwa mara kwenye maisha ya watu wengi.
Kitu kinachohusu jinsi tunavyoelewa “kuishi kama mtu mzima”.
Kuna kipindi tulikuwa field kikazi mkoa mmoja hivi. mimi na wenzangu wanne.
Tulipangiwa kuishi kwenye nyumba moja ya kampuni kwa muda wa miezi kadhaa mpaka project tulopangiwa ikamilike, na kwakuwa tuliishi wote nyumba moja hivyo kila mtu alijionea tabia za mwenzake beyond mazingira ya ofisini.
Sasa kuna rafiki yangu mmoja alikuwa jamaa flani sharp sana, kazini alikuwa moto, presentation zake safi.
Ana confidence, ana exposure, anaweza kuelezea concept ngumu na ukamuelewa ndani ya dakika chache tu.
Kwa kifupi, tulimwona kama genius flani hivi , na kiukweli alikuwa miongoni mwa wale watu wanaitwa "vichwa"
Maisha yakasonga kama kawaida lakini baada ya siku chache kuishi pamoja nikagundua kitu.
Jamaa alikuwa hajui kabisa kujihudumia na kujiongeza na sio utani.
Siku ya kwanza alipiga simu kuulizia sehemu ya kuagiza chakula wakati jana yake tumekwenda wote kula maeneo hayo.
Siku ya pili akauliza kama kuna mtu anajua ilipo dry-cleaner alikuwa anataka kufua shati lake moja.
Siku nyingine tulichelewa huko site tukarudi usiku , na kwasababu hata mamntilie wa maeneo ya pale walikuwa tayari wamefunga ofisi zao ikatulazimu kila mtu aanze kutafuta namna ya kupata msosi. Basi bwana mimi na wenzangu kadhaa tukaingia jikoni kulikuwa na unga , viungo vichache na dagaa pia. tukatengeneza kaugali chap chap na dagaa.
Rafiki yetu yeye akakaa pembeni kabisa huku akilalamika njaa inauma , nikamfata
Nikamuuliza:
“Bro hujawahi kupika hata ukiwa mwenyewe?”
Akacheka kabisa kwa kujiamini:
“Mimi sijawahi kufanya hizo vitu.”
Wengine wakacheka wakaona kawaida. Lakini mimi ile hali iliniacha nawaza sana.
Kwa sababu huyu hakuwa mtoto na wala hakuwa mjinga.
Ila alikuwa amefika utu uzima bila kujifunza basic life skills. Na kadri maisha yalivyoendelea, niligundua hii issue sio kwa wanaume tu.
Miaka kadhaa baadae nikakutana pia na baadhi ya mabinti ambao hata kufua nguo zao wenyewe ilikuwa shida. Mwingine aliniambia kabisa hajawahi kufua hata chupi yake tangu akiwa mdogo kwa sababu nyumbani kulikuwa na watu wa kufanya hizo kazi.
Na hapo ndipo nilizidi kuelewa tatizo kubwa sio gender. Tatizo ni namna jamii inavyolea watu kutokujitegemea hata kwenye vitu vya msingi vya maisha.
Sijaribu kupanga nani afanye nini kwenye mahusiano au kwenye nyumba.
Watu waishi wanavyoona inawafaa ila hoja yangu ni kwamba;
Kuna tofauti kati ya gender roles… na life skills.
Kutokujua kujihudumia ni tatizo bila kujali jinsia yako. Na naamini sehemu ya tatizo hili inaanzia kwenye malezi.
Kuna wavulana wanaolelewa wakiaminishwa kwamba kupika au kufanya usafi nyumbani “ni kazi za wanawake”. Na upande wa pili pia kuna wasichana wanaokua bila kufundishwa baadhi ya majukumu ya msingi kwa sababu siku zote kuna mtu wa kuwafanyia.
Mwisho wa siku tunapata watu wazima wenye degree zao , exposure na confidence nyingi, lakini hawawezi kufanya baadhi ya vitu basic kwenye maisha yao wenyewe.
Na ukiangalia vizuri, mtu anayejua kujihudumia huwa na uhuru fulani wa tofauti.
Anaishi na watu kwa kushirikiana, sio kutegemeana kupita kiasi au uchawa .
Hata kwenye kwenye mahusiano anaingia kama mtu mzima anayeweza kujitegemea au kujisaidia mwenyewe endapo mambo yatakuwa si shwari , sio mtu wa kutia huruma hata kwa vitu vidogo vidogo kama hivyo.
Kwa mtazamo wangu, kupika, kufua, kufanya usafi wa mazingira nyumbani
Ni life skills. Uwezo wa ku-survive na kujimudu mwenyewe kama binadamu na sio majukumu ya kijinsia.
karibuni wakuu tujadili swala hili.

- Kupika.
- Kufua.
- Kusafisha mazingira yako.
- Kujua kujitunza ukiwa mwenyewe.