Kategele
JF-Expert Member
- Oct 7, 2017
- 1,055
- 2,466
Picha linaanza napokea simu kwa ndugu zangu upande wa mama watoto wangu wanasema, samahani tunakuja kwenye maombezi kwa Mwamposa wewe kama mwenyeji tunaomba utupokee ili utupeleke kwa Mwamposa tukaombewe.
Nikasema ok poa nitawapeleka nyie njooni. Ijumaa wakaingia ndani ya jiji la Dsm nikawapokea, Jumamosi chapu nikawapeleka Kawe kuombewa, mimi nikaamsha kwenye mishe zangu za hapa jijini.
Kesho yake Jumapili waakambiwa warudi tena kweli Jumapili tena nikawarudisha kwenye ibada kama kawaida nikasema ibada ikiisha mtanistua nije kuwachukua.
Mida ya saa nane ibada ikaiisha wakanishitua nikawachukuwe nilipofika kwa Mwamposa mmoja wao akasema kuwa kuna mfanyakazi mwenzake walishawahi kufanya naye kazi miaka ya nyuma kwenye kampuni kampigia simu waonane maeneo ya PICOLO HOTEL kuna maombezi pia.
Basi bwana tukaenda pale Picolo hotel kufika pale wakatupandisha juu kuna ukumbi kule wanasali.
Nilichokikuta kule kinashangaza sana kwa kuwa ilibidi niwasubiri basi nikasema hebu ngoja nikae nisikilizie hapahapo ukumbini.
Kanisa lina waumini 13 tu, wanawake 10 na wanaume 3. Maombi yakaanza nguvu ya upako sijui nini inawashukia wakawa wanadondoka waumini wote hadi ndugu zangu nao wanadondoka.
Nikajisemea moyoni mbona haya majanga. Ikawa kama mchezo sasa wanaombewa watano waliobaki wanasimama nyuma yao kuwashikilia ili wasijibamize sakafuni. Wakizinduka wengine tena wanaombewa halafu waliodondoka wanaamka tena kuwashikilia wenzao.
Nikachoka kuangalia movie ya kitoto nikawambia oya nyie si mnadondoka humu hebu niwaache mkipona mtanishitua nije niwachukue twende nyumbani. Nimeshangaa hivi kipi kinamfanya mtu anadondoka hovyo wakati wa maombezi au ni michezo ya kuigiza?