Kuishi na mke kunataka uvumilivu wa chuma

Sasa iwe hivi,

Ili kuepuka yote hayo yanayotokea hasa kwa mwanaume yafaa unapotaka kuoa au kuolewa ni bora mkachunguzana kwa undani tabia za kila mmoja na ikiwezekana mkae katika uchumba hata mwaka mmoja au miwili ili mjuane tabia za ndani na nje nadhani kwa muda huo utakuwa umetosha sana katika kusomana na kujuana tabia na mkiridhiana basi muwe pamoja.

Tatizo hapa ninaloliona ni kwamba kila mmoja anakuwa na mhemuko wa ndoa pasipo kuchunguzana na matokeo yake ndo huja kesi kama hizi, lakini kama tungelifanya hivyo kabla nadhani kesi kama hizi zisingekuwepo.

Kuna madhaifu macheche ambayo kama wanandoa inabidi kurekebisha, lakini unapokuja kutuambia kwamba mke wangu yupo hivi au mme wangu yupo hivi mi naona siyo sahihi.

Kumbuka kwamba unapokosea kuchagua mwenzi wa kukufaa kwa mara ya kwanza kumbuka utateseka maisha yako yote, vinginevyo muvumiliane na kuchukuliana mizigo.
 
Reactions: Luv
Kitu cha Kwanza kwa mwanamke ni usafi wa ndani na nje. Wakati mwingine huwa nawaona wanawake yaani akisha pata watoto watatu wawili watatu, mapenzi yote anayahamishia kwa watoto na anamuona mme kama si chochote.

Utashangaa mme unatoka kazi, hata kukupokea hataki ndo kwanza utakuta yupo nje kanyoosha miguu na maziwa yote yako nje, sasa hapo apetite ya kumpenda itatoka wapi?
 
Preciouss, umeandka vema, lakini naona kama vile tatizo unahjaribu klizunguka, na kwa kufanya hivyo huwezi kuwasaidia wenzako, ni lazima kujiuliza, ni kwa nini mwanaume anafikia hatua ya kuchepuka, jibu ni kwamba chanzo ni mwanamke, mwanamke ndie anaeweza kumfanya mume asichepuke, atulie, ajiheshimu, wanawake wengi ni pasua kichwa, wengi hwajitambui, hawajui nini cha kufanya, mwanaume anatoka kwenye shughuli zake amechoka, amechukizwa huko alikokuwa, anafika nyumbani kwake (kwa matarajio ya kwamba atapumzisha kichwa chake) badala yake anakutana na mdomo wenye shombo wa mwanamke, hii hupelekea wanaume wengi kuamua kupitia kwenye mabaa ili huko waweze kukutana na marafiki na kupata fresh drinks na kuondoa stress, majumbani kwao hakuna amani wala utulivu, sasa ni hapo mwanaume anajikuta amejitumbukiza kwenye kufanya uzinifu, na bahati yenu mbaya, michepuko huwa wajanja sana, anajitahidi kumjengea mazingira mwanaume mpaka anasahau kwake, kwa yale maujanja, nyie mlioolewa hamuwezi chochote, mnalipua mapishi, hata ikifika usiku mume kupewa haki yake ya ndoa mpaka mpigizane kelele, yaani ni shida tupu, mjirekebishe, Biblia imeandika, mwanamke mpumbavu huibomoa nyumba yake kwa midomo yake mwenyewe, unaweza kumletea hizo zawadi mke na bado akakuoana zoba, hata kusema asante tu hakuna, mwanaume akipekeleka zawadi kwa mchepuko anapokewa mpaka na busu, badirikeni mzinusuru ndoa zenu.
Tafakari.
 
Toa HELA wewe mkeo apendeze
 
Tabia mbaya ni tabia mbaya tu mwanaye kama ni mzinifu nje hata umfanyie nini atatoka tu kuchepuka, hivi unazani wanawake hawavumilii shida za wanaume? Wanaume wengi hujifanya busy sana hawataki kuwasikiliza wake zao na kuona wanagubu badala ya kukaa chini kumsikiliza na kumpa nafasi, sasa hapo akichoka ndiyo hapo bora liende, swala la watoto ni lawazazi wote 2 usipokuwa karibu wewe unataka na mkeo awe mbali nao? Mbona miaka tulikuwa tumazaliwa mpaka watoto 10-12 na wazazi mpaka wanazikana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mke mwenye akili timamu hawezi pewa ya kutosha na asipendeze labda iwe huruka yake ya uchafu, unampa pesa kiduchu yeye afanye nini jamani toa matumizi mke apendeze

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuficha tabia ni ngumu sana..waliwabadilikia baada ya ndoa au walificha tabia kabla ya ndoa au kuna tabia zinaonekana baada ya ndoa?
Mm najua ndoa ni paradiso chochote kinyume na hapo kisiichoongeleka kikaisha basi ni mpango wa ibilisi si kila ndoa ni mpango wa Mungu
Kuna ndoa sababu ya uzinzi mimba iliingia wakaoana
Kuna ndoa sababu ya pesa mtu akaolewa
Kuna ndoa sababu ya mvuto wa nje mtu akaoa
Kuna ndoa sababu ya masters mdada akaolewa
Pia zpo za upendo wa Agape hizi wanaishi kama wachumba kwa miaka yote ya uhai wao na ndizo ndoa pekee hata uchumi ukiyumba au mmoja akateleza akafanya madudu hurejea kawaida baada ya mda mfupi na hudumu milele.
 
Barbra umetwaliwa?!
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…