Kuishi na mke kunataka uvumilivu wa chuma

Kuishi na mke kunataka uvumilivu wa chuma

Hatuku chart sana it was short chart. That's why ku trust mtu jf ni hatari people have hidden agenda
Oooh. Usijali mwaya ila kama usemavyo, japo mie naona haitakuwa hatari kuwaamini ikiwa tutakuwa na utulivu katika kuchambua wa kuwaamini.

Na sio kukurupuka tu.
 
Hata sijui naanzia wapiii kuna nn
😂😂😂😂 ngoja ncheke kwanza Dada. Maana hata huelewi pa kuanzia.

Ni hivi kuna post Demi alipost as if ye ni Me sasa Ukhuty kaiona ndio kaanza kumuuliza kama ni Me kweli.

Ila yamekwisha mwenyewe kasema alikuwa amebeba uhusika wa kina Bwana Pepsi. 😂😂😂😂😂
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]nitafutie post moja nami niuvae uhusika loooh demi kiboko wallah
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ngoja ncheke kwanza Dada. Maana hata huelewi pa kuanzia.

Ni hivi kuna post Demi alipost as if ye ni Me sasa Ukhuty kaiona ndio kaanza kumuuliza kama ni Me kweli.

Ila yamekwisha mwenyewe kasema alikuwa amebeba uhusika wa kina Bwana Pepsi. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nianze kwa kusema mimi ni kijana wa miaka 35 sasa, nimeoa mwaka wa 6 huu, na nina watoto wawili, ila ujumbe wangu wa leo vijana mnapoamua kuoa muwe mmemaanisha hawa wake zetu unahitaji akili ya ziada kuishi nao wengi wana upeo wa chini sana na wasahaulifu kupitiliza.

Hivyo kijana usipokuwa muelewa unaweza kuwa unagombana nao kwa sababu ambazo unaweza kuziepuka.

NB: Binafsi katika miaka hiyo ya ndoa nimejifunza na kushuhudia mengi upo wakati nilitaka kuachana na mke wangu kwa kelele zake na kutofuata ninachotaka mimi. Ila baadae nikaamua kumpotezea nimeamua kuwa kimya kama mjinga flani hivi ila akili kumkichwa.
======

Unaweza kutazama mkasa huu ukisomwa ktk Kipind cha JamiiLeo

======

UPDATE: 22 Novemba 2016

Wake zetu tunawapenda sana ila mnaongea mno kupitiliza. Binafsi situmii kilevi, wala si mtu outgoing kivile isipokuwa mara chache nikiwa na pesa kidogo tunatafuta outing na familia ufukweni au nje ya mji Bagamoyo ama Lushoto au Arusha.

Lakini sasa huyu mke wangu yeye hataki nifanye kazi na mwanamke yeyote, duuh! Hili kwangu haliwezekani maana kwa kazi yangu nakutana na wengi (wanaume & wanawake).

Pia usafi chumbani ni ovyo ovyo si usafi wa kitanda wala nguo za ndani, nimezungumza mpaka nimechoka, kuna wakati fulani dada wa kazi eti alikuwa anafanya usafi chumbani kwetu, bila kuingilia kati huenda angepewa na cchuup afue.

Nimeamua kuwa mhanga nafua nguo za ndani ninazozikuta kwenye tenga (zikiwemo zake) na kufanya usafi chumbani.

**Ila akili kichwani asee hapa nimechamba nimeibuka na nyaa.

27 Januari, 2017
Miaka kadhaa ya NDOA, nina USHUHUDA

29 Januari, 2017
Kujidai kusali kutwa/kucha na kushinda makanisa ni KUTAFUTA MIUJIZA huku haumuheshimu mumeo ni kujidanganya tu.



Ndoa yangu ina umri kama ya kwako.

Mwanzo tulisumbua sana, kisa hataki kufanya ninavyotaka mimi. Na niseme ukweli hiki ni kitu kinatutesa sana wanaume tunasahau wanawake ni binadamu pia wanye sifa zote za kibinadamu wakati wewe unataka aishi unavyotaka wewe yeye pia anataka uishi atakavyo yeye, magari yanagongana.

Baada ya kuligundua hilo nilikaa nae chini tukazungumza serious jamii tuliyopo inataka mwanamke aishi vipi na mme, yapi anayaweza yapi hayawezi, yapi nayaweza yapi siyawezi, zipi anadhani ni haki zake, zipi anadhani ni haki zangu na mimi pia nikamweleza tukachora msitari.

Nikienda kinyume ananilaumu na nimejifunza kukubali ikiwa nipo nje ya msitari yeye pia hivyohivyo naona kwa sasa mambo yanasonga.

Kama shetani mwingine hataingia hapo katikati pengine tukazeeka pamoja.

Nimejifunza kutambua madhaifu yake (yasiyo ya maksudi) najitahidi kuyaziba kwa moyo mkunjufu na yeye halalamiki kuna mambo amegundua ni mapungufu yangu anajitahidi kuyaziba.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ngoja ncheke kwanza Dada. Maana hata huelewi pa kuanzia.

Ni hivi kuna post Demi alipost as if ye ni Me sasa Ukhuty kaiona ndio kaanza kumuuliza kama ni Me kweli.

Ila yamekwisha mwenyewe kasema alikuwa amebeba uhusika wa kina Bwana Pepsi. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Hahahahaha ebu ngoja niitafute demi mwenza wangu yalimsibu nn
 
Back
Top Bottom