Kuishi na ndugu nyumba moja kunasababisha nashindwa kujiachia na mke wangu

Kuishi na ndugu nyumba moja kunasababisha nashindwa kujiachia na mke wangu

exalioth

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2016
Posts
2,263
Reaction score
3,897
Moja Kwa Moja Kwenye Mada

Hapa Sioni Ubaya Kuishi Na Ndugu Bali Nazungumuzia Ukiwa Na Ndugu Unaishi Nao Nyumbani Saa Nyingine Unakoswa Uhuru Wa Kujiachia Moja Kwa Moja.

Kwaupande Wangu Naona Vizuri Ni Kuishi Na Familia Yako Pekeako Bila Mchanganyiko Wa Ndugu Wengine Kwasababu Naona Hata Mambo Ya Kifamilia Yakiwa Ni Ya Siri Yanavuja Mitaani Kwasababu Wavujishaji Wanakuwa Ni Ndugu Zetu.

Mfano:

Mimi Nikigombana Na Mke wangu Majirani Wanajua Mpaka Chanzo Cha Kugombana Ila Kipindi Naishi Na Familia Yangu Huwezi Kujua Hata Tukigombana Utakuta Tunacheka Tu Utafikiri Hakuna Tatizo.

Licha Ya Majirani Hata Ndugu Ambao Wapo Mbali Huishi Nao Wanajua Mnaishije Taarifa Zinawafikia.

Kingine Nilichogundua Mfanyakazi Wa Ndani Na Ndugu Ni Vitu Viwili Tofauti Mfanyakazi Hawezi Kutoa Taarifa ya Jinsi Tunavyoishi Kwa Ndugu Zangu Ambao Siishi nao, Siri Ni Busara Kwenye Familia.

Yuda Exalioth
Jamiiforums
Geita.
 
Huna upendo na ukarimu kwa nduguzo?!

Kwani imeandikwa; “upendo husitiri wingi wa makosa”

Kujiachia bongo bana!
 
Kuishi na ndugu ni kazi sana ....hata utende wema kiasi gani watakuona mbaya tu ......mm ndugu labda aje kusalimia theni aondoke ....nikiona anakaa muda mrefu ntachofanya ni kumtaftia chumba ajitegemee mwenyewe kuepusha maneno na magomvi.....kwanza ndugu sikuiz ndio wanaoongoza kuharibu watoto
 
Hama hapo mwachie mji nenda kajenge/kapange sehemu nyingine.
Tunakoswa uwezo tu kawaida ukifanyi hivyo ni vzr sana saa nyngine kunavitu unaogaopa kuvifanya kwa kuhofia ndugu zangu wakijua kila mtu atajua
 
Sasa chagua moja watafutie mahali pa kuishi tofauti na hapo au endelea kuwakarimu tu ila itakugharimu. Lama ni watu wazima wasepe
 
Point of correction; Richa- Licha

Kama ndugu yako Ni wa kiume mwambie ajiongeze haraka iwezekanavyo, unashindwa Nini kumchana wakati huyo Ni ndugu yako na pengine Ni mdogo wako?

Kama vipi mtafutie pango Kisha mlipie miezi 2 afu ajipange mwenyewe.Ova!
 
Back
Top Bottom