Kuitwa mwizi na wananchi kuanza kushusha kipigo bila kuhoji ni kukosa ustaarabu jamii za Tanzania Bara, Wengi wamesingiziwa na kuuawa / kupata vilema

Kuitwa mwizi na wananchi kuanza kushusha kipigo bila kuhoji ni kukosa ustaarabu jamii za Tanzania Bara, Wengi wamesingiziwa na kuuawa / kupata vilema

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
Mwizi, Mwizi, Mwizi... Kusikia hii Yowe kwa watanzania wengi ni kibali cha kuanza kumfukuzia mlengwa na kujichukulia sheria kwa kumshushia kumpiga, kumponda mawe na hata kumchoma bila kumpa nafasi ya kujieleza,

Yani ile unaanza kujieleza tayari ushapigwa ngumi ya taya, umerukiwa kichwa, n.k. ukidondoka chini hesabia shughuli itaisha kwa kuondoka kwa kujikokota ukiwa kilema ama sehemu hio kuwa mahali utapofia, ponea yako labda defender ya polisi ipite utaokolewa lakini nao tayari wanakupa kesi ya wizi kwa ushahidi kwamba ulikuwa unapigwa kwa kuitwa mwizi.

Ndicho kilichotokea hata leo kwa Mandojo. Itakuwa kuna mtu alikuwa ana ugomvi nae akamuitia mwizi, labda ni yeye mwenyewe Mandojo aliibiwa lakini mwizi akamuwahi kumwitia mwizi, n.k. anayeitwa Mwizi ndio hupigwa, Hakuna maelezo !!

Yowe ya "Mwizi" inatumika kama silaha rahisi ya watu wenye nia ovu kuwatumia watu wengine kuumiza, kutia vilema na hata kuua watu wengine wasio na hatia. Hata ikitokea polisi ikawatia nguvuni watu waliojichukulia sheria mikononi, Huyo alieita mwizi anabaki salama.

Visa ni vingi sana, nikiwa chuoni tuliwahi kumpoteza mwenzetu kwa huu ushamba, Alienda kumtembelea girlfriend wake, huko alipofikia waligombana kwa kupishana kauli, alipoanza safari ya kurudi akiwa mtaani ghafla girlfriend wake akaanza kupiga yowe za kumsingizia ni mwizi, kilichofuata wananchi wenye hasira kali bila kumhoji walimshushia kipigo kikali sana hadi mauti, kisa kingine kipo mwisho wa hii post ni fundi aliekuwa anawahi kazini alfajiri ghafla anaitwa mwizi, hapewi nafasi ya kujitetea wala hakuna ushahidi, wakaanza kumpiga.

MAONI YANGU:

Tujenge utamaduni wa kistarabu tuwe na utu, kabla ya kukurupuka kuchukua maamuzi ya kupiga, kuua, kutia vilema, kuchoma, n.k. kwa kusikia yowe za "Mwizi! Mwizi huyo !", ni vema tutumie akili zaidi.

"msikilizeni huyo mtuhumiwa kisha msikilizeni na anayedai kuibiwa."

Hata kama kweli mtu ni mwizi, kitendo cha kumpiga mpaka kumuua, kumkata mikono, kumpa kilema, kumchoma, n.k. sio ustarabu.

Kama imefika mbali sana kiasi cha kutoa adhabu mtaani. ingependeza iwe ni ya viboko endapo kuna ushahidi tosha mhusika kaiba, baada ya hapo kumpeleka kwenye vyombo vya sheria.

Kwa kesi kama ya Mandojo utagundua kwamba kama angesikilizwa pamoja na aliemuitia mwizi, na hata kama wangefika mbali kumpa adhabu ya viboko au / na kumpeleka polisi, ingekuwa ni afadhali zaidi kuliko kilichotokea.

Mwezi uliopita majira ya saa 9 usiku zilisikika kelele kutoka kwa majirani wakisema "mwizi, mwizi"

Japokua nilisikia hizo kelele lakini sikutaka kutoka nje moja kwa moja kwasababu ni risk sometimes na hii nimejifunza baada ya tukio baya lililomtokea ndugu yangu.

Wakati niko ndani nikasikia sauti nje ikitokea kwenye ile nyumba iliyokua ikipiga kelele za kuita mwizi kuwa "aah wana bahati wamekimbia siku nyingine watakuja kufa kijinga"

baadhi ya majirani waliamshwa na ile sauti na ikabidi kuwauliza waliokua wanaita mwizi nini kimetokea. "Kuna wezi walikua dirishani wanataka kuiba na ndio maana tumeita mwizi"

Basi mimi niliposikia hivyo nikaona haina sababu ya mimi kutoka nje kama mwizi kasepa na hakuna alichoiba so ikanibidi niuchape usingizi tu.

Kesho yake tena majira ya saa 10 na robo usiku nyumba ile ile tena nikasikia kelele za kuita mwizi. Round hii nikachomoka na kinondo flani hivi huwa nakiweka nyuma ya mlango nikafungua geti ili niweze kukabiliana na huyo mwizi.

Katika hali isiyo ya kutarajia nikaona yule aliyeitwa mwizi anakuja kwangu na wakati huo mimi nipo getini bado sijafunga hata geti.

Huyo aliyekuwa akiitwa mwizi alikimbia na kuingia getini kwangu huku mimi nikiwa nimeduwaa. Kivipi mwizi akimbilie ndani mwangu wakati humu si sehemu salama kwake yeye wakati akijua kua itawarahisishia wananchi kumpiga kwa uraisi kwa sababu hatakua na sehemu ya kukimbilia.

Ikabidi nimfuate lakini nilishtushwa na sauti yake "Scars wananiua bure mi sio mwizi"

Nikataharuki kwa mshangao mkubwa kwasababu sauti hiyo ilikuwa si ngeni masikioni mwangu. Hapo ndipo nilipomsogelea kwa ukaribu na nikapata kujua kuwa yule ni mshkaji wangu wa kitaani.

Wakati huo alikuwa amelala chini huku damu zikimvuja kama maji, aah nilidata nikajikuta namuuliza maswali ambayo yalikuwa yananitatiza "daah mwanangu imekuaje umekuwa mwizi na mtaani wote wanakujua kuwa wewe ni fundi"?

Jamaa alijibu kwa shida sana maneno yake yalisikika kwa mbali kama mtu anayeweweseka, "Scars nilipigiwa simu kuwa kuna kazi inabidi nikaifanye na ndo maana nimejihimu asubuhi ili kuepukana na foleni maana kazi naenda kufanyia mbali. Lakini nilipofika hapa nashangaa wamenivamia na kunichoma visu kuwa mimi ni mwizi japokuwa niliwaambia kuwa mimi ni kijana wa mtaa huu huu"

Hapo nikaona niwaite vijana makamo yangu tusaidiane kumbeba mshkaji kumpeleka hospitali

Tulivyokua tunamnyanyua pale chini ndipo tulipobaini kuwa jamaa kashambuliwa vibaya sana. Shingoni kulikuwa na kitobo ambacho kilikuwa kinavuja damu ambazo zilimfanya akose nguvu ya kusimama peke yake.

Tukamchukua mpaka dispensary ya mtaani hapa ili aweze kupata matibabu ya huduma ya kwanza lakini wauguzi hawa hawakumhudumia chochote ndugu yetu wakatuambia tumpeleke Amana huku tukifuatilia PF3.

Tukakodi bajaji fasta fasta tukampakia huku akiongozana na kaka yake kuelekea hospitali ya Amana. Huku mimi nikirudi home kusafisha mazingira ya pale maana damu ilitapakaa ndani kiasi cha kufanya paonekane kama ni Vingunguti.

Majira ya saa 4 asubuhi tuliletewa taarifa kua jamaa kashafariki na ukweli halisi ni kwamba jamaa kauliwa kimakosa. Waliyemdhania kuwa ni mwizi alikimbia na walipotoka kumkimbiza wakakutana na huyu mshkaji wetu ambaye alikuwa mpita njia tu asiye na hatia akielekea kazini. Aisee nilihuzunika sana siku hiyo.

Hata kama angekua mwizi kweli Japokuwa wanasema huwezi kuthubutu kumpiga mwizi kama hukuwahi kuibiwa. Lakini hapana sio kwa kiwango cha kufikia kumpiga visu vya shingoni binadamu mwenzako bila huruma.

Halafu bora hata wagemkuta anavidhibiti kuwa ni yeye kafanya, maskini hata yule mwizi halisi aliyekimbia naye hakufanikisha kuiba chochote.

Wapumbavu wachache walikuwa wakisema siku yake ilifika

Source: Tukio lililotokea mwezi uliopita linanithibitishia kuwa "binadamu wote ni sawa ila hatupo sawasawa"
 
Mwizi, Mwizi, Mwizi... Kusikia hii Yowe kwa watanzania wengi ni kibali tosha cha kuanza kumfukuzia anaeitwa hivyo kwa lengo la kuanza kumpiga, kumponda mawe na hata kumchoma bila kumpa nafasi ya kujieleza,

Yani ile unaanza kujieleza tayari ushapigwa ngumi, umerukiwa kichwa kunachokupata mdomoni, n.k. ukidondoka chini hesabia shughuli itaisha kwa kuondoka kwa kujikokota ukiwa kilema ama sehemu hio kuwa mahali utapofia.

Ndicho kilihotokea hata leo kwa Mandojo. Itakuwa kuna mtu alikuwa ana ugomvi nae akamuitia mwizi ama ni yeye Mandojo aliibiwa akawahiwa kuitiwa yeye mwizi na waliomwibia, n.k. kinachofuata anayeitwa Mwizi ndio hupigwa, Hakuna maelezo.

CONCLUSION:

Kuna sheria ya wananchi kutojichukulia sheria mkononi lakini hii sheria ni kama pambo, ni wachache sana wanaokamatwa, Ni jambo la sisi wenyewe kwa wenyewe kujenga utamaduni wa kuanza kufanya kawaida ya kufikiri kabla ya kuua watu ama kuwatia vilema kwa kisingizio cha wizi, Mtu akiitiwa mwizi bila ushahidi wa watu kadhaa ama teknolojia ya camera basi apewe nafasi ya kujieleza
Hatari sana mkuu,Mimi uliwahi Nikita Mbeya huko,sema Mungu ni mwema jamaa alikosea kusema nimeiba nguo ya mtumba mkononi sikuwa na kitu,yeye ndio alishushiwa kipigo!
 
Me naona ata kitendo cha kumpiga mwizi tu pia sio ustarabu
kwa nin usimpeleke kwenye vyombo vya sheria badala yake ujichukulie sheria mkononi kwa kumumiza binadam mwenzako ama kukatisha uhai wake kabisa?
 
Hata kumshushia mwizi kipigo cha kutaka kumuua sio poa. Ila tatizo ni kuwa vyombo vya kusimamia sheria navyo haviwajibiki. Mwizi anajulikana ila akifikishwa polisi unasikia kaachiwa. Au wakati mwingine uswazi kuna wazazi wanakumbatia watoto wao wezi. Wananchi wanajikuta hawana la kufanya zaidi ya kujichukulia sheria mkononi kama chaputa. Kimsingi kuibiwa ni jambo baya mno linalokuumiza kiuchumi hadi kisaikolojia. Vyombo vya dola vikifanya kazi yake vizuri itapunguza haya mauaji.
 
Hii ni picha halisi inayoonesha watu hawapo sawa kiakili,kiuchumi na hata kiroho.Ana balaa la kupambana na maisha muda mwingi na kupumzika muda mfupi tena kwenye malazi duni,chakula cha kubangaiza na kesho yake isiyoeleweka.Hapo lazima kitu kidogo kikimkwaza ni rahisi kuonesha ukichaa wake na kufanya mambo hatari na ya hovyo.Hakuna subira wala kuomba maelezo.Mtu huyo duni anaona akifanya ubaya kwa mwenzie ni kama anajiponya nafsi yake kwa uchungu wa maisha yake magumu.
 
Ni tabia ya kishenzi sana, hata kama mmejaaliwa kuwa na roho mbaya na kutamani kuua watu basi angalau msikilizeni huyo mtuhumiwa.

Kisha msikilizeni na anayedai kuibiwa. Miaka ya nyuma kidogo pale mabibo hosteli kuna dogo aligombana na demu wake basi demu akamwitia mwizi, acha kijana ale kipigo. Angalau wale watoto wa chuo walikumbuka kumhoji kabla hawajamuua, wakagundua ni mwenzao kabisa na amezushiwa tu.
 
Duh jamaa akaponea chupu chupu.
 
Mwizi, Mwizi, Mwizi... Kusikia hii Yowe kwa watanzania wengi ni kibali cha kuanza kumfukuzia mlengwa na kujichukulia sheria kwa kumshushia kumpiga, kumponda mawe na hata kumchoma bila kumpa nafasi ya kujieleza,

Yani ile unaanza kujieleza tayari ushapigwa ngumi ya taya, umerukiwa kichwa, n.k. ukidondoka chini hesabia shughuli itaisha kwa kuondoka kwa kujikokota ukiwa kilema ama sehemu hio kuwa mahali utapofia, ponea yako labda defender ya polisi ipite utaokolewa lakini nao tayari wanakupa kesi ya wizi kwa ushahidi kwamba ulikuwa unapigwa kwa kuitwa mwizi.

Ndicho kilichotokea hata leo kwa Mandojo. Itakuwa kuna mtu alikuwa ana ugomvi nae akamuitia mwizi, labda ni yeye mwenyewe Mandojo aliibiwa lakini mwizi akamuwahi kumwitia mwizi, n.k. anayeitwa Mwizi ndio hupigwa, Hakuna maelezo !!

Binafsi nakumbuka nikiwa chuoni tuliwahi kumpoteza mwenzetu kwa huu ushamba, Alienda kumtembelea girlfriend wake, huko alipofikia waligombana kwa kupishana kauli, alipoanza safari ya kurudi akiwa mtaani ghafla girlfriend wake akaanza kumwita mwizi, kilichofuata wananchi wenye hasira kali bila kumhoji wakaanza kumshushia kipigo mpaka mauti, wananchi walitumika kutekeleza nia ovu ya huyo mwanamke.

MAONI YANGU:

Tujenge utamaduni wa kistarabu tuwe na utu, kabla ya kukurupuka kuchukua maamuzi ya kupiga, kuua, kutia vilema, kuchoma, n.k. kwa kusikia yowe za "Mwizi! Mwizi huyo !", ni vema tutumie akili zaidi.

"msikilizeni huyo mtuhumiwa kisha msikilizeni na anayedai kuibiwa."

Hata kama kweli mtu ni mwizi, kitendo cha kumpiga mpaka kumuua, kumkata mikono, kumpa kilema, kumchoma, n.k. sio ustarabu.

Kama imefika mbali sana kiasi cha kutoa adhabu mtaani. ingependeza iwe ni ya viboko endapo kuna ushahidi tosha mhusika kaiba, baada ya hapo kumpeleka kwenye vyombo vya sheria.
Nikiwa msasani NAMI vibaka waliita mwiz ilanawafaham, asubuhi walikuja omba msamaha
 
Back
Top Bottom