Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Hapa Tanzania watu wengi huchukulia kujenga na kumiliki nyumba ni hatua kubwa ya mafanikio katika miasha. Wafanyakazi wengi hukopa na kuishi na madeni ya viwanja na nyumba maisha yao yote ili tu wasikae katika nyumba za kupanga.
Pia wafanyakazi wengi wako tayari wasiwe na chanzo kingine chochote cha kipato kwa kuelekeza pesa yao yote wanayoipata katika ujenzi wa nyumba badala ya uwekezaji unaoleta fedha ili tu waishi katika nyumba zao wenyewe.
Katika muktadha wa utaalamu wa kifedha ni sahihi hasa kwa vijana kuelekeza nguvu na pesa zote katika ujenzi badala ya kuwekeza pesa katika biashara ambazo zitazalisha pesa zaidi na baadaye ndipo suala la ujenzi wa nyumba lifikiriwe baada ya kuwa na uhakika wa mtiririko mzuri wa kipato cha uhakika?