Kujenga na kumiliki nyumba ya kuishi ni muhimu kwa watu wa kipato cha chini?

Kujenga na kumiliki nyumba ya kuishi ni muhimu kwa watu wa kipato cha chini?

Kuwa na maamuzi sahihi ni kipaji:
Watu A, B, C, D,E, F walikopa bank, kila mmoja sh. 20m kwa marejesho ya jumla ya sh. 36m kwa muda miaka 6, Kila mmoja aliamua kuwekeza fedha yake kama ifuatavyo:-
Mtu A
  • Aliamua kuwekeza fedha yote kwenye ujenzi wa nyumba, na nyumba haikumalizika iliishia kwenye kupaua.
Mtu B
  • Aliamua kuwekeza kwenye ujenzi wa nyumba ndogo,na ilimalizika na hatimaye aliweza kuhamia
Mtu C
  • Aliwekeza milioni 10 kwenye ujenzi na kumi kwenye biashara ya kuuza vilevi
Mtu D
  • Aliwekeza fedha yote kwenye ujenzi wa ofisi ya ushonaji,ofisi imekamilika ila vitendea kazi bado kukamilisha
Mtu E
  • Aliwekeza fedha yote kwenye usafiri wa kutembelea
Mtu F
  • Aliwekeza fedha yote kwenye bashara ya vifaa vya ujenzi

Swali,je baada ya miaka sita (6) hawa watu (A,B,C,D,E,F) ni yupi atakuwa na maisha ya kuridhisha?
 
Unaona jinsi ulivyo muoga? What is 50? Muhimu uwe na hela tu maana ukiwa na hela hata watoto wako utawapa hizo nyumba ukiwa na 50. Tafuta hela nyumba itakuja as a by-product na sio unajikakamua hadi ukose hela ya kula kisa unajenga.
Bro tukutane ukiwa na 50 years ukiwa na hela nyingi alafu huna nyumba
 
Duniani tunapita tu, sasa kwa nini nijenge njiani?🙂🙂🙂🙂, Mimi masuala ya kujenga nyumba, mfano ya milioni 70, halafu niipangishe kwa laki 3 au laki 4 nipate hizo kodi.. kwanza inategemea na niliko ijenga (hata nikiishi mwenyewe baado).. hesabu zake ni baada ya miaka 15 au 17 ndo narudisha milioni 70 yangu niliyo jengea, hapo sijaweka hela niliyo nunulia kiwanja, repair, kodi ya ardhi na kodi ya majengo ya serikali na asilimia zingine.

Sasa hela hiyo si bora nika fanyie biashara ndani ya muda huo wa kusubiri kodi izalishe faida na mafaida.. au hela nilio weka irudi mara buku.. Milioni 70 ntakayo wekeza kwenye biashara ni lazima italeta faida kubwa mara idadi itakayo jizungusha.. potelea mbali mawazo ya kupata hasara..(biashara haidanganyi ukiwa serious na una imani) kwan ukijenga likaja tetemeko au bomoa bomoa na hulipwi fidia kama wale wa kimara ile inakuaga ni faida ?
 
Yupi huyo? Kujenga ni woga tu. Hata ukisoma humu sababu za watu utasikia mara unaweza kupoteza kazi ukakosa kodi,mara biashara itakufa utakosa kodi,ada. Ukiangalia deep unaona ni woga tu. Muhimu tafuta hela, jenga kwa starehe sio hadi unajibana hela ya kula kisa woga utalala nje!
Mkuu umenena point za maana. Jenga kwa hela ya faida isiyokuumiza kichwa jenga baada ya kuwa financially stable kwanza utajenga nyumba kali sana na mambo yako hayatayumba.
 
Nyumba ni asset kama ukiipangisha but ni liability kama ukiishi wewe.

All in all it's all about your dreams and plans and your priorities.
Huwezi fanya kila kitu asset.
Ujenge then wewe ukapange...☹️
 
Kama huna kipato cha uhakika inabidi ukazane na ujitihadi kupata kipato cha uhakika na sio kukumbilia kuzika pesa kwenye kiwanja na nyumba ambayo haitakusaidia kupata hicho kipato cha uhakika.
Jamaa una akili nyingi sana, i like the way unavyo fikiria wisely
 
Kwa nchi kama TZ nyumba bora za kuishi ni chache sana, hivyo ni muhimu sana kuendelea kujenga hata kabla ya mishe zingine.

Usilinganishe na nchi za watu ambako nyumba za kupanga zipo kila pale, labda na sisi tutafikia huko lakini sio leo.
Mtu mmoja yupo Canada alisema kule ni kupanga tuu. Kujenga ni gharama kubwa sana. Pia nyumba za kupanga zipo vizuri....ni za serikali. Hata Sweden...na nchi zote za Scandinavia
 
Hii hatua hata Mengi alikufa haijafikia ndio maana alikuwa anakomaa kusaka
Wanaokomaa kusaka pesa sio kwamba wote hawako financially stable, kujilimbikizia pesa na mali, kutaka kuwa juu ya wengine ni hulka na asili ya binadamu.
 
Wanaokomaa kusaka pesa sio kwamba wote hawako financially stable, kujilimbikizia pesa na mali, kutaka kuwa juu ya wengine ni hulka na asili ya binadamu.
Kama unajua ni hulka ya binadamu...itafika wapi ndo ujue upo stable?
Unapopata ela na wazo la ujenzi wewe fanya
 
Biashara ni kipaji na ni hobby pia.

Mimi binafsi nikifanya biashara,siwezi pata kiu ya soda halafu mezani kuna buku naiangalia.

Unawezaona ni kwa namna gani biashara sio fani yangu.

Kingine inabidi tushukuru wafanyakazi wa aina hiyo,maana wanawapisha wasio wafanyakazi nao waishi kupitia biashara, vinginevyo itakuwa ni urafi na roho za ubinafsi.
mkuu umenena vyema sana

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Wewe wekeza kwenye biashara nunua hiace ndani ya mwaka imekujengea wewe tuache masikini tukimbilie nyumba tuishi kwa Uhuru kwa kujiachia tukiondoa wazo la kulipa Kodi.
Ada za watt tunajenga nyumba inasomesha watoto. Yaani kila mtt akiwa na nyumba yake unamkabidhi ndio anaiomba hela mie sipendi kuombea hela.
Yaani namuwezesha kila mmoja anasimama kwa miguu yake.
Yaani ukiniomba hela nenda ukachukue kule Kodi nabaki mie naishi kwa Uhuru Tena ndio nawagongea.
Hii aliifanya mama kipindi bado mimi na ndugu zangu tunasoma.

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Kuwa na maamuzi sahihi ni kipaji:
Watu A, B, C, D,E, F walikopa bank, kila mmoja sh. 20m kwa marejesho ya jumla ya sh. 36m kwa muda miaka 6, Kila mmoja aliamua kuwekeza fedha yake kama ifuatavyo:-
Mtu A
  • Aliamua kuwekeza fedha yote kwenye ujenzi wa nyumba, na nyumba haikumalizika iliishia kwenye kupaua.
Mtu B
  • Aliamua kuwekeza kwenye ujenzi wa nyumba ndogo,na ilimalizika na hatimaye aliweza kuhamia
Mtu C
  • Aliwekeza milioni 10 kwenye ujenzi na kumi kwenye biashara ya kuuza vilevi
Mtu D
  • Aliwekeza fedha yote kwenye ujenzi wa ofisi ya ushonaji,ofisi imekamilika ila vitendea kazi bado kukamilisha
Mtu E
  • Aliwekeza fedha yote kwenye usafiri wa kutembelea
Mtu F
  • Aliwekeza fedha yote kwenye bashara ya vifaa vya ujenzi

Swali,je baada ya miaka sita (6) hawa watu (A,B,C,D,E,F) ni yupi atakuwa na maisha ya kuridhisha?
F ni uhakika tena analejesha mkopo na kuumaliza kabla ya ya miaka sita. huyu ataishi vyema sana maana hii biashara ni kubwa na inafaida sana.

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom