Umeongea vizuri sana, kuna dhana potofu sana kwamba kila mtu anaweza biashara, wakati si kweli kabisa. Miaka ya nyuma niliwahi kuwa na mchepuko nikaufungulia biashara, tena kwa kukopa pesa mahala, lipa kodi ya fremu miezi mitatu, nunua mzigo wote, leseni etc... Nikapotea kikazi kama miezi mitatu hivi, aisee kurudi fremu nyeupe!! Nikakuta sanduku zima kajaza nguo na vikoro Koro vipya. Nikafuatilia kwa jirani zake story walizonipa nikachoka, nikamwambia funga fremu hiyo. Baada ya mwezi binamu yangu from village alipoona pamefungwa akaniomba na yeye ajaribu hiyo hiyo biashara kwenye hiyo fremu. Basi nikampa nusu mtaji na kulipa kodi mwezi mmoja, aisee alikomaa after three months fremu imejaa kupita ilivyokuwa mwanzo, na aliendelea mpaka akawa na maduka mawili.