Kujenga na kumiliki nyumba ya kuishi ni muhimu kwa watu wa kipato cha chini?

[emoji1787][emoji1787][emoji1787] nijenge wapi bwana hata ya matope sina. Kwanza electronics unamaanisha vitu kama simu na vifaa vyake? Au vifaa vya umeme wa nyumbani? Sijuagi kutofautisha mwenzio

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
Mimi nauza simu na vifaa vyake.

Kumbe mjengo badobado! ukimaliza unifanye kiben 10 basi..
 
Kwa mimi ninavyoona, biashara inahitaji utulivu na maarifa zaidi namna ya kutengeneza faida kupitia hiyo biashara husika sasa utakuta vijana wanawekeza pesa na nguvu kwenye kujenga nyumba zao ili wakiwa huko wapate utulivu kwanza wa akili na mawazo.

Ukikaa kwa nyumba za kupanga kuna muda utulivu wako utakuwa unaondoka kutokana na usumbufu kwa either mmiliki wa nyumba kwani anaweza akajitokeza mtu mwenye kipato zaidi anahitaji nyumba uliyopanga kwa matumizi mengine na mwenye nyumba akakupa notice.

Huwezi kutulia kwenye biashara na kutengeneza faida kama unakuwa mtu wa kuhama hama utakuta faida unayoitengeneza kwenye biashra unaitumia kuwalipa wamiliki w nyumba na ukashindwa kujenga.
 
Biashara inataka roho ngumu

Kupoteza ni sehemu ya game ila unafanya tena na tena mpaka unatoboa.
 
Nakupa maua yako mkuu,
Tatizo ni Woga
Sisi watanzania ni waoga mno,
Hii inachangiwa pia na kujifungia ndani (Tanzania) hatutoki kujifunza wenzetu wanafanyaje biashara, wanaishije, wanapambanaje, wanakabiliana vipi na changamoto.

Tumejifunga mno na tunakatishana tamaa wenyewe kwa wenyewewenyewe na ndio maana uchumi wetu umeshikiliwa na wageni (Wahindi na waarabu)
 
Bora kujenga kwanza kuliko kuanza biashara ambayo hujui hatma Yake itakuwaje.
 
Punguza mikwara, mm nazungumzia gharama za vifaa vya ujenzi sio vyanzo vya pesa vya mtu yaan ata ujengee lwa pesa ya chumajlete bado gharama ya vifaa vya ujenzi bongo ni ghali ..umeelewa hoja yangu ?
HOja yako ni gharama ya vifaa vya ujenzi.

Unalalamikaje vitu bei kali wakati bei hupangi wewe ndugu yangu.

Anayepanga bei ni mfanya biashara kutokana na anavyoiona biashara yake.

Unapolalamika bei ya vifaa vya ujrnzi ni ghali maana yake una bei zako mfukoni ambazo haziendani na bei za wenzio wanaouza vifaa hivyo.

My point ni kwamba hakunaga kitu bei kali,ni kwamba hatunaga hela tu.

Nadhani nawewe umenipata mkuu.😄
 
Sio kila mtu anaweza kufanya biashara,na sio kila mtu ana muda wa kufanya biashara.
Pia,sio kila mtu anaweza kupata ajira, sio kila mtu anakopesheka.
Upepo wako ulipo ndilo chaguo utakaloamua kufanya.
Huwezi kufanya kila kitu na huwezi kuwa na kila kitu.
Ova!
 
NIMEKWAMA NAUZA ENEO LANGU KIBAHA KWA MFIPA.

LIKO SEHEMU NZURI HUDUMA MUHIMU ZIPO.
NGUZO MBILI ZA UMEME MPAKA SAITI.
MCHANGA UKO HAPO HAPO
TOFARI MAPAKA SITE TSH. 750
MAJI YAPO JIRANI TUPO KWENYE MCHAKATO WA KUYAINGIZA
KUTOKA MAIN ROAD KM. 1.5

Square mita 300
Bado sijapata mteja sahihi.
NATAKA MIL. 1.5

0685223804
 
Woga wa maisha ndio unapelekea maskini kujenga badala ya kuwekeza wawe na cash flow.
 
Sasa kama huwezi kufanya biashara si unawapa hizo fedha wenye kujua biashara wakuletee gawio.
Nunua hisa DSE, nunu vipande UTT, nunua bondi BOT.
Tatizo maskini mmekariri umaskini.
 
Sasa kama huwezi kufanya biashara si unawapa hizo fedha wenye kujua biashara wakuletee gawio.
Nunua hisa DSE, nunu vipande UTT, nunua bondi BOT.
Tatizo maskini mmekariri umaskini.
Sio lazima kila mtu kufanya biashara!
Na sio wote wafanye biashara moja!
 
Nyumba ni asset kama ukiipangisha but ni liability kama ukiishi wewe.

All in all it's all about your dreams and plans and your priorities.
Labda upangishe kwa Foreigners hasa Wazungu, ukipangisha kwa Mswahili Rental Income=Maintenance Costs.
 
Hasa kama kodi ya nyumba unalipa kila baada ya miezi mitatu au zaidi. Unampelekea mwenye nyumba sh 900,000 kwa miezi 3 inauma sana. Mimi niliwahi kupanga mahali fulani kodi ya nyumba ilikuwa sh 250,000 halafu Mshahara wangu mpaka makato napata sh 900,000 kwa mwezi. Nilikuwa nalipa kodi ya nyumba sh 750,000 kwa miezi 3. Ilikuwa inaniuma sana, ilibidi nimwombe mwenye nyumba niwe namlipa kodi kila mwezi yaani sh 250,000. Nilipojenga nyumba yangu nilifurahi na ninaishi maisha ya raha sana. Sasa nimejikita kwenye Biashara na Kilimo, siwazi tena masuala ya kodi ya nyumba.
 
Suppose unajenga hapo hapo Tabata karibu na ulipopanga. Gharama zitakuwaje ndugu yangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…