Kujenga na kumiliki nyumba ya kuishi ni muhimu kwa watu wa kipato cha chini?

Nyumba inakuaje liability ukiishi wewe?
Ni liability unless haujaingia madeni kuijenga ndipo uishi nitakupa mfano.

Wewe umepata kazi, mshahara wako ni 1milion. Unapanga nyumba lets say tabata. Kazini ni posta. Kodi ya nyumba ni laki 2. So unabakiwa na laki nane kudeal na expenses na utility za nyumba nje ya kodi. Hapo kutoka tabata ni approximately km 12 hadi kazini kwako posta so mafuta ya gari no cheap plus unaenda na mkeo na watoto pengine unawadrop shule.

Sasa ukaamua kufanya ujenzi, possibility ya kupata kiwanja katika eneo la mzingo wa kipenyo kamili cha duara cha ndani ya KM 30 kutokea hapo tabata ni uongo. Yaani ukienda chanika viwanja ni huko zaidi ya KM 20+ hadi 30 kutoka hapa tabata. Ukienda kigamboni ni maeneo ya umbali wa KM kuanzia 30+ ndipo viwanja vilipo, na ukienda upande wa morogoro road na bagamoyo road ni zaidi ya KM 35+ kupata viwanja.

Haya haya maeneo yenyewe ukienda utaambiwa yanaanza kuuzwa kwa bei za ghafla yaani milioni 5. So lazima ujipange na hiyo pesa. Then ukishalipia hivyo shughuli inabakia kuanza ujenzi. So itakubidi uwe na cash ili ujenzi uende chap au ukakope ili upate cash ya kuanza huo ujenzi.

Then ukimaliza inabidi ufanye kuhamia sasa makazi mapya. Of which itabidi watoto kuhamishwa shule, au kama watabakia shule hizo hizo basi itakulazimu kuingia gharama ya kuwapeleka mwenyewe au wakae boarding.

Then kuna swala la umbali sasa kumbuka sasa hivi utakuwa kwa siku unatembea KM zaidi ya 60+ au hata KM 70+ per day ambayo ukija piga kwa mwezi ni zaidi ya laki 6 kwenye usafiri tu.

Plus kule mji mpya kuna vitu vingi sana utakosa maana wakati wa ujana unatakiwa kukaa na vijana wenzako mpange mishe za maisha na utafutaji.

Sasa utarudi nyumbani saa ngapi kukaa na familia na utakaa na wenzako saa ngapi kuyajenga.

Hiyo laki sita ya kila siku plus unadeni la kumalizia kulipa ndio mwanzo wa mateso umehamia kwako ila stress pale pale na kudhoofu juu ndio maana watu wengi wanaohamia nje ya mji nyakati hizi za ujana mambo huwa yanaishia pabaya sana.

Maisha ni sayansi na hesabu. Tengeneza formula yako ambayo variables zake zitakuwa ni vigezo vyako ili uishi vizuri kipindi chako cha ujana ili uzeeke ukiwa na afya nzuri na ukajenga nyumba yako ya uzee ili ukaishi kipindi cha utu uzima kwa utulivu kabisa huko nje ya mji.

Sio unatoka kukwepa kulipa kodi ya tshs laki 2 unaenda kukaa nje ya mji huko ambao gharama za usafiri tu ni zaidi ya laki 6 kwa mwezi na bado nyumba haijaisha plus madeni ya mikopo unatumia miaka mingi unaishi kwa wasi wasi na maumivu. Wakati hiyo laki sita ungelipa kodi na laki nne ingebakia kusapoti usafiri na gharama zingine za familia plus upo karibu na town so gharama zitakuwa chini.

Hapo ni bidii yako tu kupambana na biashara ndogo ndogo ili uweze kuongeza kipato na kusave kiasi cha pesa cha kutosha kuanza ujenzi na kuumaliza bila kutegemea mkopo popote.

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Umeelezea kila kitu.
 
Yaani jinsi watu wanavyoongelea biashara kwenye huu uzi ni Kama vile kupanda basi kutoka makumbusho kwenda ubungo. Ukweli ni kwamba hakuna kazi au mishe rahisi katika maisha. Wengi humu tuna ndugu zetu tumewaona wamepewa mitaji lakini biashara ikashindikana. Wameishia kukosana na ndugu au jamaa zao. Hata biashara siyo rahisi kama tunavyoaminishwa humu. na siku zote tujitahidi kutofautisha biashara na uchuuzi. Watanzania wengi ni wachuuzi siyo wafanyabiashara.

kuhusu ujenzi wa nyumba, Mimi mpaka leo naamini Kuna vitu kwenye maisha ni priceless. Huwezi vithaminisha na chochote. Mimi nyumba yangu ya kuishi hata kama ningetumia million 800…..naamini kabisa ni sahihi. Kwa sababu ni nyumba nitaishi Mimi. Ni Kama leo uniambie una nyumba mbezi beach au mikocheni au any other prime area. Unapangisha, then wewe unaenda kuishi in the middle of nowhere. Fanya hivo kama huna namna kabisa!

Siyo kila kitu unachokifanya kwenye maisha kikupe monetary benefits. Ndo maana mtu akisema kwamba nyumba ya kuishi mwenyewe ni liability..hatuwezi kuelewana. Maisha na uhai wangu havina bei. in fact kufurahia maisha kwenye makazi mazuri kwangu ni Zaidi ya kila kitu.

Anyway, tuendelee kutafuta hela. Ndo kilituleta Napa Mjini.
 
Biashara kabla ya ujenzi unatakiwa uwe makini sana, biashara ina sayansi yake. Nashauri jenga kwanza huku unafikiria hiyo sayansi ya biashara. Kumbuka katika mahitaji makuu ya binadamu, nyumba ipo ila biashara haipo, tafakari.
Ukijenga kwa mkopo kama sio nyumba ya biashara, umejipakata
 
Aisee bora kujenga kwanza nilijiaminisha kujenga ni uoga wa maisha nikafungua biashara. Ulipita upepo kidogo nikaona nitakosa vyote nikahamia kujenga kwasababu ukiwa na nyumba hata mambo yaende vibaya namna gani nyumba haiwezi kuyumba ila biashara ikiyumba unaweza kuchanganyikana

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Kiukweli ujenzi sasa iv ni gharama sanaaa vitu vya ujenzi vipo juu mnooo
UNajengea mshahara wenye mkopo alafu usione ujenzi ni gharama mzee ?

Acheni kulazimisha vitu wakuu,watu tukomae kusaka channel za biashara.
 
Kumbuka katika mahitaji makuu ya binadamu, nyumba ipo ila biashara haipo, tafakari.
SASA KITEndo cha nyumba kuwa ni hitaji kuu ndio kinafanya tusianze na ujenzi kwa sababu hata kula ni lazima lakini hakuna anayeenda kukopa pesa benki ili awe anakula tu au yupo ?

Kuoa ni hitajio la muhimu lakini je mtu akienda kukopa benki ili aoe tutamuona mjinga sio ?

KUpumua ni hitaji la muhimu lakini je mtu akienda kununua mitungi ya oksijeni akaiweka ndani ili imsaidie endapo atakosa pumzi tutamuonaje kama sio ni mpuuzi ?,lakini why tumuone mpuuzi ?

Jawabu ni kwamba katika haya maisha hatutakiwi kujikalifisha kwa ajili ya mambo ya lazima,mambo ya lazima yatakuja tu,kwanza tufanye mambo ya hiari alafu yale ya lazima yatajiseti baadae.

Biashara ndio jambo la msingi kwanza
 
UNajengea mshahara wenye mkopo alafu usione ujenzi ni gharama mzee ?

Acheni kulazimisha vitu wakuu,watu tukomae kusaka channel za biashara.
Punguza mikwara, mm nazungumzia gharama za vifaa vya ujenzi sio vyanzo vya pesa vya mtu yaan ata ujengee lwa pesa ya chumajlete bado gharama ya vifaa vya ujenzi bongo ni ghali ..umeelewa hoja yangu ?
 
Kujenga sio lazima ila kwenda kwenye starehe ni kitu cha lazima sana kwa kijana yoyote. Unajenga nyumba utazikwa nayo?
 
Hahahaha! nyumba si umeshajenga
muda wa matumizi huu sasa, acha upare
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] nijenge wapi bwana hata ya matope sina. Kwanza electronics unamaanisha vitu kama simu na vifaa vyake? Au vifaa vya umeme wa nyumbani? Sijuagi kutofautisha mwenzio

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom