Kujenga nyumba ni usumbufu sana

SASA mkuu Kwa wale ambao ubize ni 24/7 inakuwaje?? Yaan hata ukiweka kampuni ya ujenzi inabidi uwepo pia kufuatilia Kama nondo wamelaza Kwa usahihi.

Kuna Ile unafuatilia Ila huna maarifa ya ujenzi haha mafundi wanakutajia vifaa Kwa kingereza mara ringbeam mara sijui vitu gani.....

Kwenye mitaala labda hata na hili somo la mambo ya ujenzi lingekuwepo Kwa sababu katika maisha zaidi ya asilimia 70 ya watu hupitia hatua ya kujenga. Kuliko kujifunza mambo ya mtemi mirambo na chief samore toure

Wenzetu nje wanajengaje?? Hivi wale wakina rashford nawao wanshindaga site kusimamia?? Labda tungejifunza kupitia wenzetu.
 

Ukitaka kujenga kwa sasa mkuu ni kukabana site usiibiwe sana(coz kuiba wataiba tu).

Kampuni za ujenzi zina escalate gharama coz kuna mambo mengi kama kampuni wanahitaji kulipa serikalini. So ukiweka kampuni kubaliana na gharama kubwa za ujenzi.

Mafundi wetu sio wabaya kama utawasimamia, lazima ujifunze na kuujua ujenzi, materials, gharama za ufundi, hatua za ujenzi nk.

Ni kweli haya mambo tunayahitaji mashuleni, vijana wafundishwe ABC za ujenzi kuliko historia zisizo na mashiko kwa dunia ya sasa.

Wenzetu serikali zao zinajenga, wewe unapewa mortgage contract utalipia miaka buku haha. Au wale wenye uwezo wanajenga na makampuni, lakini pia swala la weledi na uaminifu kwao ni kila kitu.
 
Ujenzi mgumu sana aiseee sasa material yote yale ununue bado uje kusimamia namna wanavyojenga duh
Tafuta mtu akusimamie, ila ukipata fundi mzuri sio lazima umsimamie. Mara nyingi utasimamia ili vipimo visizidi au vipungue. Mfano jamvi unaeza patana 500k la nchi 5 ila likamiminwa la nchi tatu.
 
Sawa Fundi mahiri wa ujenzi
 
Tafuta mtu akusimamie, ila ukipata fundi mzuri sio lazima umsimamie. Mara nyingi utasimamia ili vipimo visizidi au vipungue. Mfano jamvi unaeza patana 500k la nchi 5 ila likamiminwa la nchi tatu.
Huyo wa kusimamia ndo jipu yaani itabidi kabla ujenzi aujaanza mtu upate abc za namna ujenzi unavyokuwa na gharama estimate ya kila material. Ili hata ukimuweka mtu na wewe uwepo aisee
 
Huyo wa kusimamia ndo jipu yaani itabidi kabla ujenzi aujaanza mtu upate abc za namna ujenzi unavyokuwa na gharama estimate ya kila material. Ili hata ukimuweka mtu na wewe uwepo aisee
Toa shaka we tafta fundi muaminifu maana wapo.
 
Juzi kuna fundi nimemuamini nikamuacha sait, kuna mtu nilimuweka aniangalizie. Fundi kamimina shimo kumbe kapunja nondo nyingine kaficha. Nimeshikwa na hasira hapa nina mpango wa kuvunja niongezee nondo nimimine upya. Nimejuta sijawahi kupata hasara mpaka namalizia lakini hii ya sasa hivi kiboko.
 
Ulimlipa vzr.? 🤣
 
Sijapitia hoi situation lakini ni kweli

Kwa maoni yangu kuna haja na hawa watu kusajiliwa kuwa na ofisi zinazotambulika inakuwa rahisi kuishtaki ofisi kuliko kushtaki mtu mmoja ambaye ni ngumu kumkamata

Hawa watu wengi wao wamekuwa hasa za wizi na uongo , kongole kwa wale waaminifu
 
Nunua appartment , hzi pesa ni makaratasi tuu , NHC , Palm village na kwingineko , ulaya hakuna mtu anayejenga , mashirika yanajenga kazi yako ni kununua ama kupanga ... Ujenzi ni suluba tuuu
 
Mafundi tunadharaulika sana, kwa mujibu wa comment kwenye uzi huu hakuna mtu thamani yake kwenye kazi ni ndogo zaidi ya fundi.
Nashuhudia hilo nikiwa fundi zaidi ya miaka kumi na Tano.

Tunekua watu wakujitoa ili mkae mazingira mazuri na bora sisi mkitupa ujira mdogo, nyie mna baki kwenye nyumba zenu sisi tunaishia kupanga, mnakalia na kulalia furniture nzuri sisi tunalala chini na kukalia vigoda, nyumba zenu zina milango mizuri zetu ni milango ya bati!.

Hela mnazotupa zinaisha kabla ya kazi hata kuisha nyie mna baki kilicho bora sis tunaishia kuwa maskini , hata Asante hakuna mnaishia kututukana na kutubeza!
 
Kweli kabisa Mkuu, halafu unakuwa na amani sana ila fundi anajitahidi kufanya kazi vizuri ili asikukwaze.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…