sumbai
JF-Expert Member
- Jun 16, 2014
- 19,955
- 45,207
SASA mkuu Kwa wale ambao ubize ni 24/7 inakuwaje?? Yaan hata ukiweka kampuni ya ujenzi inabidi uwepo pia kufuatilia Kama nondo wamelaza Kwa usahihi.Tusiwalaumu mafundi tu, hii ni tabia ya watanzania kwa ujumla wetu, huko serikalini ni wizi na ufisadi tu, popote watu wakipata nafasi wanaiba tu.
Muhimu ni, kuwa na ABC za ujenzi, simamia kazi yako mwanzo mwisho, hakikisha unafatilia materials mwenyewe...hii ya kumwambia fundi waambie jamaa walete mchanga fuso moja, waambie washushe tofali 1000 ndio utaanza kuchapwa hapo hapo.
Kuna Ile unafuatilia Ila huna maarifa ya ujenzi haha mafundi wanakutajia vifaa Kwa kingereza mara ringbeam mara sijui vitu gani.....
Kwenye mitaala labda hata na hili somo la mambo ya ujenzi lingekuwepo Kwa sababu katika maisha zaidi ya asilimia 70 ya watu hupitia hatua ya kujenga. Kuliko kujifunza mambo ya mtemi mirambo na chief samore toure
Wenzetu nje wanajengaje?? Hivi wale wakina rashford nawao wanshindaga site kusimamia?? Labda tungejifunza kupitia wenzetu.