Kujiajiri kunaweza kuwa utumwa, mwaka wa tatu huu bampa to bampa kuamka alfajiri kurudi usiku, sina muda wa kutosha hata wa kupumzika na mtoto wangu

Pole mkuu
 
Funga biashara mkuu, upate muda wa kupumzika.

Mwaka wa tatu kwanini hutafuti mbinu ya kudhibiti mauzo na bidhaa zako ili uweke msaidi upate muda wa kupumzika!?

Au ni biashara inayokuhitaji wewe Kwa asilimia mia Moja Kila ikiwa wazi?
Watanzania kweli ni wavivu, wenzenu Japan mtu anafanya kazi masaa 16 kwa siku na hawalalamiki. Mijitu mivivu tu.
 
Umesema wewe huna muda kwahiyo sishangai . jipe muda maana ya kujiajiri ni ipi siku ukiitambua utaelewa nilichoimanisha . Kujiajiri sio utumwa bali ni kujituma sa kama umejiajiri na unaona utumwa we bado maana ulikuwa umeajiliwa afu unahisi kujiajiri ni simple
 
Bora kujiajiri ....
Bora kuajiriwaa.....
Bora kuajiariwa na uwe na biashara ya pembenii.....
Etc
Mapambano ya maisha Kila uchaoo
Bora kuajiriwa halafu uwe na mambo Yako
Mfano mie mwalimu ikija siku nikapata Uafisa Elimu Kata,nakuwa nimemaliza Kila kitu

uAEK hauna mambo mengi na stress ni zero,nakuwa huru kufanya mambo yangu,mshahara unalingia na Niko huru kufanya biashara zangu plus posho ya 250,0000 Kila mwezi ya Uafisa Elimu Kata na pikipiki juu
 
Una masaa 24 ndani ya siku.
Umetumia jumla masaa 12.
Still una masaa 12 yamebaki
Ukilala masaa 8 still yatabaki masaa 4

Kama umezaliwa mwanaume lazima upambane kila siku mpk utakapoondoka duniani.

Jitambue wewe ni nani, halafu piga kazi.
(Kazi kazi mkuu)
 
Kweli mkuu apambane asije akajaribu upompoma kama ule wa mpwayungu village
 
Mkuu kama umeona kuamka asubh ni utumwa kujiajiri hasa kwenye biashara basi ni utumwa mara 1000 nalala sa 7 naamka sa 11, kwa maana hyo ukiacha kz ukajarbu kujiajiri utakataa tamaa kbsa.
 
Me naona utumwa unatengenezwa kwanza na mtu mwenyewe.
 
Bora umeongea wewe,mimi huu mwaka wa pili sijui kama kuna weekend. Ni utumwa askwambie mtu,serikali iangalie iwapatie vijana ajira. watu wanateseka sana na ndoa zenyewe zinavunjika kila kukicha kwasababu ukipumzika tu pesa ya matumizi hakuna na ukisema ujitume na kazi yenyewe unaonekana uko bize na umeitenga familia
 
Inabidi ujipange na pia kujitoa. Ukikaa nyumbani hakuna pesa itaingia siku hiyo, ila kama umeamua kuutumia huo muda na familia, kuna umuhimu na thamani yake pia. Ukiwa na mtazamo wa lazima upate pesa kila siku, basi familia nayo utaisikia tu kama ambavyo nayo itakusikia tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…