Kujiajiri kunaweza kuwa utumwa, mwaka wa tatu huu bampa to bampa kuamka alfajiri kurudi usiku, sina muda wa kutosha hata wa kupumzika na mtoto wangu

Kujiajiri kunaweza kuwa utumwa, mwaka wa tatu huu bampa to bampa kuamka alfajiri kurudi usiku, sina muda wa kutosha hata wa kupumzika na mtoto wangu

Duh.
Ujumbe ushatumwa.
Hao, wanakuja. #Kataakujiajiri
#Vaenivaenibaibui
#Usikubalimagofu
#Usikimbizeupepo
#Siolaananihakiilakuuandio
#Utawasikiahaofreemasonhuyo
😌
🤬
 
Uhuru wa kuwa na muda wa kufanya mambo yako nao una umuhimu aisee.

Utamu wa ngoma ingia ucheze, usilewe na maneno matamu ya motivational speakers kujidanganya kwamba kila mtu aliejiajiri anaweza kuamua aamke saa ngapi, aende likizo wiki nzima mbugani, n.k. haya mambo wanaoyaweza ni kundi la watu wachache waliojiajiri, hapa utawakuta kina Mo, Bakhresa, na matajiri wengine walio invest ama kuweza kuajiri watu wa kusimamia miradi yao,

Kiuhalisia huku kwenye kujiajiri kundi kubwa ni day workers, yani hakuna uhuru wa kusema leo nilale hadi saa nne, nipumzike weekend nzima, niende likizo mbugani, n.k. yani kuamka ni almost kila siku asubuhi na kurudi ni usiku, hatupendi lakini inatulazimu

Ni mwaka wa tatu huu kwenda ofisini saa moja kurudi saa moja ama mbili ni mwendo mdundo bampa to bampa,

Naweza kusema nna nafuu siku pekee ya kumpumzika ni jumapili tu, nje ya hapo labda krismas na pasaka imeisha hio.

Muda wa kurudi ndio hivyo tena ni usiku yani hata kupata muda wa kuspend na mwanangu unakuwa limited, nikifika mimi nimechoka nae anakaribia kwenda kulala.
Ukiangalia vizuri utakuta hata mtoto si wako.
 
Hivi hayo mambo watu wanasemaga ni mambo gani? Utasikia...unapata muda wa kutosha kufanya mambo yako...

Kujiajiri au kuajiriwa hakuna tofauti, maana in each case ni lazima ufanye kazi.

Hii ni tofauti na kuwekeza (investment) ambapo unaweka mpunga mahali halafu huo mpunga unakuletea mpunga zaidi...bila kufanya chochote. Kwa mfano unaweza wekeza kwenye hisa za makampuni au bond etc.

Pia kuna ujasiriamali. Mjasiliamali anaweza kuwa amejiajiri au ameajiri au vyote viwili kwa pamoja.
 
Funga biashara mkuu, upate muda wa kupumzika.

Mwaka wa tatu kwanini hutafuti mbinu ya kudhibiti mauzo na bidhaa zako ili uweke msaidi upate muda wa kupumzika!?

Au ni biashara inayokuhitaji wewe Kwa asilimia mia Moja Kila ikiwa wazi?
Kama biashara inamuhitaji kila siku hana tofaut na aliyeajiliwa
 
Uhuru wa kuwa na muda wa kufanya mambo yako nao una umuhimu aisee.

Utamu wa ngoma ingia ucheze, usilewe na maneno matamu ya motivational speakers kujidanganya kwamba kila mtu aliejiajiri anaweza kuamua aamke saa ngapi, aende likizo wiki nzima mbugani, n.k. haya mambo wanaoyaweza ni kundi la watu wachache waliojiajiri, hapa utawakuta kina Mo, Bakhresa, na matajiri wengine walio invest ama kuweza kuajiri watu wa kusimamia miradi yao,

Kiuhalisia huku kwenye kujiajiri kundi kubwa ni day workers, yani hakuna uhuru wa kusema leo nilale hadi saa nne, nipumzike weekend nzima, niende likizo mbugani, n.k. yani kuamka ni almost kila siku asubuhi na kurudi ni usiku, hatupendi lakini inatulazimu

Ni mwaka wa tatu huu kwenda ofisini saa moja kurudi saa moja ama mbili ni mwendo mdundo bampa to bampa,

Naweza kusema nna nafuu siku pekee ya kumpumzika ni jumapili tu, nje ya hapo labda krismas na pasaka imeisha hio.

Muda wa kurudi ndio hivyo tena ni usiku yani hata kupata muda wa kuspend na mwanangu unakuwa limited, nikifika mimi nimechoka nae anakaribia kwenda kulala.
Mkuu kinacho tusumbua wengi ni financial education kujiajiri(self employee) ni sawa au ni kugumu kuliko kuajiriwa.
Ukisha fikia kwenye level ya kuwa na biashara(busness) au investment hapo ndio hela inaanza kuingia bila wewe kuteseka.
Wengi wanachanganya kuajiriwa, kujiajiri, biashara na uwekezaji.
 
Watanzania wavivu sana wenzetu washaacha kupumzika weekend na kufanya kazi masaa 8 huko ni 24/7 wanakimbizana.
 
Mimi nashangaa mtu anayedhani kujiajiri ndio kupata nafasi ya kupumzika
Ukiona mtu anapumzika ujue ameshaweka mahesabu sawa faida na hasara anajua zinatoka wapi hivyo biashara inaweza kujiendesha yenyewe pasipo yeye kuwepo kila siku
 
Back
Top Bottom