Kujiajiri ni utumwa zaidi ya kuajiriwa, waliojiajiri wengi wanakosea kujiweka kundi moja na wamiliki wa biashara

endelea kuajiriawa mkuu.....tuache na yetu.....
 
Wote tupo kwenye rat race.... Tofauti ni madaraja tu, kuna walioajiriwa wanakula maisha safi sawa na wafanya biashara waliofanikiwa, na wapo wadaraja la chini wana unga unga tu maisha sawa na wafanyabiara wanao pambana.....

Ila biashara ukiiotea inakuvusha kanani asubui asubui, wakati kazin ukionekana una mafanikio bos anaanza uchunguzi wap kuna vuja....

Stay on your lane!...
 
Mkuu toka jaana naona upo busy na kupinga waliojiajiri , wamekukosea nini? Halafu unapotoa mfano wa waliojiajiri kwa nini unachagua team za mchangani?
Atakuwa alikuwa mwajiriwa akadanganywa na motivation speaker na akaacha kazi akaenda jiajiri mtaji ukakata so ni aina fulani ya kujutia hivi.
Kasahau mafanikio ya kujiajiri ni stage,
 
Dogo naona baada ya vitasa vya Jana umebadili maelezo lakini.....same shit different toilet! Jipange kabla hujapangwa.
 
Waliojiajiri wengi ni watumwa wa biashara zao Wala Haina ubishi. Tafakari mtu anaduka, kazini anaingia saa Moja anatoka saa nne usiku Kila siku kwa wiki mwaka mzima. Sasa huyu c ni mtumwa wa kujiajiri? Wanaofurahia kujiajiri ni wachache kama ilivyo walioajiriwa wanaoinjoy ni wachache
 
So unatoa maoni au elimu gani juu ya swala kama hili au ume laumu pasina kuacha faida yoyote
 
Ww utakuwa mgonjwa wa akili......
wahi hospitali kabla mambo hayajaharibika zaidi
 
hiyo ni ratiba tu ya kufanya kazi kama mtumwa ili uishi kama mfalme utumwa ni pale unapopangiwa na bosi wako kazi ambayo hauipendi lakini kwa njaa zako unalazimika uifanye tu mfano mimi miaka mnne iliyopita nilikuwa dereva wa bajaj ya mkataba nilikuwa naamka SAA 11 alfajiri mpaka saa4 usiku nikamaliza mkataba kwa sasa naamka muda nitakao na ninampango wa kuongeza bajaj ya pili na nina duka

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
 
Salary addiction plus .
Acha kukwepa majukumu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…