miamiatz
JF-Expert Member
- Dec 4, 2017
- 505
- 941
Katika harakati za kujiajiri kuna mambo manne ambayo endapo yataweza kukutana kwa pamoja basi suala la kujiajiri na kukua kijasiriamali litakuwa kama baraka kwako. Mambo hayo ni:
a. Wazo sahihi
b. Wakati sahihi
c. Sehemu sahihi
d. Uwepo wa rasilimali sahihi
Wazo sahihi la biashara ni hatua namba moja ya kufikia mafanikio katika suala la ujasiriamali.
Ila wazo sahihi lililopatikana wakati usio sahihi basi linakuwa sio wazo sahihi tena. Ila pia kama wazo lenyewe limezaliwa wakati sahihi ila sehemu yenyewe sio sahihi basi wazo hilo pia huwa si sahihi tena mpaka litapopelekwa sehemu sahihi.
Kila wazo la kijasiriamali huhitaji rasilimali fedha na rasilimali nyenginezo kutekelezwa. Bila kuwa na rasilimali sahihi basi wazo hubaki kuwa fikra tu.
Kwa wale wanaopambana kujiajiri katika ujasiriamali itakuwa wamewahi jikuta katika mtego huu. Kuna wakati una wazo zuri na linahitaji ulifanye sehemu flani afu unahangaikia kupata ofisi ama fremu katika eneo hilo madalali wanahangaika wanakosa ofisi katika eneo hilo na wanakupeleka mtaa mwingine.
Kama ilivyo shida kupata nyumba ya kuishi sehemu unayoitaka yenye kiwango unachokitaka kwa bajeti uliyojiwekea ndivyo pia ilivyo kwa ofisi ya ujasiriamali.
Kuna wakati unaweza jikuta una mtaji na una wazo zuri na ni wakati mzuri ila sehemu unayopaswa kuliweka wazo lako unaikosa badala yake unapata sehemu nyengine ambayo haifai kwa wazo hilo.
Sasa nini cha kufanya kutatua changamoto hii? Maoni yenu ni muhimu wadau wote wenye uzoefu wa kukumbana na jambo hili. Kwa uzoefu wangu nimejifunza mambo kadhaa wakati wa kutafuta wazo sahihi la biashara:
Kwanza inabidi kuwa na mawazo kadhaa badala ya kuwa na wazo moja hata kama una mtaji mkononi.
Pili mawazo yako ya biashara yanapaswa kuzaliwa katika field yaani katika pita pita zako mitaani badala ya mawazo hayo kuzaliwa ukiwa chumbani ama ofisini kwako. Wazo linalozaliwa katika field ni wazo ambalo unapita sehemu unaona fursa na unaona eneo linalofaa kuweka ofisi yako na unauliza unaambiwa linaweza kupatikana.
Tatu yafaa kujua kila kiasi cha pesa chaweza kuwa mtaji tosha ama kisiwe mtaji tosha kulingana na namna unavyoliunda wazo lako. Kuna ambao kwao laki ni mtaji hali ya kuwa kwa mwingine hata milioni kumi anaona bado sio mtaji bali ni senti.
Nasubiri mawazo yenu wadau mnashauri nini cha kufanya kukabiliana na jambo hili.
#KukuzaMaarifa #KuongezaUstawi #miamiatz
Sent using Jamii Forums mobile app