Kujiajiri: Wazo sahihi, wakati sahihi, sehemu sahihi na uwepo wa rasilimali sahihi

Kujiajiri: Wazo sahihi, wakati sahihi, sehemu sahihi na uwepo wa rasilimali sahihi

Tafuta maarifa kabla ya kuanza mkuu .. kunachangamoto huko ila changamoto ndo kazi yenyewe.
Wewe kama mjasiriamali ingekuwa vizuri kama ungenipa maarifa muhimu kabisa nayotakiwa kuwa nayo kabla sijafanya maamuzi yoyote kwenye biashara
 
Wewe kama mjasiriamali ingekuwa vizuri kama ungenipa maarifa muhimu kabisa nayotakiwa kuwa nayo kabla sijafanya maamuzi yoyote kwenye biashara
1. Sijui uliko kuna fursa zipi ...
2. Sijui una ujuzi upi ...
3. Sijui una mtaji kiasi gani ...
Kuna kitu kinaitwa SWOT analysis ambacho kitakusaidia wewe kujua kama kweli unafaa kuwa mjasiriamali au la!
 
1. Sijui uliko kuna fursa zipi ...
2. Sijui una ujuzi upi ...
3. Sijui una mtaji kiasi gani ...
Kuna kitu kinaitwa SWOT analysis ambacho kitakusaidia wewe kujua kama kweli unafaa kuwa mjasiriamali au la!
Asilimia kubwa jamii za Ki TZ zinafanana lengo langu Mimi nikupata uelewa in general sio mbaya ukanifafanulia hata kupitia fursa unazoziona eneo ulipo huko.
 
Asilimia kubwa jamii za Ki TZ zinafanana lengo langu Mimi nikupata uelewa in general sio mbaya ukanifafanulia hata kupitia fursa unazoziona eneo ulipo huko.
Ok,
Kwenye ufugaji - wafugaji wengi wana changamoto ya malisho ... tengeneza biashara ya malisho kwa ajili ya mifugo kwa kuandaa mazingira ya kupunguza gharama na karaha za wakata majani...

Kwenye elimu: Masomo mengi yanafundishwa kwa English lakini vijana wengi hawajui lugha hiyo - wafundishe lugha hiyo kwa ubunifu ili waelewe waweze kuyamudu masomo mengine ..

Kwenye maji: Anza biashara ya kusambaza maji kwa waliokuzunguka.

Nishati: Tengeneza mazingira ya kusambaza nishati mbadala ya Tanesco

Chakula: Tengeneza mazingira ya kusindika vyakula ili vitumike kipindi cha uhaba.

Yako mengi ila utakaloliona linakufaa ndo unaanza kulitafutia maarifa yake ... yapo tu mkuu.
 
Ebu niwaeleze kitu hapa ...
Hapa duniani kila mtu yuko kivyake kama vile unavyojua kila computer ilivyo na serial number tofauti na nyenzake - hivyo hivyo kila mwanadamu ana SIRI yake ya kufanikiwa maishani. Kitu ambacho ni huru kwa kila mtu ni maarifa. Namna ya kuyatumia ndo hapo kila mtu anakuwa na utofauti wake ... nitoe mfano:-
Nilianza kufuga baada ya kusoma ile post ya kufuga kuku 6 ukafikisha 200 ... nilienda hadi wakafika 160, hivi ... kuna jamaa alikuja kwangu akaomba nimuuzie mbegu ... nikamuuzia na kumpatika pamphlet ya ufugaji. Baada ya miezi sita aliponikaribisha kwake ... nilimkuta ana kuku zaidi ya 1000; amewaachia kwenye fance - wengi kweli kweli.
Yeye alipokuwa anaulizwa alisema mwalimu wangu ni Tutor B; lakini walionitembelea kwangu walikuta wamepungua hata hawazidi 20;
Hapa kuna kitu nilijifunza toka kwa huyo niliyemfundisha.
1. Shughuli unayoifanya wewe - ifanye wewe kweli kweli kwa ukaribu - ukimwachia mtu hutajua ni wapi kakosea. Mimi niliwaachia vijana wangu baada ya kuona kuwa ninakoelekea ni kuzuri kumbe wao wakaharibu.

2. Yaliyoandikwa kwenye vitabu yana mchango karibia 45%; 55% inakuhitaji wewe mwenyewe ufanye utafiti wa kina kujua namna ya kufika walau 90% ya mafanikio yako.
 
Nimeajiriwa na nimejiajiri ila kuajiriwa kulikoma mwaka jana september baada ya maradhi kunikubili kwa muda mrefu ambayo mpaka sasa bado napambana nayo. Kiukweli waajiri ni wanyanyasaji sana. Nilipata ajali nikidrive kutokea job kwenda home afu madhara yakawa ndani kwa ndani kwenye uti wa mgongo maeneo ya shingo afu madokta wakasema nipumzike kwa muda mrefu ila mwajiri alikuwa hata nikijaza fomu ya likizo ananuna badala ya kusaini. Kuajiriwa na private companies nako kuna changamoto nyingi sana.

Najuta kuajiriwa na muajiri huyo wakati biashara zangu zilikuwa zikienda hata kabla hajaniajiri.

Nilitaka kufata historia ya Mengi. Miaka kadhaa ambayo mzee huyu alikuwa anaendesha IPP na kadhalika pia alikuwa akitumikia ajira kama Director kwenye baadhi ya taasisi nyenginezo.

Bahati mbaya ajira kwangu ilinidhoofisha na kunijeruhi si kama yeye ilimneemesha na kumuimarisha.

Nahisi mengine ni privacy labda iwe person to person.

Sent using Jamii Forums mobile app
Pole sana ndugu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yah utapona tu. May God bless you.
Yeap ubongo upo sawa kabisa. Mkanda wa gari na airbag zinasaidia sana. Kikubwa kilitokea wataalam wa afya huita whiplash injury. Na shingo iliathirika sana bila kujijua sehemu ya uti wa mgongo eneo la shingo iliathirika zaidi na kupelekea ubongo kukosa mawasiliano ya uhakika toka mwili ulio chini ya shingo. Hii hupelekea numbness kwa baadhi ya nyakati, loss of energy, na kuanguka wakati mwingine, pia kushindwa kuconcentrate. But napambana na maradhi kwa kasi sana na bila shaka yataisha mana dalili ni njema.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom