Kujiandikisha Ili upige kura ni kurasimisha uharamia wa CCM katika uchaguzi

Kujiandikisha Ili upige kura ni kurasimisha uharamia wa CCM katika uchaguzi

BOB LUSE

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2014
Posts
3,738
Reaction score
3,199
CCM imejipanga kukalia viti Kwa hila, hata kumwaga damu na kupoteza watu kama tulivyo shuhudia Mwaka huu.

Ni ujinga wa Hali ya juu kwenda kupanga foleni, ujiandikishe, upige kura wakati CCM wameshaandaa nani atashinda wakisaidiwa na vyombo vya Dola.

Vizuri, tuwaachie wenyewe, ndani yao wauwane, wapotezane na wapige kura.

Usipoteze muda kubariki uchaguzi ambao, refa ni Mchezaji.
 
Situliqmbiwa 80% ya wananchi miaka hiyo walisemaga CCM iendelee. Wapinzani wakiwekwa tu kwa lazima ili kufurahisha wazungu. Kama ni kweli basi CCM ikishinda chini ya 80% huwa imeibiwa. Au wanaoipenda walikuwa bize hawakuwa na Muda wa kwenda kuwapigia au kujiandikisha.
 
Kulasimisha*Kurasimisha

Endelea kuhamasisha wenzako wasiajindikishe lakini kumbuka siku ya kupiga kura wanapiga wale walijiandikisha tu na hapo ndio CCM itatoa kipigo cha mbwa koko
 
Vizuri,tuwaachie wenyewe, ndani yao wauwane,wapotezane na wapige kura.
wakiwa peke yao hawatauana, watapeana vyeo kila mmoja atulie. Pendekeza wapinzani wafanye nini, siyo kususia. Sema tunahitaji civil war!
 
CCM imejipanga kukalia viti Kwa hila,hata kumwaga damu na kupoteza watu kama tulivyo shuhudia Mwaka huu.

Ni ujinga wa Hali ya juu kwenda kupanga foleni,ujiandikishe,upige kura wakati CCM wameshaandaa nani atashinda wakisaidiwa na vyombo vya Dola.

Vizuri,tuwaachie wenyewe, ndani yao wauwane,wapotezane na wapige kura.
Usipoteze muda kubariki uchaguzi ambao,refa ni Mchezaji.
Ni kweli mengi yanatokea wakati wa uchaguzi. Ila tuwe na matumaini kuwa wingi wetu unaweza kufanya wizi/udhalimu wao usifanye kazi. TWENDE KUJIANDIKISHA.
 
Ni kweli mengi yanatokea wakati wa uchaguzi. Ila tuwe na matumaini kuwa wingi wetu unaweza kufanya wizi/udhalimu wao usifanye kazi. TWENDE KUJIANDIKISHA.
Niliwahi enda uchaguzi wa Mwisho wa Serikali za mitaa,mtaani kwetu,walijua diwani aliyekuwepo na Mwenyekiti, hatuwataki, wakatangaza kuwa karatasi za kupigia kura zimeisha, hatukupiga mpaka Mwisho! Kwanini nikapoteze muda Tena?
 
CCM imejipanga kukalia viti Kwa hila, hata kumwaga damu na kupoteza watu kama tulivyo shuhudia Mwaka huu.

Ni ujinga wa Hali ya juu kwenda kupanga foleni, ujiandikishe, upige kura wakati CCM wameshaandaa nani atashinda wakisaidiwa na vyombo vya Dola.

Vizuri, tuwaachie wenyewe, ndani yao wauwane, wapotezane na wapige kura.

Usipoteze muda kubariki uchaguzi ambao, refa ni Mchezaji.
Wewe hufai katika maendeleo ya demokrasia hapa nchini.. Hii mada ni ya hovyo kuliko mada zote zilizoanzishwa mwaka huu.. Mods Maxence Melo Naomba mada hii ifutwe.. Hatupo hapa JF kuhamasisha watu wasijiandikishe kupiga kura..
 
Kulasimisha*Kurasimisha

Endelea kuhamasisha wenzako wasiajindikishe lakini kumbuka siku ya kupiga kura wanapiga wale walijiandikisha tu na hapo ndio CCM itatoa kipigo cha mbwa koko
Kipigo cha mbwa koko ni mfumo wa maisha wanaotutawala nao kila siku. Bila shaka hapo ulipo mkoa mzima wanatawala CCM.
Sina muda na uchaguzi, bize shambani kutafuta pesa ya kununua Panadol.
 
Upuuzi ni Wewe kutojiandikisha huku ukijiaminisha kua unaikomoa serikali ianyoongozwa na CCM kumbe ndio kwanza unaipa ushindi wa kishindo
acha ujinga nenda kajiandikishe na upige kura ni wajibu wako kikatiba
 
Back
Top Bottom