“Kujigamba” sio njia sahihi ya kuanzisha urafiki na Afrika

“Kujigamba” sio njia sahihi ya kuanzisha urafiki na Afrika

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
1663760879361.png

Mkutano wa kilele wa kutafuta fedha za kukabiliana na mabadiliko ya tambianchi barani Afrika umefanyika hivi karibuni mjini Rotterdam, Uholanzi, na kuhudhuriwa na viongozi wa nchi sita za Afrika, lakini kwa upande wa nchi za Magharibi, ni waziri mkuu wa Uholanzi pekee ndio amehudhuria mkutano huo. Kitendo hiki cha nchi za Magharibi kwa mara nyingine tena kimethibitisha kuwa hazitaki kufuata kanuni ya usawa na heshima katika kuendeleza uhusiano na nchi za Afrika.

Mkutano wa kuisaidia Afrika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ulioandaliwa na Kituo cha Kimataifa cha Mabadiliko (Global Adaptation Center) cha Uholanzi ulifanyika tarehe tano Septemba. Viongozi walioalikwa kutoka nchi sita za Afrika zikiwemo Senegal, Ghana, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Ethiopia wote walikwenda Ulaya kuhudhuria mkutano huo. Lakini wakati huohuo, licha ya mwaliko kutoka kwa waziri mkuu wa Uholanzi ambayo ni nchi mwenyeji wa mkutano huo, viongozi wote walioalikwa kutoka nchi za Magharibi zikiwemo Ufaransa, Canada na Finland hawakuwepo.

Hali hii haikuwapendeza viongozi wa Afrika. Akizungumza kwenye mkutano huo, Rais Macky Sall wa Senegal ambaye pia ni mwenyekiti wa zamu wa Umoja wa Afrika ameeleza kusikitishwa kwake na kutokana na viongozi wengi wa nchi zilizoendelea kiviwanda kutohudhuria mkutano huo. Rais Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) pia alikosoa vikali kutokuwepo kwa viongozi wa nchi za Magharibi. Ameeleza kuwa mabadiliko ya tabianchi haswa yanatokana na nchi za magharibi, na kwamba Afrika ilichangia kidogo sana katika tatizo hilo, lakini sasa ndio kanda inayoathiriwa zaidi na mabadiliko hayo.
98330572477242bc8a43cf7064a1047a.png


Hii si mara ya kwanza kwa nchi za Magharibi kujigamba mbele ya nchi za Afrika. Kwenye Mkutano wa Kilele wa Umoja wa Ulaya na Afrika uliofanyika mjini Brussels mwezi Februari mwaka huu, takriban viongozi 40 wa Afrika walikusanyika, lakini baadhi ya wakati, ni Waziri Mkuu wa Ubelgiji pekee alikuwa pamoja nao.

Katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na maendeleo ya kasi ya uhusiano kati ya Afrika na China, ushawishi wa nchi za Magharibi unazidi kupungua siku hadi siku. Ili kubadilisha hali hiyo, nchi za Magharibi zimetangaza hatua mbalimbali. Hata hivyo, nchi hizo zimeshindwa kuacha tabia ya kujigamba kwa nchi za Afrika, na daima zinachukulia Afrika kama eneo lililo nyuma kimaendeleo, na inaonekana ni vigumu kwao kuzitendea nchi za Afrika kwa usawa. Licha ya hayo, nchi za Magharibi zinailazimisha Afrika kufuata utaratibu wao wa kisiasa na hata utamaduni wao. Katika masuala ya kimataifa, nchi za Magharibi pia hupenda kunyooshea vidole na kulazimisha Afrika kufanya mambo ambayo nchi hizo zinazotaka. Kwa mfano, hivi karibuni nchi za Magharibi zililazimisha nchi za Afrika kuilaani Russia kufuatia mgogoro kati yake na Ukraine, jambo ambalo nchi za Afrika hazikufanya.

Afrika sasa sio eneo la kikoloni tena, na ni bara linaloendelea kwa kasi, na linastahili kuheshimiwa na kutendewa kwa usawa. Nchi za Magharibi lazima ziache tabia yake ya kujigamba, ili kuendeleza kihalisi uhusiano wake na nchi za Afrika.
 
Hii habari ni kama mmnawafokea ingali mkijua hakuna mmagharibi anasoma huo uzi… waste of time.
 
Back
Top Bottom