Mwanasayansi Kalivubha
JF-Expert Member
- Feb 4, 2024
- 344
- 926
Kuchelewa sio nadharia bali kupo ila inatakiwa udhibiti hisia za kuchelewa ili usijipoteze zaidi
Zipo sababu nyingi zinafanya watu wachelewe ila bila kujali kuwa ulicheleweshwa au ulijichelesha ni muhimu kuwa na utulivu zaidi hasa pale unapojiona kuchelewa.
Kushindwa kudhibiti hisia za kuchelewa kumefanya watu wengi wakurupukie gari lolote hata kama haliwafikishi waendapo na yote hii ni hofu inayoletwa na HISIA ZA KUCHELEWA.
Watu wengi hasa wakike wameamua kuolewa na yoyote ilimradi mwanaume kwa sababu tu wamejiona kuchelewa na ile hofu imewasukuma wavamie yoyote hali inayoleta majuto baadaye kwa wengi.
Usipodhibiti hisia za kuchelewa utajikuta unakosea zaidi kwenye maamuzi kwa sababu utachagua kwa pupa ukidhani usipofanya hivyo utakosa tena na hapo utajikuta kwenye chaguo baya zaidi.
Unapojiona tayari umechelewa kwanza kubali huo ukweli kisha tulia ili katika maamuzi yako yasikufanye uchelewe tena zaidi.
#Mwanasayansi Saul Kalivubha.
#Fikia Ndoto Zako