Kujilinda/ kujihami kwa sasa ni lazima

Kujilinda/ kujihami kwa sasa ni lazima

Mushkov

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2024
Posts
667
Reaction score
1,403
Kutokana na vitendo vya kuvamia, kuteka na kuumiza watu hasa wakosoaji wa serikali kushamiri, kwa sasa wakati umefika ili kila Kiongozi mpigania uhuru wa kweli wa Nchi kulindwa na kujilinda kwa mbinu na njia zote. Ni muhimu kuwa na kikosi cha siri cha kuwalinda wapambanaji hasa walio katika hatari ya kufanyiwa ubaya wowote.

Lakini pia nashauri kila Mtanzania mpenda ma mpigania haki asikae kifara, awe na mbinu za kujihami.
Ukikuta kuna mtu/watu wanakunyemelea kutaka kukuteka au kukufanyia ujinga wowote ule, hakikisha unajihami kwa nguvu zote na kwa kutumia mbinu na njia za kisasa kabisa.

Tukiwashikisha adabu wachache tu, hakuna mtu atathubutu kutusogelea.

Kamwe tusiruhusu tena Mtanzania yeyote kutekwa au kushambuliwa kizembe bila mtekaji huyo kunyonyolewa.
 
Back
Top Bottom