Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
KUJIONA MTOTO MDOGO KUMEWAFELISHA WENGI!
Anaandika, Robert Heriel.
Yule Shahidi.
Aliyekuambia miaka 20 ni mtoto ni Nani?
Wakati kuna wenzako wamekuwa Wafalme, Marais, Mawaziri, na wapo wenye Wake na Watoto katika umri huohuo!
Kuna kundi kubwa la watu lime-Relax kabisa Kwa kisingizio kuwa bado ni wao ni watoto wadogo.
Sipo hapa kama Motivation Speaker asiyejua nini anasema, kila neno nitakaloandika hapa nimelipima, na sasa nalitolea Hesabu yake.
Licha ya kuwa Mimi ni Mwanafalsafa, mwanafasihi lakini pia ni mfanyabiashara. Hivyo naongea Kwa uzoefu hata Kama wapo wataoona Nina uzoefu mdogo lakini siku zote wenye hekima na akili hujifunza Kwa mambo madogo madogo, katika uzoefu mdogo mdogo, kamwe mtu hawezi jifunza katika uzoefu Mkubwa Kama alishindwa katika uzoefu mdogo.
Kauli ya "Mimi bado mtoto mdogo" ina maana kuu zifuatazo;
i. "Ninamuda wa kutosha".
Jambo ambalo sio Kweli. Hii inafanya wengi kutokufanya mambo ya maana hata kama wananafasi ya kufanya hivyo kisa wanajiona watoto.
Unakuta kijana anafuja Mali au pesa azipatazo kisa anajiona anaomuda mwingi tuu huko Baadaye.
Au unakuta kijana hajishughulishi kazi kuwaza mambo ya kitoto toto, sijui kuvaa vizuri, Kula bata, hata kama Hana kazi.
ii. " Mimi siwezi kufanya/Sina uwezo wa kufanya"
Kauli ya Mimi bado mtoto mdogo inamaana ya kuwa Mimi sina nguvu, Mimi siwezi, Mimi sina bado sijakomaa kufanya mambo makubwa.
Kwa hiyo nahitaji msaada, bila kusaidiwa sidhani Kama nitaweza.
Kauli hii pia hujikita katika mtu kujikosoa Kama anamapungufu ya kimaumbile Kama mlemavu, kiziwi, kipofu, au mapungufu ya kiuchumi Kama vile Hana mtaji, au katoka familia Masikini, au Hana Ujuzi wala elimu.
Kauli hii ni kisingizio au lawama ambazo mtu humtupia mtu mwingine au sababu nyingine au Jambo jingine.
iii. " nilicho nacho hakitoshi, ni kidogo"
Wengi wanaosema wao bado ni watoto wadogo hurejelea maana ya kuona vitu walivyo nao bado ni vidunchu tuu. Wala haiviwezi kufanya lolote. Jambo ambalo sio Kweli.
Mtaji wangu ni mdogo, kipaji changu ni kichanga wengeni watanicheka. Dooh!
Hakuna kitu kidogo na kamwe usipende kuona vitu katika macho ya udogo. Dunia hakunaga dogo.
Kumbuka wewe mwenyewe ulikuwa Tone la Shahawa tuu. Kama Jambo hilo halitakufundisha maana ya maisha basi Taikon sina mfano mwingine.
Mjane wa Serepta alipokutana Eliya akasema;
1 Wafalme 17:12
Naye akasema, Kama BWANA, Mungu wako, aishivyo, sina mkate, ila konzi ya unga katika pipa, na mafuta kidogo katika chupa; nami ninaokota kuni mbili ili niingie nijipikie nafsi yangu na mwanangu, tuule tukafe.
Kisa hiki unaweza ukaenda kukifuatilia wewe mwenyewe. Utajifunza zaidi kuliko nitakavyoeleza hapa.
Mfano No:01 KISINGIZIO CHA UMRI
Lawama hizi aliwahi kuzitoa Nabii Jeremia, zingatia maneno yaliyokolezwa;
Yeremia 1:4
Neno la BWANA lilinijia, kusema,
Yeremia 1:5
Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.
Yeremia 1:6
Ndipo niliposema, Aa, Bwana MUNGU! Tazama, siwezi kusema; maana mimi ni mtoto.
Mfano No. 02. KISINGIZIO CHA MAUMBILE.
HIki alikitolea Nabii Musa akitaka kukimbia kazi anayotaka kupewa na Mungu, Zingatia maneno yaliyokolezwa,
Kutoka 4:10
Musa akamwambia BWANA Ee Bwana, mimi si msemaji, tokea zamani, wala tokea hapo uliposema na mtumishi wako; maana mimi si mwepesi wa kusema, na ulimi wangu ni mzito.
Kutoka 4:11
BWANA akamwambia, Ni nani aliyekifanya kinywa cha mwanadamu? Au ni nani afanyaye mtu kuwa bubu au kiziwi, au mwenye kuona, au kuwa kipofu? Si mimi, BWANA?
Mfano No 03. KISINGIZIO CHA KIMAZINGARA NA WATU WA ENEO FULANI.
Hapa nitamtolea mfano Nabii Yona,
Yona anapewa kazi kwenda Ninawi, anakimbilia Tarshishi Kwa kisingizio cha watu wa Ninawi walivyo Makatili, waovu hivyo aliogopa kuuawa au kudhuriwa na watu Wale.
Mifano hiyo inatosha,
Elewa mambo Yafuatayo;
I. Umri wako sio sababu ya kufanya ushindwe kufanya mambo makubwa.
Anza na kidogo ulichokuwa nacho. Kama ni kipaji kitumie hata kama unaona hakuna wa kukusapoti. Fanya hivyohivyo.
Umri mdogo haukuzuii kufanya biashara isipokuwa unakusaidia kujifunza biashara ungali kijana Mdogo. Usisubiri uwe mtu mzima ndio ujifunze Kazi Fulani au biashara Fulani.
ii. Tumia kidogo ulicho nacho. Anza na kidogo.
Tumia kidogo ulichonacho, usiangalie mapungufu yako kama alivyoangalia Nabii Musa, akaambiwa atumie Fimbo kukomboa Waisrael😂😂.
Ndio inachekesha Kwa sababu, Misri ni taifa, linaulinzi na silaha za kila namna, lakini Musa anaambiwa aende na fimbo yake tuu kukomboa ndugu zake. Kitakachokomboa watu sio Ile fimbo au silaha aliyoibeba Musa isipokuwa MTAZAMO na FALSAFA.
Wote waliofanikiwa wanafanana Jambo moja kuu, Spirit, mtazamo na falsafa. Hata kama watatumia njia tofauti lakini mambo hayo matatu wanafanana.
iii. Yatawale mazingira na wanaokuzunguka.
Ni kweli huna mtaji,
Ni kweli hauna jina,
Ni kweli kuna wafanyabiashara wakubwa, ma-Godfather, waliotawala field yako.
Ni kweli huna connection,
Lakini hizo hazitoshi kuwa sababu za kukuzuia kufanikiwa.
Mtu anashindwa kutokea ndani mwake na sio nje yake. Vivyohivyo, mtu anashinda kutokea ndani mwake na sio nje.
Unapoanzisha Jambo lolote lile usipende kuangalia ni changamoto gani utakumbana nazo, Anza Jambo hilo bila kuwaza hizo changamoto kisha kuwa mstahimilivu, lazima utoboe.
Jambo lolote unaloanza kuliangalia Kwa jicho la kuona vizingiti utakavyokutana navyo mara nyingi hutolianza.
Kama unataka kufanya biashara fanya, sijui mambo ya Kodi utajulia mbele Kwa mbele, sijui mambo ya wateja utajulia mbele Kwa mbele.
Unapopambana adui yake kabla hujaangalia Ubora wake, Anza Kwanza kuangalia mapungufu yake. Hiyo itakufanya upate nguvu zaidi ya kukabiliana naye.
Adui yeyote unayeanza kuangalia ubora wake atakupigia kutokana na kukujengea hofu. Hofu itakufanya usipigane Kwa akili na utulivu.
Musa alipotuma Wapelelezi 12 kwenda kuupeleleza Yericko, wapelelezi 10 walileta Ripoti hii;
Hesabu 13:32
Wakawaletea wana wa Israeli habari mbaya ya ile nchi waliyoipeleleza, wakasema, Ile nchi tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi inayowala watu wanaoikaa; na watu wote tuliowaona ndani yake ni watu warefu mno.
Hesabu 13:33
Kisha, huko tuliwaona Wanefili, wana wa Anaki, waliotoka kwa hao Wanefili; tukajiona nafsi zetu kuwa kama mapanzi; nao ndivyo walivyotuona sisi.
😂😂😂😂 Unasikia Ripoti Hiyo; hao ni wapelelezi 10 wanatoa Ripoti.
Ripoti hiyo inawanyong'onyesha Waisrael na wanashindwa kabla hawajaanza.
Lakini Watu wawili nao no Joshua na Kalebu wanatoa Ripoti yao kivyao😀 kana kwamba walienda sehemu mbili tofauti.
Ripoti ya Joshua na Kalebu inasema;
Hesabu 14:6
Na Yoshua mwana wa Nuni, na Kalebu mwana wa Yefune, waliokuwa miongoni mwao walioipeleleza nchi, wakararua nguo zao;
Hesabu 14:7
wakanena na mkutano wote wa wana wa Israeli wakasema, Nchi ile tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi njema mno ya ajabu.
Hesabu 14:8
Ikiwa BWANA anatufurahia, atatuingiza katika nchi hii atupe iwe yetu, nayo ni nchi yenye wingi wa maziwa na asali.
Hesabu 14:9
Lakini msimwasi BWANA, wala msiwaogope wale wenyeji wa nchi, maana wao ni chakula kwetu; uvuli uliokuwa juu yao umeondolewa, naye BWANA yu pamoja nasi; msiwaogope.
Ripoti hiyo ilirejesha Imani na nguvu Kwa Waisrael.
Joshua na Kalebu badala ya kuangalia ukubwa wa maadui zao, wao waliangalia Uzuri wa nchi Ile kuwa inawafaa, pili waliona kuwa tayari Watu wa nchi Ile Wanahofu Kwa habari walizozisikia kuwahusu Waisrael.
Mwisho Wale Wapelezi 10 walioleta Hofu waliuawa ili kuepusha wasijewakasambaza siku ya hofu miongoni mwa watu.
Taikon hajasema uue mtu anayejua hofu Ila ninakuambia mtu yeyote anayependa kukukatisha tamaa ni Bora umpunguze kwenye Circle yako. Asiwe karibu yako.
Ogopa tabia na fikra za kujiona mtoto, huwezi au bado unamuda wa kutosha.
Ningeweza kuandika zaidi lakini Kwa sasa niishie hapa, nisiwachoshe Sana.
Ulikuwa na Yule Mtibeli.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam