DOKEZO Kujiondoa kwa Majeshi ya Africa Kusini nchini Msumbiji na kuiacha Tanzania na Rwanda dhidi ya kundi la kigaidi la Ansar al-Sunna kuna maana gani?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Hiyo itakua vita ngumu sana na umoja wa mataifa hauwezi ruhusu!

Zanzibar tu inaishinda sembuse kuikalia nchi nyingine au kui annex
Na ndio maana hii nchi tunahitaji kuwa na kiongozi Mwamba haswa amiri jeshi mwenye amri nzito kwa masilahi ya taifa. Maendeleo ya kweli hayaji kwa kujifungia chumbani. Hatuhitaji kuwa na viongozi wanasiasa tena.
 
Hakuna faida yoyote ile kama bado mfumo ni ule ule katika nchi hii. Utachukua madini na gesi lakini wanufaika watakuwa si wananchi bali viongozi uchwara.
 
Hii ina maana sasa askari wa nchi zilizobaki waendelee kuuawa na hao magaidi bila huruma.
 
Hakuna faida yoyote ile kama bado mfumo ni ule ule katika nchi hii. Utachukua madini na gesi lakini wanufaika watakuwa si wananchi bali viongozi uchwara.
Sio kwamba hakuna faida itakayopatikana, kikubwa hatuna hao viongozi wa shoka kwa sasa. Huo ufisadi wenyewe unatokana na viongozi wa kisiasa kufanya siasa ni kazi na sio wito kwa ajili ya kulitumikia taifa. Ipo siku atapatikana kiongozi atakayebadilisha hii mifumo na siasa isiwe tena kimbilio la wasaka utajiri.
 
Rwanda itatumia msumbiji kuivuruga tanzania hasa ukizingatia inamiona tanzania kama aduni katika mpango wake wa kuzitibua nchi zote za maziwa makuu ili yenyewe ionekane ndo kisiwa cha amani
Usigeuze hisia ukafanya ndio uhalisia. Ho kamwe halitatokea. Uhudiano wa Tanzania na Msumbiji kamwe hauwezi kuvunjika, kutetereka au kusuasua kwani umejengwa kwa misingi ya kindugu na uliasisiwa tangu enzi ya Mondllz eĺlpll
Rwanda itatumia msumbiji kuivuruga tanzania hasa ukizingatia inamiona tanzania kama aduni katika mpango wake wa kuzitibua nchi zote za maziwa makuu ili yenyewe ionekane ndo kisiwa cha amani
Sio sahihi. Msumbiji kamwe haiwezi kuisaliti Tanzania. Mahusiano yetu ni ya kidugu yaliyojengwa tangu enzi ya Mondlane na Nyerere. Ndio maana hata mwenge wa uhuru wa Tanzania ulikimbizwa Msumbiji mara tu baada ya uhuru. Hivyo Rwanda hawezi ruhusiwa kuitumia ardhi ya Msumbiji kuhujumu Tanzania.
 
Hawana maslahi nako na hawana mpaka upande wa Kaskazini,Tanzania ndio Huwa wajinga tunawapa watu service ya Bure.

Huu upuuzi ni WA tangu enzi ya Nyerere,tuko DRC na Mozambique Sasa sijui tunanufaika na nini ,si Bora tubakie tunalinda kwenye mipaka yetu?
 
Kulinda kwene mipaka ni uzaifu strength ni kushambulia any possible attack!!

Kifupi huwezi kulinda mipakani huku ukimuacha adaui ajipange nadhan umeona jinsi hamas walivowafanya israel ndo scenario za ivo
 
Mkuu hamna mahusiano kwen maslahi

Upunguze hisia……
Kuna leak moja nishaisoma inaelezea hiko kitu anachokisema jamaa
 
Inavyoonekana wa-Tanzania wengi sana siyo watu wa kufanya utafiti kuhusiana na mambo mengi ya Migogoro iliyopo ktk nchi zetu hizi za Afrika. Mgogoro uliopo nchini Msumbiji SIYO KWELI kwamba ni mgogoro wa kidini au masuala ya Ugaidi unaoambatana na masuala ya dini, hususani dini ya kiislamu, the answer is NO. Ule purely ni Mgogoro wa kisiasa utokanao na watawala wa nchi hiyo ya Msumbiji (FRELIMO) kushindwa kuongoza Watu (wananchi) vizuri, matokeo yake wakazalisha vurugu hizi zinazoendelea hivi sasa.
Fanyeni tafiti zenu vizuri ili muweze kubaini kiini hasa Cha kuibuka kwa Mgogoro huo. Mgogoro huo una historia ndefu kidogo, na kwa bahati mbaya sana hata sisi wa-Tanzania (Utawala wa CCM ) nao ni chanzo kimojawapo Cha kuasisi Mgogoro huo wa huko Msumbiji. Na ukibahatika kuwasikia wenyewe Raia wa Msumbiji ambao ni wahusika hasa wa Mgogoro huo(yaani Watu wafuasi wa chama Cha RENAMO kinachopingana na Utawala wa FRELIMO) utaona wanaeleza Wazi kabisa kwamba Maadui zao wakubwa kwenye huo Mgogoro ni Utawala wa FRELIMO ya Msumbiji na Utawala wa CCM ya Tanzania, yaani hawafichi kabisa kuhusu suala hili. Wapiganaji wa RENAMO wanaamini kwa dhati kabisa kwamba bila ya Mwl. Nyerere na CCM yake kuisaidia FRELIMO katikà Vita vyao, basi Chama Cha RENAMO kingeshika madaraka na kuwa chama Tawala nchini Msumbiji, CCM ndio imekuwa kikwazo kwao RENAMO Cha kuweza kuwa chama Tawala. Sisi wa-Tanzania tunahesabiwa Kama maadui kwenye huo Mgogoro wa huko Msumbiji hususani kutokana kitendo cha Utawala wa CCM kuisaidia Sana Serikali ya FRELIMO kwenye masuala ya vita.
 
Mkuu ugaidi ni ugaidi kama ni mgogoro ni kati ya nani na nani??
Tofautisha kundi la kigaidi na mgogoro!!

Kundi linavuka msumbiji linavuka nchi linakuja tanzania linauwa watu wanarudi msumbiji hafu unasema si ugaidi!!

Mkuu jielimishe kuhusu haya maswala yamkini hujui ugaidi ni nini

Ni kweli serikali ya msumbiji iliyatelekeza kimaendeleo maeneo hayo ya kaskazini lakin hilo halifanyi kikundi kilichopo kutokua n kikundi cha kigaidi!!

Kundi lolote la kigaidi ili liweze kukua linahitaji
-Vijana wasio na elimu
-vijana wasio na ajira
-umasikini uliokithiri
-Uwepo hafifu wa serikali maeneo husika
-itikadi za kidini
-uwezo wa kurecruit wapiganaji
-network ya pesa na siraha
Makundi yote ya kigaidi yamezaliwa kwene mazingira yanayofanana
 
R
Rudia kusoma Tena hiyo comment yangu, Kuna maelezo ya nyongeza nimeweka.
Aidha, fanya kwanza utafiti wako wa kina juu ya suala hili. Usikurupuke kuandika vitu
 
Unaweza kuweka source yako inayoeleza chanzo cha mgogoro huo kuwa wa kisiasa kati ya RENAMO na FRELIMO?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…