Inavyoonekana wa-Tanzania wengi sana siyo watu wa kufanya utafiti kuhusiana na mambo mengi ya Migogoro iliyopo ktk nchi zetu hizi za Afrika. Mgogoro uliopo nchini Msumbiji SIYO KWELI kwamba ni mgogoro wa kidini au masuala ya Ugaidi unaoambatana na masuala ya dini, hususani dini ya kiislamu, the answer is NO. Ule purely ni Mgogoro wa kisiasa utokanao na watawala wa nchi hiyo ya Msumbiji (FRELIMO) kushindwa kuongoza Watu (wananchi) vizuri, matokeo yake wakazalisha vurugu hizi zinazoendelea hivi sasa.
Fanyeni tafiti zenu vizuri ili muweze kubaini kiini hasa Cha kuibuka kwa Mgogoro huo. Mgogoro huo una historia ndefu kidogo, na kwa bahati mbaya sana hata sisi wa-Tanzania (Utawala wa CCM ) nao ni chanzo kimojawapo Cha kuasisi Mgogoro huo wa huko Msumbiji. Na ukibahatika kuwasikia wenyewe Raia wa Msumbiji ambao ni wahusika hasa wa Mgogoro huo(yaani Watu wafuasi wa chama Cha RENAMO kinachopingana na Utawala wa FRELIMO) utaona wanaeleza Wazi kabisa kwamba Maadui zao wakubwa kwenye huo Mgogoro ni Utawala wa FRELIMO ya Msumbiji na Utawala wa CCM ya Tanzania, yaani hawafichi kabisa kuhusu suala hili. Wapiganaji wa RENAMO wanaamiki kwa dhati kabisa kwamba bila ya Mwl. Nyerere na CCM yake kuisaidia FRELIMO katikà Vita vyao, basi Chama Cha RENAMO kingeshika madaraka na kuwa chama Tawala nchini Msumbiji, CCM ndio imekuwa kikwazo kwao RENAMO Cha kuweza kuwa chama Tawala. Sisi wa-Tanzania tunahesabiwa Kama maadui kwenye huo Mgogoro wa huko Msumbiji hususani kutokana kitendo cha Utawala wa CCM kuisaidia Sana Serikali ya FRELIMO kwenye masuala ya vita.