DOKEZO Kujiondoa kwa Majeshi ya Africa Kusini nchini Msumbiji na kuiacha Tanzania na Rwanda dhidi ya kundi la kigaidi la Ansar al-Sunna kuna maana gani?

DOKEZO Kujiondoa kwa Majeshi ya Africa Kusini nchini Msumbiji na kuiacha Tanzania na Rwanda dhidi ya kundi la kigaidi la Ansar al-Sunna kuna maana gani?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Umesema msumbiji ilitawaliwa na mkoloni mreno,
Vyama vya ukombozi vilivyopigania uhuru ni RENAMO na FLERIMO,
Baada ya uhuru FLERIMO kashika dola RENAMO akatengwa,
Ukaibuka mvutano wa RENAMO na FLERIMO,
FLERIMO akaenda kusini RENAMO kaskazini kama kikundi cha waasi,

Vurigu zinatokana na gesi ya kaskazini upande wa FLERIMO RENAMO wanaitaka,
Tatizo sio udini.

Swali kwako je RENAMO na FLERIMO si ni kama CUF na CHADEMA?

Mmoja anawakristo wengi mwingine waislamu wengi?
 
Abbreviation
RENAMO
Leader
Ossufo Momade
Chairman
André Magibire
Founded
1975
Headquarters
Avenida Ahmed Sekou Touré Nº 657, Maputo
Youth wing
RENAMO Youth League
Ideology
Mozambican nationalism
Conservatism
Economic liberalism
Anti-communism
Political position
Centre-right[1] to right-wing
 
Renamo ni ya Mwaka 1975 mkuu,
Ilianzishwa na viongozi waliojitoa FLERIMO, maafisa wa usalama,
Wakipinga sera ya ujamaa,

Nadhani msingi wa vurugu ulianzia kwenye kupinga ujamaa.

Issue ya uislam labda ilikuja baadae
 
Shida huelewi!!
Africa should fight as one national siyo hizo izo idea zako za Cat eating Cats
Afrika hii,yenye matabaka yasiyoelewana wala kufungamana ngumu sana kuungana nakuwa moja hilo sahau,dini,ukanda,kabila na hali za kiuchumi zimewatawanya waafrika kamwe hawewezi kuwa wamoja.
 
Rwanda itatumia msumbiji kuivuruga tanzania hasa ukizingatia inamiona tanzania kama aduni katika mpango wake wa kuzitibua nchi zote za maziwa makuu ili yenyewe ionekane ndo kisiwa cha amani
Hapana, siyo kweli.
Kwa sasa hivi, Mozambique ipo stable na mandate ya SADC ni mpaka December mwaka huu.
SANDF wanaondka na watachukua nafasi ya MONUSCO Congo, ila kwa mandate ya tofauti. Mandate ya kupigana na ku-disable vikundi vya kigaidi.
Tanzania pia, itaongeza troops Congo. Lengo kubwa ni kuondoa M23 na offensive zimeanza wiki hii from FARDC.
Vikosi vya SADC mpaka sasa havilipwi Mozambique, kuviweka kule ni upotevu wa hela.
 
Ukichunguza kwa umakini Sana utagundua kwamba yale maeneo karibia yote yenye vurugu kule Msumbiji yana historia kongwe sana kuhusiana na suala la vurugu za kisiasa, hata kabla ya Taifa hilo la Msumbiji halijapata uhuru wake kutoka kwa mkoloni wao Ureno. Kambi nyingi sana za Makundi ya kisiasa ya Wapigania Uhuru wa nchi hiyo ya Msumbiji ziliwekwa katika ukanda huo wa Kaskazini mwa nchi hiyo, maeneo ambayo hadi leo hii bado yanaendelea kukumbwa na vurugu. Makundi ya Wapigania Uhuru ya vyama vya Siasa vya FRELIMO na RENAMO vilikuwa na Kambi zao nyingi za wazi na za siri kubwa ktk maeneo hayo yenye vurugu kwa sasa. Baada ya kufanikisha suala la kuuangusha utawala wa mkoloni wao Ureno, maeneo hayo tayari yalikuwa yamevurugwa vibaya sana na vita vya ukombozi, miundombinu yote ya kujenga uchumi kama vile viwanda viliharabiwa kabisa na mapigano ya vita.
Mbaya zaidi, hata chama cha Siasa cha FRELIMO kilipofanikiwa kushika madaraka ktk nchi hiyo ya Msumbiji, haikukishirikisha Chama cha RENAMO ktk kuitawala nchi hiyo ya Msumbiji, badala yake vyama hivyo viligawanyika na kuwa vyama vinavyohasimiana, vikapigana vita tena wao kwa wao ili kugombea kupata udhibiti wa madaraka ktk nchi hiyo, hatimaye Chama cha RENAMO kilizidiwa nguvu na kushindwa vita. Chama cha FRELIMO kutokana na msaada mkubwa waliopata kutoka kwa Mwl. J. K. Nyerere na CCM yake, walifanikiwa kuhodhi na kudhibiti mamlaka na madaraka yote ya nchi hiyo ya Msumbiji, na RENAMO kikawa Chama kikuu cha Upinzani dhidi ya FRELIMO.
Mbaya zaidi tena, utawala wa FRELIMO ulikichukulia Chama cha RENAMO kama Kundi la Waasi wala siyo Chama cha Siasa, Matokeo yake Wanachama na Wapiganaji wa RENAMO wakakimbilia msituni na kuweka Kambi zao nyingi za Siri kwenye huo Upande wa Kaskazini mwa nchi hiyo ya Msumbiji.

Serikali ya Msumbiji Kama ililitelekeza kabisa kwa muda mrefu eneo hilo lililopo Kaskazini mwa nchi hiyo kwa sababu ililiona kama eneo lenye maficho ya Waasi wa RENAMO, hata huduma za kijamii zilikuwa duni sana kwenye maeneo hayo. Wananchi wengi wa upande huo wa Kaskazini mwa nchi waliona kama Serikali ya Msumbiji imewatenga na haikuwa inawajali. Serikali ilijichimbia mizizi kwenye eneo la Kusini mwa nchi hiyo ya Msumbiji na kuigawa nchi ktk mapande mawili ya Kaskazini na Kusini. Serikali hiyo ya Msumbiji ilirudi tena kwa kasi upande wa Kaskazini mwa nchi hiyo baada ya Ugunduzi wa Nishati ya Gesi kwenye maeneo hayo ya Kaskazini, hapo ndipo ukawa mwanzo mpya wa kuibuka kwa Vurugu hizi zinazoendelea hivi sasa ktk eneo hilo la Kaskazini mwa nchi hiyo ya Msumbiji.

Suala la Dini au Udini ktk vurugu hizo za huko Msumbiji linatumika tu na wahusika kama "SCAPEGOAT" ili kuweza kupata msaada wa kijeshi na wa silaha za kupigania vita dhidi ya maadui zao.
Mkuu Kuna nondo muhimu sana unazo kuhusu mgogoro huu,kwa heshima nakuomba anzisha Uzi au kama usha andika Uzi weka humu watu wapitie nondo zako.
 
Ndio yaan tanzania sasa itapigana na majeshi ya rwanda na kundi la magaidi kwa wakati mmoja..
Na hii nchi ilivo na rushwa kazi ipo uzembe uzembe utakua na madhara makubwa sana
Kile ki nchi ni kidogo sana kwa tz hakiiwezi, ili waiweze labda ni hadi watapoivuruga intellijensia ya tz kwa kupenyeza watu wao ( na sidhani kama kuna uzembe kiasi hicho) kinyume na hapo itabaki kuwa propaganda tu.
 
Kile ki nchi ni kidogo sana kwa tz hakiiwezi, ili waiweze labda ni hadi watapoivuruga intellijensia ya tz kwa kupenyeza watu wao ( na sidhani kama kuna uzembe kiasi hicho) kinyume na hapo itabaki kuwa propaganda tu.
Kama wanaweza ivuruga DRC wanashindwaje Tz!! nchi iliyojaa rushwa
 
Kile ki nchi ni kidogo sana kwa tz hakiiwezi, ili waiweze labda ni hadi watapoivuruga intellijensia ya tz kwa kupenyeza watu wao ( na sidhani kama kuna uzembe kiasi hicho) kinyume na hapo itabaki kuwa propaganda tu.
Daima akili nzuri iliyotulia ndiyo inayoleta matokeo mazuri.

"Ukubwa wa pua siyo wingi wa kamasi"

'Aheri ng'ombe Saba walio wanono kuliko ng'ombe elfu Saba walio wadhaifu.'

Nafikiri nimeeleweka.
 
Daima akili nzuri iliyotulia ndiyo inayoleta matokeo mazuri.

"Ukubwa wa pua siyo wingi wa kamasi"

'Aheri ng'ombe Saba walio wanono kuliko ng'ombe elfu Saba walio wadhaifu.'

Nafikiri nimeeleweka.
Ok nimekuelewa, je unafikiri uwezo wao wa akili ni mkubwa kulinganisha na uwezo wa wa tz, nipe facts maana siamini kama wana uwezo huo hata kiakili.

Wanachoweza kutuzidi ni uzalendo na ndio silaha kubwa wakiitumia kila kitu kinawezekana.
 
Ok nimekuelewa, je unafikiri uwezo wao wa akili ni mkubwa kulinganisha na uwezo wa wa tz, nipe facts maana siamini kama wana uwezo huo hata kiakili.

Wanachoweza kutuzidi ni uzalendo na ndio silaha kubwa wakiitumia kila kitu kinawezekana.
Hawajazidi kwa uzalendo bali ni propaganda
 
Hayo makundi yote ya kigaidi yanayopewa majina ya Kiislam ni makundi hanayoundwa na nchi za magharibi kiustadi wa ujasusi na wanatumi a tamaa za wajinga wenye njaa ili waendelee kuchota mali za Afrika.

Wajinga ndiyo waliwao.
Kuutenganisha uislamu na ugaidi ni sawa na kutajrib kutenganisa moyo na damu,

Kwahiyo waislamu safi wakoradhi kutumiwa na makafiri kuuana na kuumiza watu wengine?na kuendela kuuchafua uislam
 
Ok nimekuelewa, je unafikiri uwezo wao wa akili ni mkubwa kulinganisha na uwezo wa wa tz, nipe facts maana siamini kama wana uwezo huo hata kiakili.

Wanachoweza kutuzidi ni uzalendo na ndio silaha kubwa wakiitumia kila kitu kinawezekana.
Na uzalendo hawana
Kilichopo ni ukizingua wanakuua kwaiyo kuna mambo watu hawafanyi kwasababu wanaogopa kufa!!
 
Inavyoonekana wa-Tanzania wengi sana siyo watu wa kufanya utafiti kuhusiana na mambo mengi ya Migogoro iliyopo ktk nchi zetu hizi za Afrika. Mgogoro uliopo nchini Msumbiji SIYO KWELI kwamba ni mgogoro wa kidini au masuala ya Ugaidi unaoambatana na masuala ya dini, hususani dini ya kiislamu, the answer is NO. Ule purely ni Mgogoro wa kisiasa utokanao na watawala wa nchi hiyo ya Msumbiji (FRELIMO) kushindwa kuongoza Watu (wananchi) vizuri, matokeo yake wakazalisha vurugu hizi zinazoendelea hivi sasa.
Fanyeni tafiti zenu vizuri ili muweze kubaini kiini hasa Cha kuibuka kwa Mgogoro huo. Mgogoro huo una historia ndefu kidogo, na kwa bahati mbaya sana hata sisi wa-Tanzania (Utawala wa CCM ) nao ni chanzo kimojawapo Cha kuasisi Mgogoro huo wa huko Msumbiji. Na ukibahatika kuwasikia wenyewe Raia wa Msumbiji ambao ni wahusika hasa wa Mgogoro huo(yaani Watu wafuasi wa chama Cha RENAMO kinachopingana na Utawala wa FRELIMO) utaona wanaeleza Wazi kabisa kwamba Maadui zao wakubwa kwenye huo Mgogoro ni Utawala wa FRELIMO ya Msumbiji na Utawala wa CCM ya Tanzania, yaani hawafichi kabisa kuhusu suala hili. Wapiganaji wa RENAMO wanaamini kwa dhati kabisa kwamba bila ya Mwl. Nyerere na CCM yake kuisaidia FRELIMO katikà Vita vyao, basi Chama Cha RENAMO kingeshika madaraka na kuwa chama Tawala nchini Msumbiji, CCM ndio imekuwa kikwazo kwao RENAMO Cha kuweza kuwa chama Tawala. Sisi wa-Tanzania tunahesabiwa Kama maadui kwenye huo Mgogoro wa huko Msumbiji hususani kutokana kitendo cha Utawala wa CCM kuisaidia Sana Serikali ya FRELIMO kwenye masuala ya vita.
Ule ni ugaidi wa waisilamu
 
Back
Top Bottom