Habari wanabodi? Ni matumaini yangu kwamba hamjambo humu ndani na mnaendelea na harakati za mapambano ya kuzuia ugonjwa wa corona. Kiukweli inabidi tumuombe Mungu wetu ili atusaidie tushinde haya mapambano.
Wanabodi kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu, nimegundua kwamba Zitto Kabwe ana uwezo mdogo sana wa kuchanganua mambo, ni mtu muongo sana na mpotoshaji mkubwa wa umma.
Jana Prof. Janabi aliandaa Hand over note kwa wafanyakazi waliochini yake ya a kuwapangia majukumu yao. Ghafla Mh. zito Kabwe akutuma ujumbe katika mtandao wa twita wa kupotosha na kudanganya Umma kuwa Prof. Janabi amefukuzwa kazi kutokana na voice note ya Prof. Janabi iliyokuwa iiliyozagaa siku chache zilizopita kwenye makundi ya mtandao wa whatSapp kuwaelimisha na kuwakumbusha watu namna ya kujikinga na ugonjwa wa korona.
Kutokana na hilo tukio la kupotosha watu kuwa Prof. Janabi amefukukuzwa limesababisha nimuone Mh. Zitto Kabwe kama ni msomi wa hovyo sana na mtu ambaye bado hajaelimika, anapenda kukurupuka, pia ana uwezo mdogo sana wa kuchanganua mambo, haelewi lugha ya Kiingereza vizuri.
Wasomi wana viwango vyao mfano msomi akipata taarifa yoyote lazima afanye utafiti ili kuwa na uhakika na habari aliyopewa. Pia lazima azingatie ni nani aliyetoa hiyo taarifa kwa kuangalia na kuzingatia chanzo cha habari hiyo(CREDIBLE SOURCE). Kwa ndugu yetu Zitto Kabwe imekuwa ni tofauti sana kwa sababu amedhihirisha kiwango kikubwa cha ujinga wake.
Wanabodi wenzangu, najaribu kujiuliza ni mambo mangapi amepotosha na kudanya umma huyu mwanasiasa uchwara kama alivyoitwa na RC wa Dar es salaam? wanabodi watu kama hawa ni hatari sana katika jamii kama jamii haitachukua jukumu la kuwakanya. Watakuja kusababisha majanga makubwa sana kwa jamii kwa sababu ya uongo wao, uwezo wao mdogo wa kuchanganua mambo na ukurupukaji wao.
Hivyo wanabodi naomba tushirikiane kupiga kelele ili mamlaka husika wawachukulie hatua hawa Zitto Kabwe na Mwenzake JOHN MREMA kwa kwa kutoa habari za uongo ambazo zimesababisha upotoshaji kwa Umma.
Karibuni kwa michango
Ahsanteni.