Habari wana jf napenda kutanguliza huu uzi kama ulivyoandikwa hapo juu. Najua kuna baazi ya watu hawawezi kunielewa. Ila ukweli upo hivi kukaa kijijin kwa kijana unaejitafuta kimaisha ni kufeli na nasema hivi kwasbabu nazoziona mimi.
Cha kwanza.... KUZUNGUKWA NA WATU WASIOSAHIHI NA WENYE MITAZAMO HASI.
Kijijini watu wengi hawaamin kuish ndoto zao na wanaamin kila aliyefanikiwa ni mchawi, freemason,jambazi.. na kila ukijaribu kufanya kitu tofaut na mila za hapo kijijin. Wengi hawaamin unaweza kufanikiwa watakukatisha sana tamaaa
2.KUDUMAA AKILI NA KULIZIKA MAPEMA.
kijijni ukimilki pikpik tu wanaanza kukuita boss kitu ambacho kinalufanya ujionee umefanikiwa na kulizika mapema.
Pia hata mazingira hayaruhusu mtu ukue kiuchumi unakosa sehem ya kutizamia au role model tofaut na mjin
3.MZUNGUKO WA PESA NI MDOGO SANA
Kijjn ni rahis sana kuuwa pesa ukifungua biashara kutokana na mzunguko. Pesa huja mara moja tu wakat wa mavuno na kuna baazi ya biashara kama nguo baazi ya wanakijij huwa na dhana kwamba kununua nguo mpka sikukuu au safari. Na ukinunua nguo bila kuzingatia hivo vitu husema unaharibu pesa au unatumia pesa ovyo
5.KUKOSA NDOTO ZOZOTE
kijijin mtu akiamka asubuh anaenda shamba na akirud shamb anawaza aoge akae kijiweni apige stori bas siku imeisha. Na kubishana na vitu visivokuwa na msingi na kupiga umbea
Kiufupi yapo mengi yanayomzuia mtu kukua na kuwa na mtazamo chanya ila kwa machache ndo hayo
NB.ushauri wangu kama unajitafuta kimaisha usikae kijijini sana ni bora uanze na level za wilaya
ILA KUKAA VIJIJINI VIJANA WENZANGU NI KUFELI KIJIJINI HAKUNA MAENDELEO NA NDO MAANA HAKUNA AFSA BIASHARA WALA MASOKO
KIJIJINI SHUGHULI KUBWA NI KILIMO NA NDO MAANA KUNA AFSA KILIMO
kama una maoni unaweza ukashare ila mi kwa mtazamo wangu upo hivyo
Kwa mtazamo wako (na wale wenye awazo kama yako), uko sahihi ila inafaa utoke nje ya box na uyaangalie maisha ya kijijini kwa kwa mtazamo chanya.
Kumbuka kwamba hivyo vyakula vyote mnavyokula hapo mjini vinatoka kijijini. Siku hizi sio sawa na enzi au zama zile ambapo hakukuwa na mawasiliano. Walio mjini wanawasiliana na walio vijijini kwa simu, email au Whatsapp na biashara inaendelea baina ya mzalishaji na mlaji ndani ya muda mfupi sana. Vijana walio vijijini kama sio wale wavivu na walevi kupindukia wanapiga hela ndefu na sio tu katika msimu wa kilimo bali kwa mwaka mzima kwa kuzingatia shughuli au kipindi. Kijijini huwezi kufanya shughuli -biashara moja tu na ukapata mafanikio. Huku vijijini kuna kila fursa isipokuwa fursa ya Utapeli-uchwara hakuna .
Fursa zilizopo ni e.g.
1. Ufugaji-kibiashara ikiwemo biashara ya mazao ya mifugo -mayai, mifugo hai, nyama, ngozi etc
2. Kilimo-biashara; Unalima kile utakachouza/kina soko la mapema au kulima kwa mkataba mazao ya muda mfupi na yasiyo asilia hapo kijijini e.g. dengu, rozela, mkunazi, Ashwagandha (
Withania somnifera) .n.k
3. Biashara ya duka la rejareja na kuuza vyakula vya mifugo
4. Ufundi e.g. Utengenezaji vifaa vya chuma - grills, uchomeleaji (vijiji vingi kuna umeme)
5.Uanzishaji wa karakana ndogo kutoa huduma za kifundi e.g. Kukarabati/kurepair vifaa vya usafiri (gereji) ref. hakuna kijiji kisicho na bodaboda
6. Utoaji wa huduma ya Lishe e.g. kuweka genge la vyakula - Dagaa, nyanya, vitunguu n.k. au Kuanzisha Bucha n.k.
NB: Fursa huku Vijijini ni nyingi sana - inahitaji tu kijana ajitambue na azitambue fursa zilizopo na kupata ushauri afanye kipi na kwa malengo gani na kwa muda gani.
Vijana wengi hukimbilia mjini kwa kuhadaiwa na vibiashara vya mkononi a.k.a Umachinga, Starehe au kuajiriwa kwenye makampuni au kuajiriwa kwa watu binafsi.